Kampuni ya gesi ya Kilwa Enegy matatani |
Waziri wa Nishati na Madini Willium Ngeleja. |
WANANCHI
wa kaya zaidi ya 3000 wa Kata ya Kivule Wilaya Ilala wameijia juu Kampuni
ya Kilwa Enegy inayotaka kuwahamisha kupisha mradi wa umeme wa gesi kwa
kuchelewesha kulipa fidia kwa zaidi ya miezi sita.
Wananchi hao wanataka tathmini ifanyike upya kwenye nyumba zao na walipwe fidia kwa kiwango cha kimataifa kutoakana na kuyumba kwa uchumi kila kukicha duniani .
Wakati kampuni hiyo ikifanya tathmini Agosti mwaka jana kwenye eneo la mita 60, iliwaahidi wananchi hao itakuwa imekwisha walipa fedha zao ndani ya siku 21 kitu ambacho hakikufanyika.
Akizungumza, Mohamed Abdalraman miongoni mwa wanaobolewa nyumba zao, alisema kutokana na ahadi hiyo, imewafanya washindwe kuendeleza maeneo yao na kusababisha baadhi ya maeneo kuwa vichaka vya majambazi.
“Hadi sasa ni zaid ya miezi sita hatujui tutalipwa lini na kiasi gani, tunataka tathmini ifanywe upya na tulipwe kwa kiwango cha kimataifa kulingana na gharama za ujenzi zilivyopanda kwa zaidi ya asilimia 25.
“Tunaiomba Serikali iingilie kati tatizo hili tulipwe haraka kwa sababu tumechoka kusumbuliwa na tunataka malipo yalingane na gharama za nyumba zetu ili kuepuka usumbufu, wakitulipa kidogo tutakuwa na hasira nao kila siku,”alisema.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ufuatiliaji wa mchakato huo,
Denis Ikandilo alisema Machi 23, mwaka huu waliwapa siku saba kampuni ya
Kilwa Enegy ili iwe imetoa majibu itawalipa lipa lini.
Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
No comments:
Post a Comment