Makachero wapya hao..
Jeshi la Polisi Nchini limeanzisha utaratibu mpya wa
kuwafanyia askari wake tathimini kila baada ya miaka mitatu kwa ajili ya
kuboresha utendaji wa jeshi hilo.
Hayo yalizungumzwa jana na Mkuu wa jeshi
la polisi nchini IGP Saidi Mwema wakati wa kufunga
mafunzo kwa askari polisi kwenye chuo cha taaluma cha (CCP)kilichopo Mjini
Moshi.
Alisema kuwa tathmini hiyo itatoa nafasi kwa askari
polisi ambao watakuwa wanafanya vizuri kuendelea na utandaji ndani ya Jeshi hilo,lakini kwa wale ambao watakuwa hawafanyi vizuri Jeshi
hilo
litasitisha mkataba wa kuendelea kuwa mtumishi.
Mwema alisema Jeshi hilo
limeamua kufanya hivyo ili kuweza kuwatumikia wananchi waliowaajiri kwa
uadilifu,pamoja an kuondoa malalamiko ambayo yamekuwepo kwa baadhi ya askari.
Hata hivyo alisema tathmini hiyo,haitawahurumia askari
ambao hawatakuwa na sifa,na watanyimwa mikataba ya kuendelea na utumishi,hivyo
kutakuwa kwenda kufanya kazi nyingine uraiani.
“Kwa viongozi wa juu wakiwemo Makamanda katika Komandi
yoyote,wanatakiwa kuwa waadilifu na kama
wataona askari yoyote utendaji wake hauridhishi atoe taairfa kwenye ngazi za
juu kwa miezi mitatu ili askari aweze kutoa sababu alisema Mwema.
Kwa upande
wake Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil alisema licha ya kuwepo kwa
mafanikio kwa jeshi hilo ila bado hayajasaidia kupunguza
matukio yanayoendelea kulichafua jeshi hilo.
Miongoni mwa matukio ambayo yaliyotajwa na Katibu huyo kwa
jeshi la polisi ni pamoja an kuendekea kuwepo kwa matukio kwa askari kujihusisha na rushwa na kuwabambikia wananchi
keshi na kuwatesa raia,vitendo vya utovu wa nidhamu mitaani,ambavyo vinaendelea
kuchafua jeshi hilo.
Alisema kuwa kwa Polisi ambao wamekuwa na tabia za utovu
wa nidhamu wanatakiwa kuondolewa ili kuendelea kulinda heshima ya jeshi hilo.
Katika mahafali hayo wanafunzi waliofanya mtihani 3264
waliofaulu mtihani walikuwa 3210 na waliofeli ni 54 walipata nafasi ya kufanya mitihani
mwingine,na wakifaulu wataingizwa kazini na ambao watashindwa wataenda kutafuta
ajira nyingine.
|
No comments:
Post a Comment