Tuesday, September 4, 2012

UMOJA WA WENYEVITI WA VITONGOJI HAI WAMTAKA RC KUFUTA KAULI KUWA ATAWAFUKUZISHA KAZI.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti wa Vitongoji Wilayani Hai,Saimon Mnyampanda akizungumza kwenye mkutano wao uliofanyika ukumbi wa fM Bomangombe.

Wenyeviti wa Vitongoji wakiwa kwenye umoja wao .

Wakizungumza kwenye kikao chao kilichokaa juzi kwenye ukumbi Fm bomangombe Wilayani Hai,walimtaka Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama kufuta kauli yake aliyoitoa agust 22 kwenye vyombo vya habari baada ya wenyeviti hao kugomea zoezi la kuwaongoza makarani wa sensa hadi hapo wangelipwa madai yao.

Walisema kuwa hata hivyo licha ya kukaa kikao na Mkuu wa Wilaya ya Hai Novatus makunga na kuamua kuondoa mgonmo huo,lakini hata hivyo posho zao za sensa sawa na shilingi million 5,800,000 walikuwa bado hawajalipwa pamoja na madai yao mengine ya posho ya shilingi million 280.

Walisema kuwa kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa ni ya Kisiasa kutokana na kutafsi sheria ya Tawala za Serikali za Mitaa ambayo inaeleza mtu mwenye mandeti ya kumuondoa madarakani Mwenyeviti wa Vitongoji ni Wananchi waliowaweka madarakani.


No comments:

Post a Comment