Saturday, March 31, 2012

PICHA MIKUTANO YA KUFUNGA KAMPENI ARUMERU
CCM WAKIFUNGA KAMPENI KWA KUMNADI MGOMBEA SIOI SUMARI ENEO NA KING'ORI.

CHADEMA WAO WALIANZIA USA NA KUFUNGIA TENGERU ..

Jeshi la Polisi Nchini limeanzisha utaratibu mpya wa kuwafanyia askari wake tathimini 

 IGP Saidi Mwema akitoa hotuba yake wakati wa kufunga mafunzo hayo.

Mgeni Rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil

Makachero wapya hao.. 

Jeshi la Polisi Nchini limeanzisha utaratibu mpya wa kuwafanyia askari wake tathimini kila baada ya miaka mitatu kwa ajili ya kuboresha utendaji wa jeshi hilo.

Hayo yalizungumzwa jana na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Saidi Mwema wakati wa kufunga mafunzo kwa askari polisi kwenye chuo cha taaluma cha (CCP)kilichopo Mjini Moshi.

Alisema kuwa tathmini hiyo itatoa nafasi kwa askari polisi ambao watakuwa wanafanya vizuri kuendelea na utandaji ndani ya Jeshi hilo,lakini kwa wale ambao watakuwa hawafanyi vizuri Jeshi hilo litasitisha mkataba wa kuendelea kuwa mtumishi.

Mwema alisema Jeshi hilo limeamua kufanya hivyo ili kuweza kuwatumikia wananchi waliowaajiri kwa uadilifu,pamoja an kuondoa malalamiko ambayo yamekuwepo kwa baadhi ya askari.

Hata hivyo alisema tathmini hiyo,haitawahurumia askari ambao hawatakuwa na sifa,na watanyimwa mikataba ya kuendelea na utumishi,hivyo kutakuwa kwenda kufanya kazi nyingine uraiani.

“Kwa viongozi wa juu wakiwemo Makamanda katika Komandi yoyote,wanatakiwa kuwa waadilifu na kama wataona askari yoyote utendaji wake hauridhishi atoe taairfa kwenye ngazi za juu kwa miezi mitatu ili askari aweze kutoa sababu alisema Mwema.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil alisema licha ya kuwepo kwa mafanikio kwa jeshi hilo ila bado hayajasaidia kupunguza matukio yanayoendelea kulichafua jeshi hilo.

Miongoni mwa matukio ambayo yaliyotajwa na Katibu huyo kwa jeshi la polisi ni pamoja an kuendekea kuwepo kwa matukio kwa askari  kujihusisha na rushwa na kuwabambikia wananchi keshi na kuwatesa raia,vitendo vya utovu wa nidhamu mitaani,ambavyo vinaendelea kuchafua jeshi hilo.

Alisema kuwa kwa Polisi ambao wamekuwa na tabia za utovu wa nidhamu wanatakiwa kuondolewa ili kuendelea kulinda heshima ya jeshi hilo.

Katika mahafali hayo wanafunzi waliofanya mtihani 3264 waliofaulu mtihani walikuwa 3210 na waliofeli ni 54 walipata nafasi ya kufanya mitihani mwingine,na wakifaulu wataingizwa kazini na ambao watashindwa wataenda kutafuta ajira nyingine.


 

Thursday, March 29, 2012

NMB YATOA MSAADA WA VYAKULA NA MAGODORO MONDULI,VYOTE VIKIWA NA DHAMANI YA MILLION 10



MKUU WA WILAYA YA MONDULI JOWIKA KASUNGA,anayeongea,AKIWA KWENYE GARI PAMOJA LENYE MSAADA,AKIWA PAMOJA NA MENEJA WA NMB KANDA YA KASKAZINI VICKY BISHUMBO,wa tau kushoto,akiwa na MKUU WA KITENGO CHA MAHUSIANO  YA KJIJAMII  WA BENK YA NMB BI SHAIROSE BANJI WAPILI wa pili kusoto. 



FAMILIA 27 KATI  YA  2123 ZILIZOKUWA ZIMEATHIRIWA NA MAFURIKO KATIKA BONDE LA MTO WA MBU WILAYANI MONDULI   MKOANI ARUSHA  MWISHONI  MWA MWAKA JANA  ZINAKABILIWA NA HALI NGUMU YA MAISHA NA  ZINAHITAJI MSAADA  WA HALI NA MALI.

MWANDISHI  WETU  RODRICK ,MUSHI ANAYO  TAARIFA ZAIDI 

AKIZUNGUMZA BAADA YA KUPOKEA MSAADA WA  VYAKULA NA VIFAA VYA NDANI YAKIWEMO MAGODORO NA MABLANKETI VILIVYOTOLE NA BENK YA NMB ,MKUU WA WILAYA YA MONDULI  BW JOWIKA KASUNGA AMESEMA  FAMILIA HIZO BADO ZIMEHIFADHIWA  KWA NDUGU NA JAMAA ZAO  NA ZINAISHI KWA KUTEGEMEA MISAADA

WAKIZUNGUMZA  BAADA YA KUKABIDHIMSAADA HUO  MKUU WA KITENGO CHA MAHUSIANO  YA KJIJAMII  WA BENK YA NMB BI SHAIROSE BANJI  NA BAADHI YA WATENDAJI  WA BENK HIYO  WAMEAHIDI KUENDELEA  KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI  KUWASAIDIA WANANCHI HAO

KWA UPANDE WAO BAADHI YA WANANCHI WALIOPATIWA MSAADA HJUO  PAMOJA NA KUISHUKURU BENK HIYO  WAMEWAOMBA WADAU  WENGINE KUJITOLEA KUWASAIDIA

BONDE LA MTO  WA MBU LILILOKO WILAYANI MONDULI MKOANI ARUSHA LILIKUMBWA NA MAFURIKO MAKUBWA MWISHONI MWA MWAKA JANA AMBAYO PAMOJA NA KUSABABISHA MAAFA MAKUBWA BAADHI YA WATU  WALIPOTEZA MAISHA

Mchungaji Msigwa awataka wananchi kumchagua  Nassari akawe'Mbwa mbwekaji Bungeni'

Msigwa akizungumza kwenye mk Mwandishi Wetu, Arumeru


MBUNGE wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, amewatakawananchi wa Jimbo la Arumeru Mashariki, wamchague mgombea wa chama chao kwanini sawa na ‘Mbwa atakaye bweka Bungeni’, kwa kupigania maslahi ya jimbo lao.
 

Akituhubia katika mikutano ya kumnadi mgombe kupitiaCHADEMA Joshua Nassari, jana katika kata za Makiba, Kikwe na  Ngarenanyuki, Mchungaji Msingwa, alisema ilikuweza kupata mwakilishi mwenye uchungu na jimbo hilo ni muhimu wananchiwakaweka itokadi za vyama vyao pembeni na kumchagua mgombea wao.
 

“Bungeni kuna keki ya Taifa, na ili kuipa ni lazimawananchi mumchague Nassari, ili aweze kuipigania kwa maslahi yenu kwa mudamrefu majimbo mengi yaliyokuwa yakiongozwa na wabunge kutoka Chama ChaMapinduzi (CCM),  hayana maendeleo kwaniwengi wao hawana uchungu na maisha ya Watanzania. Leo mimi niko huku Rais Kikwete,amekwenda Iringa katika jimbo ninaloliongoza mimi kama Mbunge kutoka CHADEMA.


“Mradi wa maji alioufungua Iringa ni Sh. Bilioni 75, leoMbunge wa Mtera Livingston Lusinde, nakuja hapa kutukana hebu muulizeni katika jimbolake la Mtera ana maji kiasi gani. Eti CCM wanajenga hoja eti akichaguliwambunge wa upinzani hakuna maendeleo hili si kweli, mchagueni Nassari iliArumeru iweze kupata maendeleo kama ilivyo katika majimbo yetu tunayoyaongozaCHADEMA,” alisema Mchungaji Msigwa.


Aidha alisema kutokana na hali hiyo hivi sasa Atumeruinakabiliwa na ukosefu wa huduma za maji, barabara pamoja na huduma za afya.
Kwa upande wake Meneja Kampeni msaidizi Vicent Nyerere,aliwataka wananchi kutafakari kwa kina kuhusu hatima yao na mahitaji ya jimbohilo kuliko kusilikiza maneno ya CCM ambao muda mwingi wamekuwa wakitukanakatika majukwaa ya siasa badala ya kutangaza sera zao.


Alisema ili kuweza kuondoka na umasiki unaowakabili hivisasa wanahitaji kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua Nassari, ili awezekusimamia miradi ya maendeleo ya jimbo hilo.



Wednesday, March 28, 2012

MAENDELEO YA WANA MERU NI WANA MERU WENYEWE KUAMUA NANI KUWA MUAKILISHI WAO KWENYE UCHAGUZI UTAKAOFANYIKA APRIL 1,JUMAPIL

 Mgombea wa ubunge kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Sioi Sumari,akiomba kura.

 Hapa Sioi Akiombewa na Wazee wa Kimila
Tatizo la Maji kwa wananchi wa Arumeru ni moja ya kero ambazo zimekuwa zikiwakumba wananchi wa Arumeru,na huu ndo wakati wenyewe wa wao kuamua ni Mbunge yupi atakaewatatulia matatizo yao kwenye uchaguzi huu mdogo.

Tuesday, March 27, 2012

                           Nassari, akiomba kura

 


Mgombeaubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joshua Nassari,amewataka wananchi wa Arumeru Mashariki kutoichagua CCM kama ishara yakutoridhiwa na mwenendo wa chama kwa kushindwa kutoa huduma za maendeleoikiwemo maji na umeme.

Alisemakukosekana kwa huduma za jamii kama vile ukosefu wa umeme, elimu bora, afya,maji na migogoro ya ardhi,  sasa ni fursaya pekee kwa wananchi wa jimbo hilo kukataa ahadi mpya za chama tawala CCM na badalayake wahoji utekelezaji wa ahadi za chaguzi zilizotangulia.

 Aidhamgombea huyo ameulinganisha uchaguzi huo kuwa ni sawa na mapambano baina yagiza na nuru, haki dhidi ya dhuluma, haki dhidi ya rushwa na umaskini dhidi yautajiri, huku akidai kuwa CCM kimekuwa kikitumia fedha, kuvunja hakikuwadhulumu wapiga kura haki yao ya msingi kumchagua mgombea wanayemtaka.


                             Mwandishi wetu Arumeru
                                                    ARUMERU KWAWAKA MOTO..

WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo  katika jimbo la Arumeru Mashariki zikipamba moto katika duru ya lala salama,  jana umesambazwa waraka maalum ambao unakihusisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja wanachama wake ambao ni wapambanaji wa ufisadi nchini.

Waraka huo ambao umesambazwa katika mitaa mbalimbali ya Wilaya ya Arumeru umewahusishaWaziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi Dk. HarrisonMwakyembe, munge wa Kahama James Lembeli pamoja na Mbunge wa Same Anne Kilango,wakiwataka wananchi kuwa mamini na uchaguzi huo.

Warakahuo unasema kuwa wao kama makada mahiri ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), walikuwepondani ya chama chao tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere,ambapo kwa wakati huo chama hicho kilikuwa kimbilio la masikini na wanyonge.

Warakahuo mbali na kuzagaa katika mitaa ya mji ya Arumeru na vitogiji vyake piaulikuwa ukigawiwa na katika mikutano ta CHADEMA iliyofanyika katika Kata yaNshupu, na hauna nembo yoyote ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zaidi ya kupewaanuani ya kamati maalum.

Warakahuo ambao umewekwa picha ya viongozi hao walipokuwa katika ibada katika moja yaKanisa la  lililopo Kawe Jijini Dar esSalaam.

Akihutubiamikutano ya kumnadi mgombea Ubunge kupitia CHADEMA, Mwenyekiti wa Taifa wachama hicho Freeman Mbowe, amewataka wananchi wa jimbo hilo kulinda amani nautulivu siku ya uchaguzi kwa kumchagua Joshua Nassari.

Akihutubia mikutano ya kampeni iliyofanyika katika kata  za Nkoasenga, Nshupu, Nguruma, Ndoombo,Urisho na Shambarai Burka, Mbowe, alisema kuwa uchaguzi huo mdogo kumekuwa na vitendo vya hujuma kutoka kwa CCM ambapo hivi sasa wamekuwa wakiandaa makundiya vijana na kuwapiga wanachama wao.

Habari na Mwandishi wetu Arumeru





Sunday, March 25, 2012


CCM yadai kukamata barua ya CHADEMA
  Kinamama wakimshangilia Mgombea Ubunge wa CCM Sioi Sumari katika  kijiji cha Ngongongare,Kata ya Maji ya Chai.

MPANGO wa siri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kuandaa makundi ya vijana watakaofanya fujo kupinga matokeo endapo mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Sioi Sumari atatangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo mdogo, umejulikana.

Mpango huo ambao upo katika barua inayodaiwa kuandikwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Willbroad Slaa, mbali na kuainisha makundi hayo pia imeelezea hofu ya Chama hicho juu ya kushindwa kwenye uchaguzi huo mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki. 

Barua hiyo iliyosomwa jana kwenye mkutano wa kampeni za mgombea ubunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Sioi Sumari na Mratibu wa Kampeni Mwigullu Nchemba ambapo alidai kwamba, Dk. Slaa amekuwa akiwashutumu viongozi wenzake kwa kutumia lugha za matusi kwenye uchaguzi huo mdogo. 

Alidai katika barua hiyo Dk. Slaa amewalalamikia kwa kutumia lugha chafu yakiwemo maneno ya kumkashifu Rais mstaafu Benjamin Mkapa hatua ambayo ilionyesha kutokukomaa katika siasa ikiwa ni pamoja na kukiweka chama hicho kwenye mazingira ya kushindwa.

 “Barua hii ninayoisoma mbele yenu inawaagiza Vincent Nyerere ambaye ni Meneja kampeni za CHADEMA, na Mbunge wa Karatu Mchungaji Israel Natse kujipanga kwa kuandaa makundi ya vijana wa kufanya fujo kupinga matokeo endapo mgombea wa CCM, Sioi Sumari atashinda.

“Sasa ili mchujue hawa watu ni hatari tayari wameingiza vijana wa kufanya fujo siku ya kutangaza matokeo kama walivyofanya Igunga ambako walishindwa kihalali kabisa,” alisema Nchemba wakati akisoma barua hiyo na kuongeza: 
Habari na Mwandishi wetu Arumeru.

              *Mbowe, amnadi Nassari
Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe,akimnadi mgombea ubunge kupitia chama hicho Joshua Nassari.       


 WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki leo zikiingia wiki ya lala salama, huku vyama viwili, Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Chama Cha Mapinduzi vikiendelea kuumana vikali, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amewaambia watu wa jimbo hilo kuwa nchi nzima sasa inawaangalia wao hasa maamuzi watakayoyafanya ndani ya siku sita zijazo.

Akimnadi mgombea wa CHADEMA Joshua Nassar kwenye mikutano ya kampeni katika vijiji mbalimbali vya kata za Makiba, King’ori, Maroroni, Nkoarisambu na Songoro jana, Mbowe aliwaambia wananchi kuwa ‘wanazo siku saba tu za kufanya maamuzi ya msingi juu ya mstakabali wa maendeleo ya Arumeru na Tanzania kwa ujumla’ na dunia nzima inawasubiri kwa hilo.

Aliwaambia wananchi kuwa anamhitaji Nassar kwenda kuongeza idadi ya makamanda wapiganaji bungeni kwa ajili ya kuwatetea wanyonge dhidi ya watawala, hususan wakati huu ambapo nchi inajiandaa kuandika katiba mpya, ambapo aliongeza kuwa mgombea huyo ataungana na wenzake 48 kudai haki ya ardhi ziwemo ndani ya katiba mpya.

“Ndugu zangu, iko tofauti moja kubwa kati ya CHADEMA na CCM, sisi tunapigania kupata ridhaa kwa ajili kuwatetea Watanzania, kulinda rasilimali za nchi zinanufaishe wananchi wote, kupambana na ufisadi unaozidi kulimaliza taifa, lakini wenzetu tayari walishapata ridhaa hiyo, lakini wameshindwa kabisa kuitumia kwa ajili ya kusimamia rasilimali zetu kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Habari na Mwandishi wetu, Arumeru
      
IGP Said Mwema.
Wakuu wa Jeshi la Polisi katika nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameunga mkono juhudi za kuanza Kituo cha Uchunguzi cha Rufaa cha Kanda kwa Masuala ya Uhalifu (RRFC).
‘’ Tunapaswa kufanyakazi kwa kushirikiana kwa manufaa ya wote hapo baadaye,’’ Fabien Ndayishimiye, Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Burundi aliwaambia wataalamu wa EAC mjini Bujumbura waliokuwa wanakagua miundo mbinu ya uchunguzi ya jeshi hilo kuona kama inafaa kukiweka kituo hicho cha RRFC nchini humo.
Katika taarifa iliyotolewa na Sekretariati ya EAC, Mkuu wa huyo wa Jeshi la Polisi alisema kwamba kanda ya Afrika Mashariki ni familia moja na kwamba uhalifu wowote unaofanywa katika nchi moja unagusa nchi nyingine.
Kamati ya wataalamu nane wa masuala ya uchunguzi wa uhalifu katika jeshi la Polisi katika kanda  ya Afrika Mashariki ilianza kukagua miundombinu hiyo ya kanda kuanza Machi 8, 2012.
Nchini Rwanda, Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo (IGP), Emmanuel Gasana aliunga mkono juhusi za EAC za kutaka kuanzisha kituo hicho na kwamba nchi yake inaunga mkono juhudi hizo.
‘’Tunasubiri kwa hamu kuanzishwa kwa kituo bora zaidi ili kudhibiti uhalifu unaojitokeza,’’ alisema katika taarifa yake.
Wakati huohuo IGP wa Tanzania, Saidi Mwema alisema kwamba Tanzania imeshapitisha na kufanya mabadiliko katika jeshi la Polisi, ikiwa ni pamoja na kuweka mitambo ya kisasa ya miundombinu yake ya uchunguzi katika jeshi hilo.
‘’Tunataka kuona watu katika Afrika Mashariki yenye mtangamano wanapata manufaa na kujivunia huduma  zenye weledi za majeshi yao ya polisi,’’ Mwema alisisitiza na kuongeza kwamba ‘’mambo hayo yote yanaungwa mkono kwa dhati na serikali ya Tanzania.’’
 Mwandishi wetu,Arusha.

Panga la Serikali kuvishukia vyuo, shule


 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Stadi nchini, Philiph Mulugo.


Serikali imesema, itazifunga shule na vyuo vyote ambavyo havijasajiliwa na vile ambavyo havijakidhi vigezo na viwango vya kutoa elimu hapa nchini, ili kulinda hadhi ya elimu ya Tanzania iliyovamiwa na soko holela.

Hayo yamebainishwa na wakati wa akihitimisha kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Mamlaka Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

Huku akizungumza kwa ukali, Mhe. Mulugo amesema “sekta ya elimu haiwezi kuachwa hivi hivi kama haina mwenyewe, haiwezekani tukawa tunaendesha elimu kwa mfumo holela, hadi kufikia mwanafunzi kuingia sekondari huku hajui kusoma na kuandika”.

Naibu Waziri amesema siku hizi kuna matangazo mengi ya shule na vyuo kwenye vyombo vya habari ambavyo havijasajiliwa, hivyo ameiagiza VETA, kufanya ukaguzi na kuvibaini vyuo hole na kuvifunga ili kulinda hadhi ya elimu yetu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya VETA, Prof. Idrissa Mshoro,  aliwatanga Watanzania kubadili mtizamo wao kuhusu vyuo vya VETA, wakidhani ni kwa ajili ya wale waliofeli darasa la saba au kidato cha nne, VETA  ya sasa inatoa mafunzo kwa wote, na kuna fani mpya ambazo zinahitaji wahitimu walipasi vizuri kuweza kuzimudu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadia Moshi, amewataka wadau wa elimu kujitokeza zaidi katika kuwekeza kwenye kujenga vyuo vya ufundi na kueleza ndilo suluhisho pekee la tatizo la ajira kwa vijana, kwa sababu vijana wakipatiwa elimu ya ufundi, na kuwezeshwa kwa vifaa,  wataweza kujiajiri wenyewe mara tuu wamalizapo chuo.


Maadhimisho hayo ya  wiki moja, yamehusisha maonyesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na vyuo vya VETA nchini na kuhusisha wajasiliamali wadogo wadogo waliowezeshwa na VETA, na yamehitimishwa kwa maandamano maalum ya wadau wa VETA katika viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga.

Habari na Mwandishi wetu, Tanga

Kampuni ya gesi ya Kilwa Enegy matatani

Waziri wa Nishati na Madini Willium Ngeleja.



WANANCHI wa kaya zaidi ya 3000 wa Kata  ya Kivule Wilaya Ilala wameijia juu Kampuni ya Kilwa Enegy inayotaka kuwahamisha kupisha mradi wa umeme wa gesi kwa kuchelewesha kulipa  fidia kwa zaidi ya miezi sita.

Wananchi hao wanataka tathmini  ifanyike upya  kwenye nyumba zao na walipwe fidia kwa kiwango cha kimataifa  kutoakana na kuyumba kwa uchumi  kila kukicha duniani .

Wakati kampuni hiyo ikifanya  tathmini Agosti mwaka jana  kwenye eneo la mita 60,  iliwaahidi wananchi hao itakuwa imekwisha walipa fedha zao ndani ya siku 21 kitu ambacho hakikufanyika.

Akizungumza, Mohamed Abdalraman miongoni mwa wanaobolewa nyumba zao, alisema  kutokana na ahadi hiyo, imewafanya washindwe kuendeleza maeneo yao na kusababisha baadhi ya maeneo kuwa vichaka vya majambazi.

“Hadi sasa ni zaid ya miezi sita hatujui tutalipwa lini na kiasi gani,  tunataka tathmini ifanywe upya na tulipwe kwa kiwango cha kimataifa kulingana na gharama za ujenzi zilivyopanda kwa zaidi ya asilimia 25.

“Tunaiomba Serikali  iingilie kati tatizo hili tulipwe haraka kwa sababu tumechoka kusumbuliwa na tunataka malipo yalingane na gharama za nyumba zetu ili kuepuka usumbufu, wakitulipa kidogo tutakuwa na hasira nao kila siku,”alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ufuatiliaji  wa  mchakato huo, Denis Ikandilo alisema  Machi 23, mwaka huu waliwapa siku saba kampuni ya Kilwa Enegy ili iwe imetoa majibu itawalipa lipa lini. 

  Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 



HABARI YA MKAZI WA MOSHI KUKUTWA NA MBWA ALIYEMCHUNA YAZUA GUNZO MITAANI.

PICHA YA MBWA AMBAYE ALIKUWA AMESHACHUNWA NA BWANA TOMAS TAYARI KWA KUNYWA SUPU.

Habari ya Mkazi wa Chekereni ya Kahe Wilaya ya Moshi Vijijini Thomas Mlay (28) kukutwa na mbwa aliyekuwa amemchuna imekuwa habari ambayo ilivuta hisia za watu wengi na kuwa gunzo sehemu mbambali nchini.

Tukio hilo ambalo lilitokea Machi 21 mwaka huu majira ya saa tisa mchana huko maeneo ya Chekereni ya Mabogini.Kamanda wa Polisi Absalom Mwakyoma alisema mgambo wa Kahe Chekereni alimkamata mtuhumiwa huyo akiwa amemchuna mbwa akidai kuwa anataka kula nyama yake.

Alisema kuwa mgambo huyo alipata taarifa kutoka kwa uongozi wa kijiji hicho kuwa Thomas Mlay katika hali isiyo ya kawaida akiwa nyumbani kwake aliweza kumkamata mbwa wa nyumbani kwao na kumchinja kisha kumchuna ngozi kwa nia ya kumchemsha na kunywa supu yake.

Kamanda alisema kuwa kutokana na hali hiyo wanakijiji kupitia uongozi wa kijiji cha Chekereni walimkamata na kumhoji kutokana na tukio hilo na kutoa sababu zilizompelekea kumchuna mbwa huyo kuwa ni kutaka kunywa supu yake.

Aliongeza kuwa kutokana na sababu hiyo uongozi wa kijiji walipata utata kama kweli alitaka kunywa supu kama alivyodai au alitaka kuwauzia watu kwani baada ya mbwa huyo kuchunwa alikuwa akionekana kama mbuzi mdogo.

Mwakyoma alisema uongozi wa kijiji hicho ulipata mashaka na mtu huyo na kuamua kumfikisha katika kituo cha polisi Moshi kwa mahojiano ambapo ilibainika kuwa ana matatizo ya akili. Hata hivyo, bado anaendelea kuhojiwa ili kujua kwa undani dhamira yake iliyosababisha kufanya kitendo hicho.



ZOEZI LA MANISPAA YA MOSHI KUWA KATIKA HADHI YA JIJI,KUKAMILIKA MWISHONI MWA MWAKA HUU..Mmiji wa Moshi Unavyoonekana hivi sasa,Jengo la Kibo Tower




Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Bernadette Kinabo akizungumzia zoezi la Mji wa Moshi Kuwa katika hadhi ya jiji.

Zoezi la upanuzi wa Manispaa ya Moshi kuwa katika hadhi ya jiji linatarajiwa kumalizika mapema mwishoni mwa mwakaa huu baada ya hatua za awali kumalizika.

 Hatua hizo za awali ambazo zimekamilika hadi sasa ni pamoja na upanuzi wa kilomita za mraba 142 tofauti na kilomita za awali ambazo zilikuwa kilomita za mraba 58.

Akizungumza na dira ya leo ofisini kwake Mkurugenzi wa Manisoaa ya Moshi Bernadette Kinabo amesema kilomita za ziada zimepatikana kutoka halmashauri ya Moshi Vijijini jambo ambalo hapo awali liliwekewa urasimu na viongozi waliomaliza muda wake akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.

Kinabo amesema kuwa zoezi hilo  huenda likakamilika mwishoini mwa mwaka huu,baada ya kupitishwa kwenye halmashauri ambazo mji utapanukia,pamoja na usshirikiano Mkubwa aliouonyesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama.


Amesema kuwa hali imekuwa nzuri katika mchakato huo baada ya uongozi wa halmashauri ya moshi vijijini kubadilika,kutokana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kuzuia wananchi kukubaliana na suala hilo ambalo lilikuwa na maslahi kwa wananchi na ardhi yao ingepanda dhamani badala ya kutegemea kilomo pekee.







Uongozi wa Elimu Jimbo Katoliki la Moshi,waeleza kusikitishwa na mmonyoko wa maadili kwa wanafunzi.

MKURUGENZI WA ELIMU JIMBO KATOLIKI LA MOSHI(KULIA)FATHER WILLIUM RUAICHI.

MWEZESHAJI KWENYE SEMINA HIYO,WANAOONEKANA NI WAALIMU WAKUU,WAKUU WASAIDIZI,NA WAALIMU WA NIDHAMU KUTOKA SHULE 31 ZA SEKONDARY ZINAZOMILIKIWA NA KANISA KATOLIKI..


 Uongozi wa Elimu Jimbo Katoliki la Moshi,umeeleza kusikitishwa na mmonyoko wa maadili kwa vijana hususani wanafunzi,huku wakisema kuwa hawapo tayari kulifumbia macho suala hilo bali wataanza kwa kuwawajibisha baadhi ya waalimu ambao wamekuwa wakikikua maadili,ikiwemo uvaaji wanapokuwa makazini ikifuatiwa na wanafunzi.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa elimu Jimbo katoliki la Moshi,Fatha Willium Ruaichi wakati wa semina iliyofanyika kwenye jimbo hilo kwa lengo la kuwawezesha wakuu wa shule za sekondari,wasaidizi wao,pamoja na waalimu wa nidhamu kwa shule zinazomilikiwa na kanisa katoliki.

Hata hivyo kutokana na mmonyoko wa maadili kuongezeka kwa kasi,ambapo pia waalimu nao walilalamikiwa kwenye semina hiyo kwa kuvaa nguo ambazo haziendani na maadili,Mkurugenzi huyo alisema Waalimu ambao watakuwa wanakinzana na taratibu za mavazi zilizowekwa na uongozi wa kanisa basi basi watasitishiwa mikataba yao.

Ruaichi alisema katika kusimamia madili ya wanafunzi waalimu wana nafasi kubwa kuhakikisha wao wanakuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi hao,ndipo kuweza kuwawajibisha wanafunzi ambao wamekuwa wakivaa sare za shule ambazo haziendani na maadili yaliyowekwa na kanisa hilo.

Alisema kuwa uvaaji wa waalimu unatakiwa kufuata maadili ya shule,kutokana na maadili ya shule kutotofautiana na yale ya Wizara ya elimu,ili kuweza kupiga vita uvaaji mbovu kwa wanafunzi ambao zinawaacha sehemu ya miili yao wazi ambao wamekuwa wakiadhiriwa na utandawazi.

“Shule za dini tunatakiwa kuwa mfano wa kuiga katika mambo ya maadili,na suala hili tumekuwa tukilitilia mkazo sana,lakini wakati mwingine wakuu wa shule wamekuwa wakituangusha katika usimamizi”Alisema Ruaichi.

Mwisho

Thursday, March 22, 2012

KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA(LAAC) YAIOMBA KURUGENZI YA MASKATA NA TAKUKURU KUONGEZA KASI KATIKA UTENDAJI
 
mwenyekiti wa kamati hiyo Bw Augustine Mrema

KAMATI ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa(LAAC) imeiomba ofisi ya
mkurugenzi wa mashtaka nchini(DPP) kuharakisha mchakato wa kuandaa
majalada ya kesi dhidi ya watumishi wa halmashauri za wilaya,jiji na
manispaa nchini ili kuwatendea waliosimamishwa kazi.

Pamoja na DPP lakini pia kamati hiyo imeiomba taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa nchini(TAKUKURU) kuongeza kasi katika uchunguzi
wake dhidi ya watumishi hao ili wale wabadhirifu wachukuliwe hatua
ikiwa ni fundisho kwa wengine.

Akizungumza na viongozi wa halmashauri za Jiji la Arusha, Arusha na
Monduli mkoani humo,mwenyekiti wa kamati hiyo Bw Augustine Mrema
alisema taasisi hizo pamoja na kufanya kazi nzuri kwa maendleo ya
taifa lakini zinatakiwa kuongeza kasi ya utendaji.

“Kwa namna moja au nyingine hiki kitendo cha taasisi hizi kuchelewa
kutoa maamuzi juu ya majalada ya watumishi waliosimamishwa na wengine
kufukuzwa kazi ni kuchangia ucheleweshaji wa kesi dhidi ya watumishi
wabadhirifu”alisema.

Mwenykiti huyo alisema pia kitendo cha baadhi ya halmashauri kuongozwa
na makaimu wakuu wa idara kwa zaidi ya miaka miwili ni kuwanyima
nafasi ya kufanya maamuzi kwa wakati wakihofia nafasi zao na kwamba
ipo haja kwa suala hilo kurekebishwa.

Mrema alisema ili kuisadia serikali kusimamia halmashauri kuwa na
nidhamu ya matumizi ya fedha za umma,wahisani na wananchi kwa ujumla
ipo haja kwa taasisi hizo kutekeleza wajibu wake kwa wakati ili
kuwatendea haki wanaotuhumiwa.

Mwenyekiti huyo alitolea mfano halmashauri za wilaya ya Monduli ambayo
kuna nafasi 12 za wakuu wa idara muhimu ambazo zinaendeshwa na makaimu
huku pia halmashauri ya jiji nayo ikiwa na nafasi 6 zinazokaimiwa.

Kamati hiyo iliiomba serikali kuhakikisha taasisi zake hizo zinakuwa
mstari wa mbele katika kusukuma halmashauri kutekeleza wajibu wake
jambo ambalo litachochea maendeleo ya haraka katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wao wajumbe wa kamati mbunge wa bahi,Bw Omary Badwel na
mbunge wa mtwara mjini ,Bw Hasnain Murji waliomba TAMISEMI kujaza
nafasi zinazokaimiwa katika halmashauri ya Monduli na jiji la Arusha.

Nao mbunge wa viti maalum mkoani Morogoro,bi Suzan Kiwanga na mbunge
wa mbozi mashariki bw godfrey Zambi walisema kuna uzembe wa wakuu wa
idara katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.
 
Habari na Dixon Busagaga,Arusha,