HABARI YA MKAZI WA MOSHI KUKUTWA NA MBWA ALIYEMCHUNA YAZUA GUNZO MITAANI.
|
PICHA YA MBWA AMBAYE ALIKUWA AMESHACHUNWA NA BWANA TOMAS TAYARI KWA KUNYWA SUPU.
Habari ya Mkazi wa Chekereni ya Kahe Wilaya ya Moshi Vijijini
Thomas Mlay (28) kukutwa na mbwa aliyekuwa amemchuna imekuwa habari ambayo
ilivuta hisia za watu wengi na kuwa gunzo sehemu mbambali nchini.
Tukio hilo
ambalo lilitokea Machi 21 mwaka huu majira ya saa tisa mchana huko maeneo ya
Chekereni ya Mabogini.Kamanda wa Polisi Absalom Mwakyoma alisema mgambo wa Kahe
Chekereni alimkamata mtuhumiwa huyo akiwa amemchuna mbwa akidai kuwa anataka
kula nyama yake.
Alisema kuwa mgambo huyo alipata taarifa kutoka kwa uongozi wa kijiji hicho
kuwa Thomas Mlay katika hali isiyo ya kawaida akiwa nyumbani kwake aliweza
kumkamata mbwa wa nyumbani kwao na kumchinja kisha kumchuna ngozi kwa nia ya
kumchemsha na kunywa supu yake.
Kamanda alisema kuwa kutokana na hali hiyo wanakijiji kupitia uongozi wa kijiji
cha Chekereni walimkamata na kumhoji kutokana na tukio hilo na kutoa sababu zilizompelekea kumchuna
mbwa huyo kuwa ni kutaka kunywa supu yake.
Aliongeza kuwa kutokana na sababu hiyo uongozi wa kijiji walipata utata kama
kweli alitaka kunywa supu kama alivyodai au alitaka kuwauzia watu kwani baada
ya mbwa huyo kuchunwa alikuwa akionekana kama
mbuzi mdogo.
Mwakyoma alisema uongozi wa kijiji hicho ulipata mashaka na mtu huyo na kuamua
kumfikisha katika kituo cha polisi Moshi kwa mahojiano ambapo ilibainika kuwa
ana matatizo ya akili. Hata hivyo, bado anaendelea kuhojiwa ili kujua kwa
undani dhamira yake iliyosababisha kufanya kitendo hicho.
|
No comments:
Post a Comment