MTANZANIA WA KWANZA KUPANDA MLIMA EVAREST WILFRED MOSHI KUINGIA NCHINI LEO MAY 30.
Mtanzania wa kwanza kupanda mlima evarest ambao ni mlima mrefu kuliko yote duniani Wilfred Moshi leo anatarajiwa kuingia Nchini baada ya Kutokea Nepal ulipo mlima huo.
Akizungumza na mtandao wa www.tanzania-leo.blogsport.com mmoja wa ndugu wa karibu alisema kuwa anatarajiwa kuingia nchini majira ya saa 12:00 mchana leo.
Hata hivyo haijajulikana kama atakuwepo kiongozi yeyote wa Serikali katika kumpokea Wilfred ambaye ameitangaza vema nchini yetu duniani,ila mtandao huu ulitanabaishiwa kuwa watakuwepo familia ya Wilfred,Ndugu jamaa na marafiki.
Kwa habari zaidi endelea kufuatilia hapa www.tanzania-leo.blogsport.com
Hongera sana Wilfred Moshi. nimeamin watanzania tunaweza....Mungu mbariki Wilfred kwa kutuwakilisha...Mungu ibariki Tanzania...Mungu ibariki Kilimanjaro...Mungu bariki Wachagaaaaa!!!!!
ReplyDelete