MWEZESHAJI KWENYE SEMINA HIYO,WANAOONEKANA NI WAALIMU WAKUU,WAKUU WASAIDIZI,NA WAALIMU WA NIDHAMU KUTOKA SHULE 31 ZA SEKONDARY ZINAZOMILIKIWA NA KANISA KATOLIKI..
Uongozi
wa Elimu Jimbo Katoliki la Moshi,umeeleza kusikitishwa na mmonyoko wa maadili
kwa vijana hususani wanafunzi,huku wakisema kuwa hawapo tayari kulifumbia macho
suala hilo bali wataanza kwa kuwawajibisha baadhi ya waalimu ambao wamekuwa
wakikikua maadili,ikiwemo uvaaji wanapokuwa makazini ikifuatiwa na wanafunzi.
Hayo
yalibainishwa na Mkurugenzi wa elimu Jimbo katoliki la Moshi,Fatha Willium
Ruaichi wakati wa semina iliyofanyika kwenye jimbo hilo kwa lengo la
kuwawezesha wakuu wa shule za sekondari,wasaidizi wao,pamoja na waalimu wa
nidhamu kwa shule zinazomilikiwa na kanisa katoliki.
Hata
hivyo kutokana na mmonyoko wa maadili kuongezeka kwa kasi,ambapo pia waalimu
nao walilalamikiwa kwenye semina hiyo kwa kuvaa nguo ambazo haziendani na
maadili,Mkurugenzi huyo alisema Waalimu ambao watakuwa wanakinzana na taratibu
za mavazi zilizowekwa na uongozi wa kanisa basi basi watasitishiwa mikataba yao.
Ruaichi
alisema katika kusimamia madili ya wanafunzi waalimu wana nafasi kubwa
kuhakikisha wao wanakuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi hao,ndipo kuweza kuwawajibisha
wanafunzi ambao wamekuwa wakivaa sare za shule ambazo haziendani na maadili
yaliyowekwa na kanisa hilo.
Alisema
kuwa uvaaji wa waalimu unatakiwa kufuata maadili ya shule,kutokana na maadili
ya shule kutotofautiana na yale ya Wizara ya elimu,ili kuweza kupiga vita uvaaji
mbovu kwa wanafunzi ambao zinawaacha sehemu ya miili yao wazi ambao wamekuwa
wakiadhiriwa na utandawazi.
“Shule
za dini tunatakiwa kuwa mfano wa kuiga katika mambo ya maadili,na suala hili
tumekuwa tukilitilia mkazo sana,lakini
wakati mwingine wakuu wa shule wamekuwa wakituangusha katika usimamizi”Alisema
Ruaichi.
Mwisho
|
No comments:
Post a Comment