CUF YAWATAKA WAFUASI WAKE NA WANANCHI ZANZIBAR KUWA WATULIVU, WAVUMILIVU NA KUTOA MAWAZO YAO BILA JAZBA
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na katibu Mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Chama
cha Wananchi(CUF) kimewataka wananchi kutulia na Serikali kufanya
uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa
wiki Mjini Zanzibar.
Taraifa
ya Chama hicho kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa
Uenezi na Mahusiano na Umma,Salim Bimani ilisema “Chama cha CUF kinatoa
wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu na kuitumia fursa ya
kutoa mawazo yao bila jazba na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha
mawazo yao”
Taarifa
hiyo ilisema kwamba vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa moto na
kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni
wa Kizanzibari.
“Uchunguzi
wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria bila
uonevu wala upendeleo” Alisema Bimani katika taarifa yake hiyo ambayo
pia alisema kwamba ni lazima kwa wakati huu na kwa haraka iwezekanavyo,
Serikali izungumze na Mashekhe bila ya kuona muhali na kwa uwazi kabisa
ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa faida ya nchi.
Chama
hicho kimesema kwamba pamoja na sababu au visingizio mbalimbali
vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwemo za hamasa za wananchi,
chuki binafsi, ukosefu wa hekima,matumizi ya nguvu za dola na hata
uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutokupendelea maridhiano ya
kisiasa Zanzibar.
“Chama
cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania,hakiwezi
kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika
nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar
wakibainika kufurahia mazingira hayo,kwa maslahi binafsi na pia kutoa
kauli za kutatanisha za kisiasa” Alisema Bimani katika taarifa yake.
TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINEZO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA
Mgeni
rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi
Juma Maalim na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo na UwaGeneral Officer Commanding (GOC) Meja Jenerali Hassan Vuai Chema akitoa heshima zake. wakishiriki kuimba wimbo wa taifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya walinda amani Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe
za Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa
inayoadhimishwa kila Mwaka tarehe 29 Mei. Picha zote na MO BLOG
Mgeni
rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi
Juma Maalim akiweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu
ya mashujaa.
Naibu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi.
Hopolang Phororo akiweka Shada la Maua kama ishara ya kuwakumbuka
walinda Amani wa Afrika.
Mkuu
wa Makumbusho ya Mnazi mmoja Zanzibar Ameir Ibarahim Mshenga akionesha
picha ya Watafiti wa mambo ya bahari waliyofanya Zanzibar katika kikao
cha k kujadili suala la uharibifu wa mambo ya bahari kilichofanyika leo ukumbi wa Makumbusho ya Kasri uliopo Forodhani
(Picha na Iddy Haji-Maelezo Zanzíbar)
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Kamishna wa Utamaduni na Michezo Zanzibar Hamadi Bakari Mshindo amesema ipo haja ya Kitengo cha Urithi wa Baharini kuwa makini na jasiri katika kusimamia vyema urithi wa Zanzibar kwani kitengo hicho kinaweza kuwa sehemu muhimu ya kuvutia watalii ambao wanaweza kuzuru maeneo ya urithi huo.
Amesema
maeneo ya Urithi wa Bahari ni sehemu muhimu kwani Wageni kutoka nchi
mbalimbali wamekuwa wakiyatembelea ili kujua historia ya maeneo hayo
jambo ambalo linaweza kuwa kichochoe kikubwa cha kuongeza wageni ambao
huja kuitembelea Zanzibar kila msimu.
Kamishna Mshindo ameyasema hayo katika kikao cha kujadili suala la uharibifu wa mambo ya bahari kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Kasri uliopo Forodhani mjini Zanzíbar.
Amesema lengo la kikao hicho ni kujadili njia nzuri za kuhifadhi urithi wa baharini ambao kama utawekewa mikakati mizuri unaweza kuisaidia Zanzíbar kupiga hatua kwani ni eneo muhimu la kuvutia watalii.
Kamishana amesema kutokana na umuhimu wake kuna haja pia ya wadau walioshiriki
katika kikao hicho kuwa na mkakati wa pamoja wa kuhakikisha mazingira
ya urithi huo yanahifadhiwa kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Amefahamisha kuwa Urithi huo ni pamoja na Meli ambazo zilizama katika bahari, mapango na vitu ambavyo vimekuwa vikitupwa katika bahari mambo ambayo yanageuka kuwa urithi ambapo watu kutoka maeneo mbalimbali huwa na hamu ya kujua historia ya vitu hivyo.
Aidha
urithi huo huchangia kuongezeka kwa mazalio ya viumbe hai wa bahari
ambao hugeuza maeneo hayo kuwa nyumba zao za kujihifadhia na hivyo kusababisha ongezeko la samaki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale Dkt.Amina Ameir amesema kuna haja ya jamii kuelimishwa juu ya umuhimu huo sambamba na kuacha tabia ya kuchukua mabaki ya urithi huo kwa lengo la kwenda kuuza mabaki hayo kwa watu wasio husika.
Amesema
kuna Wazamiaji ambao hutumiwa na watu kwa lengo la kuzamua mabaki ya
Meli na Mamboti ambayo yalizama na kwenda kuyafanya bishara ya chuma
chakavu jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kisheria.
Ameongeza kuwa Idara yake itachukua
mkakati wa makusudi kwa kushirikiana na wadau husika kuwafahamisha
wananchi kuwa Mabaki ya meli zilizozama ni urithi wa Nchi na hivyo
wananchi hawana haki ya kuchukua mabaki hayo bila kupata idhini ya
Kitengo cha Urithi wa Mambo ya Bahari.
Akitoa historia yake Mkuu wa kitengo hicho Fakih Othman amesema kitengo hicho kilianzishwa mwaka 2011 kikiwa na malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti juu ya urithi wa baharini katika maeneo yote ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Malengo
mengine ni pamoja na kushirikiana na taasisi mbalimbali za nje na ndani
ya nchi zinazojishughulisha na uhifadhi na utunzaji wa urithi wa
Baharini.
Fakih ametaja changamoto zinazokikabili kitengo cha Urithi wa Mambo ya Baharini kuwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi, ukosefu wa mafunzo pamoja na kutokuwepo kwa fungu maalum kwa ajili ya kuendeleza kitengo hicho.
ZIARA YA WAZIRI WA NCHI AFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR KATIKA KANISA LILILOCHOMWA MOTO
-Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson
D,Kaganga akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Mohd Aboud maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto
katika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30
wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
PICHA NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR.
PICHA NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud
akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God
Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa
Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni Mkuu wa Jeshi
la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson
D,Kaganga akielezea kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile
kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea
Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa
na tokeo hilo.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson
D,Kaganga akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa
ikitolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mohd Aboud baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea
Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na baadhi yao kuhusishwa
na tukio hilo.
-Mkuu wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman
Jongo akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na
Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu
mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo
limechomwa moto.
Mku wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na
baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of
God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa na
baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa
Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi
Zanzibar Mussa Ali Mussa.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa
hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na
Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka
kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
habari na fullshangwe
No comments:
Post a Comment