
Mwanaharakati
kutoka kituo cha msaada wa sheria wanawake na watoto mkoani Iringa
Bw Jackson Gaso ambaye amejitolea kupambana na raia wa India
anayemiliki taasisi ya mikopo ya Brac kwa kunyanyasa wanawake Iringa

Mwanamke mjane Edina Panzi (47) siku aliyofungiwa ndani ya m,ahabusu za Brac

Hapa akichuma mbonga katika bustani yake kwa ajili ya kuuza ili aweze kulipa deni analodaiwa Brac


Sakata
la mwanamke mjane Edina Panzi(47) kufungiwa katika moja kati ya ofisi
za taasisi ya mikopo ya Brac tawi la Iringa taasisi inayomilikiwa na
Raia wa India kwa madai ya kushindwa kulipa deni lake kiasi cha
shilingi 5800 limechukua sura tofauti baada ya mwanaharakati wa
kituo cha msaada wa kisheria wanawake na watoto Bw Jackson Gaso
kujitosa kuifikisha taasisi hiyo mbele ya vyombo vya sheria.
Gaso
amejitokeza kumsaidia mwanamke huyo kama njia ya kupinga vitendo vya
unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyofanywa na taasisi
hiyo ya Brac ambayo ipo chini ya raia wa India.
Hivyo amesema
kuwa kituo chake kinajipanga kumfikisha mahakamani mkurugenzi wa
taasisi hiyo kwa ukiukaji wa haki za binadamu kama njia ya kusaidia
jamii inayonyanyaswa na taasisi hiyo.
Habari na Francis Godwin Iringa.
No comments:
Post a Comment