Mchungaji Msigwa awataka wananchi kumchagua Nassari akawe'Mbwa mbwekaji Bungeni'
Msigwa akizungumza kwenye mk Mwandishi Wetu, Arumeru
MBUNGE wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, amewatakawananchi wa Jimbo la Arumeru Mashariki, wamchague mgombea wa chama chao kwanini sawa na ‘Mbwa atakaye bweka Bungeni’, kwa kupigania maslahi ya jimbo lao.
Akituhubia katika mikutano ya kumnadi mgombe kupitiaCHADEMA Joshua Nassari, jana katika kata za Makiba, Kikwe na Ngarenanyuki, Mchungaji Msingwa, alisema ilikuweza kupata mwakilishi mwenye uchungu na jimbo hilo ni muhimu wananchiwakaweka itokadi za vyama vyao pembeni na kumchagua mgombea wao.
“Bungeni kuna keki ya Taifa, na ili kuipa ni lazimawananchi mumchague Nassari, ili aweze kuipigania kwa maslahi yenu kwa mudamrefu majimbo mengi yaliyokuwa yakiongozwa na wabunge kutoka Chama ChaMapinduzi (CCM), hayana maendeleo kwaniwengi wao hawana uchungu na maisha ya Watanzania. Leo mimi niko huku Rais Kikwete,amekwenda Iringa katika jimbo ninaloliongoza mimi kama Mbunge kutoka CHADEMA.
“Mradi wa maji alioufungua Iringa ni Sh. Bilioni 75, leoMbunge wa Mtera Livingston Lusinde, nakuja hapa kutukana hebu muulizeni katika jimbolake la Mtera ana maji kiasi gani. Eti CCM wanajenga hoja eti akichaguliwambunge wa upinzani hakuna maendeleo hili si kweli, mchagueni Nassari iliArumeru iweze kupata maendeleo kama ilivyo katika majimbo yetu tunayoyaongozaCHADEMA,” alisema Mchungaji Msigwa.
Aidha alisema kutokana na hali hiyo hivi sasa Atumeruinakabiliwa na ukosefu wa huduma za maji, barabara pamoja na huduma za afya.
Kwa upande wake Meneja Kampeni msaidizi Vicent Nyerere,aliwataka wananchi kutafakari kwa kina kuhusu hatima yao na mahitaji ya jimbohilo kuliko kusilikiza maneno ya CCM ambao muda mwingi wamekuwa wakitukanakatika majukwaa ya siasa badala ya kutangaza sera zao.
Alisema ili kuweza kuondoka na umasiki unaowakabili hivisasa wanahitaji kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua Nassari, ili awezekusimamia miradi ya maendeleo ya jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment