ZOEZI LA MANISPAA YA MOSHI KUWA KATIKA HADHI YA JIJI,KUKAMILIKA MWISHONI MWA MWAKA HUU..Mmiji wa Moshi Unavyoonekana hivi sasa,Jengo la Kibo Tower |
Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Bernadette Kinabo akizungumzia zoezi la Mji wa Moshi Kuwa katika hadhi ya jiji. |
Zoezi
la upanuzi wa Manispaa ya Moshi kuwa katika hadhi ya jiji linatarajiwa
kumalizika mapema mwishoni mwa mwakaa huu baada ya hatua za awali kumalizika.
Hatua hizo za awali ambazo zimekamilika hadi
sasa ni pamoja na upanuzi wa kilomita za mraba 142 tofauti na kilomita za awali
ambazo zilikuwa kilomita za mraba 58.
Akizungumza
na dira ya leo ofisini kwake Mkurugenzi wa Manisoaa ya Moshi Bernadette Kinabo
amesema kilomita za ziada zimepatikana kutoka halmashauri ya Moshi Vijijini
jambo ambalo hapo awali liliwekewa urasimu na viongozi waliomaliza muda wake
akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.
Kinabo
amesema kuwa zoezi hilo huenda likakamilika mwishoini mwa mwaka
huu,baada ya kupitishwa kwenye halmashauri ambazo mji utapanukia,pamoja na
usshirikiano Mkubwa aliouonyesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama.
Amesema
kuwa hali imekuwa nzuri katika mchakato huo baada ya uongozi wa halmashauri ya
moshi vijijini kubadilika,kutokana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
kuzuia wananchi kukubaliana na suala hilo ambalo lilikuwa na maslahi kwa
wananchi na ardhi yao ingepanda dhamani badala ya kutegemea kilomo pekee.
No comments:
Post a Comment