*Mbowe, amnadi Nassari
Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe,akimnadi mgombea ubunge kupitia chama hicho Joshua Nassari.
WAKATI
kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki leo zikiingia wiki ya lala
salama, huku vyama viwili, Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Chama Cha
Mapinduzi vikiendelea kuumana vikali, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe
amewaambia watu wa jimbo hilo
kuwa nchi nzima sasa inawaangalia wao hasa maamuzi watakayoyafanya ndani ya
siku sita zijazo.
Akimnadi
mgombea wa CHADEMA Joshua Nassar kwenye mikutano ya kampeni katika vijiji
mbalimbali vya kata za Makiba, King’ori, Maroroni, Nkoarisambu na Songoro jana,
Mbowe aliwaambia wananchi kuwa ‘wanazo siku saba tu za kufanya maamuzi ya
msingi juu ya mstakabali wa maendeleo ya Arumeru na Tanzania kwa ujumla’ na
dunia nzima inawasubiri kwa hilo.
Aliwaambia
wananchi kuwa anamhitaji Nassar kwenda kuongeza idadi ya makamanda wapiganaji
bungeni kwa ajili ya kuwatetea wanyonge dhidi ya watawala, hususan wakati huu
ambapo nchi inajiandaa kuandika katiba mpya, ambapo aliongeza kuwa mgombea huyo
ataungana na wenzake 48 kudai haki ya ardhi ziwemo ndani ya katiba mpya.
“Ndugu
zangu, iko tofauti moja kubwa kati ya CHADEMA na CCM, sisi tunapigania kupata
ridhaa kwa ajili kuwatetea Watanzania, kulinda rasilimali za nchi zinanufaishe
wananchi wote, kupambana na ufisadi unaozidi kulimaliza taifa, lakini wenzetu
tayari walishapata ridhaa hiyo, lakini wameshindwa kabisa kuitumia kwa ajili ya
kusimamia rasilimali zetu kwa faida ya kizazi hiki na vizazi vijavyo.
Habari na Mwandishi wetu, Arumeru
No comments:
Post a Comment