Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo Stadi nchini, Philiph Mulugo.
Serikali imesema, itazifunga
shule na vyuo vyote ambavyo havijasajiliwa na vile ambavyo havijakidhi vigezo
na viwango vya kutoa elimu hapa nchini, ili kulinda hadhi ya elimu ya Tanzania
iliyovamiwa na soko holela.
Hayo yamebainishwa na wakati wa
akihitimisha kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Mamlaka Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi (VETA) yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Tangamano jijini
Tanga.
Huku akizungumza kwa ukali,
Mhe. Mulugo amesema “sekta ya elimu haiwezi kuachwa hivi hivi kama haina
mwenyewe, haiwezekani tukawa tunaendesha elimu kwa mfumo holela, hadi kufikia
mwanafunzi kuingia sekondari huku hajui kusoma na kuandika”.
Naibu Waziri amesema siku hizi
kuna matangazo mengi ya shule na vyuo kwenye vyombo vya habari ambavyo
havijasajiliwa, hivyo ameiagiza VETA, kufanya ukaguzi na kuvibaini vyuo hole na
kuvifunga ili kulinda hadhi ya elimu yetu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri
ya VETA, Prof. Idrissa Mshoro, aliwatanga Watanzania kubadili mtizamo wao
kuhusu vyuo vya VETA, wakidhani ni kwa ajili ya wale waliofeli darasa la saba
au kidato cha nne, VETA ya sasa inatoa mafunzo kwa wote, na kuna fani mpya
ambazo zinahitaji wahitimu walipasi vizuri kuweza kuzimudu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi
Mkuu wa VETA, Mhandisi Zebadia Moshi, amewataka wadau wa elimu kujitokeza zaidi
katika kuwekeza kwenye kujenga vyuo vya ufundi na kueleza ndilo suluhisho pekee
la tatizo la ajira kwa vijana, kwa sababu vijana wakipatiwa elimu ya ufundi, na
kuwezeshwa kwa vifaa, wataweza kujiajiri wenyewe mara tuu wamalizapo
chuo.
Maadhimisho hayo ya wiki
moja, yamehusisha maonyesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na vyuo vya VETA
nchini na kuhusisha wajasiliamali wadogo wadogo waliowezeshwa na VETA, na
yamehitimishwa kwa maandamano maalum ya wadau wa VETA katika viwanja vya
Mkwakwani mjini Tanga.
Habari na Mwandishi wetu, Tanga
|
No comments:
Post a Comment