CCM yadai kukamata barua ya
CHADEMA
Kinamama wakimshangilia Mgombea Ubunge wa CCM Sioi Sumari katika kijiji cha Ngongongare,Kata ya Maji ya Chai.
MPANGO
wa siri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kuandaa makundi ya
vijana watakaofanya fujo kupinga matokeo endapo mgombea wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) Sioi Sumari atatangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo mdogo, umejulikana.
Mpango
huo ambao upo katika barua inayodaiwa kuandikwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk.
Willbroad Slaa, mbali na kuainisha makundi hayo pia imeelezea hofu ya Chama
hicho juu ya kushindwa kwenye uchaguzi huo mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru
Mashariki.
Barua
hiyo iliyosomwa jana kwenye mkutano wa kampeni za mgombea ubunge wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) Sioi Sumari na Mratibu wa Kampeni Mwigullu Nchemba ambapo
alidai kwamba, Dk. Slaa amekuwa akiwashutumu viongozi wenzake kwa kutumia lugha
za matusi kwenye uchaguzi huo mdogo.
Alidai
katika barua hiyo Dk. Slaa amewalalamikia kwa kutumia lugha chafu yakiwemo
maneno ya kumkashifu Rais mstaafu Benjamin Mkapa hatua ambayo ilionyesha
kutokukomaa katika siasa ikiwa ni pamoja na kukiweka chama hicho kwenye
mazingira ya kushindwa.
“Barua
hii ninayoisoma mbele yenu inawaagiza Vincent Nyerere ambaye ni Meneja kampeni
za CHADEMA, na Mbunge wa Karatu Mchungaji Israel Natse kujipanga kwa kuandaa
makundi ya vijana wa kufanya fujo kupinga matokeo endapo mgombea wa CCM, Sioi
Sumari atashinda.
“Sasa
ili mchujue hawa watu ni hatari tayari wameingiza vijana wa kufanya fujo siku
ya kutangaza matokeo kama walivyofanya Igunga
ambako walishindwa kihalali kabisa,” alisema Nchemba wakati akisoma barua hiyo
na kuongeza:
Habari na Mwandishi wetu Arumeru.
No comments:
Post a Comment