Saturday, August 18, 2012

WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI WAPONGEZA UONGOZI WA CHUO HICHO KWA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI.




Friday, August 10, 2012

WANANCHI WALALAMIKIA ITIKADI ZA KISIASA KUGEUKA KISIKI CHA MAENDELEO.
Hapa Diwani wa Kata ya Kimochi,Anamenyisa Macha akishauri kuairishwa kwa mkutano wa wananchi baada mtendaji kushindwa kufika.

Mwananchi akitoa hoja ya kusikitishwa kushindwa kufika kwa mtendaji huyo wa Kijiji kwenye Mkutano.

Mkutano huo ilibidi ufunguliwe na kufungwa.
Wananchi wa kijiji cha mdawi Kata ya Kimochi,Wilaya ya moshi vijijini wamemlalamikia Mtendaji wa kijiji hicho Lenard Mende kwa kushindwa kuwepo ofisi siku za kazi,pamoja na kuwa mtoro kwenye mikutano ya Serikali,ambayo inakuwa na lengo la kujadili shughuli za maendeleo ya kijiji hicho.

Akizungumza baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo na kuahirishwa bila kujadili agenda yoyote wananchi walikuwa wamefika kwenye mkutano huo walisema kuwa hiyo ni mara ya pili kushindwa kufanyika kwa  mkutano baada ya mkutano uliofanyika jula 8 mwaka huu,mtendaji huyo kuondoka baada ya kuulizwa swali na mmoja wa wananchi.

Mkti wa kijiji cha mdawi Rumisha Kinyaa aliwaeleza wananchi waliokuwa wamefika kwenye mkutano huo ambao ulihairishwa agusti 4 mwaka huu, kuwa walikuwa wamempa taarifa ya uwepo wa Mkutano huo Mtendaji wa Kijiji,lakini hadi kufika muda wa mkutano hakufika.

Alisema kuwa hawataweza kuendelea na Mkutano huo,ilihali muwakilishi wa Mkurugenzi hayupo,hivyo agenda mbalimbalimbali ambazo zingejadiliwa kwa siku hiyo ingekuwa ni kazi bure kama wangefanya bila kuwepo kwa Mtendaji.

“Miongoni mwa mambo ambayo wananchi walikuwa wahoji kwenye mkutano huo ni pamoja na kutokufika kwa mtendaji huyo ofisini siku za kazi,jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wananchi wa kijiji,wakati yeye ameletwa kwa ajili ya kushirikiana na wananchi kuleta maendeleo”Alisema Kinyaa.

Kwa  wake Diwani wa Kata ya Kimochi,Anamenyisa Macha alisema kuwa changamoto nyingi zinazotokea kwenye kijiji hicho zinatokana na itikadi za kisiasa ambazo zinasababishwa na mvutano wa vyama vya siasa,pamoja na wananchi kupingana na kugawa kwa kijiji cha Mdawi.

Alisema kuwa kinachotakiwa ni wananchi na viongozi kuondoa itikadi zao na kuwatumikia wananchi,ili kuweza kuleta maendeleo,pamoja na kuchunguza malalamiko yalipo kwa wananchi kuwa hawakuhusishwa katika ugawaji wa kijiji hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi alipuulizwa kuhusiana 
na tatizo lililopo kwenye kijiji hicho cha Mdawi,alisema kuwa amebanwa na shughuli za mbio za Mwenge ambao ulikwua Mkoani Kilimanjaro,huku akiahidi kulifuatilia baada ya kumalizika kwa mbio za Mwenge.
MKUU WA MKOA WA KILIMANAJRO  AKUTANA AN WAKUU WA WILAYA ZA MKAO HUO KUJADILI SHUGHULI MBALIMBALIZ AMAENDELEO
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama,akizungumza jambo kwenye kikao hicho kilichofanyika wilayani rombo mkoani Kilimanjaro.

Wakuu wa Wilaya Mbalimbali Mkoani Kilimanajro.


Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri.


Mkuu wa Mkoa akisikiliza taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Rombo hayupo pichani.

Akiwasilisha taarifa yake kuhusiana na fursa za maendeleo zilipo katika Manispaa ya Moshi alisema kuwa
Kufungwa kwa viwanda vya moshi,ambavyo vilikuwa vikizalisha bidhaa mbalimbali,immelezwa kusabisha tatizo la ajira kwa wakazi wa manispaa ya Moshi ambayo wakazi wake zaidi ya asilimia 80 walikuwa wakitegemea ajira kutoka kwenye viwanda hivyo.

Matokeo ya kufungwa kwa viwanda hivyo imesabisha wananchi wengi kukosa ajira,hivyo kupelekea kushukwa kwa vipato vya wananchi wake pamoja na kuongezeka kwa wafanayabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga,ambao wanategemea kazi hiyo kuweza kjioatia kipato cha kila sikukwa ajili ya kujikimu. 

 Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Bernadetha kinabo kwenye Mkutano uliofanyika Wilayani Rombo chini ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro leonidus Gama ambao umehudhuriwa na Wakurugenzi na wakuu wa Wilaya sita Mkoani hapa, lengo likiwa ni kuajdili vipaumbele vya maendeleo kwa mkoa wa Kilimanajro.


Tuesday, August 7, 2012

                                    LOWASA TUPO TAYARI KWA LOLOTE
 
KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imesema Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.

Akizungumza mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Lowassa alisema kamati yake imeridhishwa na maandalizi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

“Tumepewa maelezo na jeshi letu na tumeridhika kuwa ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na limejipanga vizuri sana kwa uhakika, kiakili na kivifaa,” alisema Lowassa.

Kabla ya Lowassa kuzungumza na waandishi wa habari, alifanya kikao cha faragha kilichohusisha pia wajumbe wa kamati hiyo na makamanda wa JWTZ walipofika bungeni kutoa taarifa kwa kamati hiyo.

 
Hata hivyo, katika tamko hilo Lowassa alisema Tanzania inatarajia mgogoro huo utamalizika kwa njia za kidiplomasia kwa sababu Watanzania na Wamalawi ni ndugu wa muda mrefu.

“Ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na kama ilivyo ahadi yao (JWTZ), wako tayari kulinda mipaka ya nchi yetu hadi tone la mwisho. Tunasali sana tusifike hapo,” alisema Lowassa na kuongeza: “Tunategemea hatutafika huko, lakini kwa heshima ya nchi yetu kama ikibidi kufika huko (vitani) tutafika kulinda mipaka yetu”.

Mwenyekiti huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu, alisema kama Tanzania itafikishwa mahali itabidi damu ya Watanzania imwagike, nchi iko tayari kulinda mipaka yake kwa nguvu.


Alisema kama itabidi kuingia vitani, itatumia umoja na mshikamano wa Watanzania wa mwaka 1978 wakati wa Vita na Uganda kulinda mipaka ili kulinda heshima ya nchi.

Alisema mwaka 1978 wakati Rais wa Uganda, Idd Amin na majeshi yake walipochukua sehemu ya Tanzania na kujitangazia ni mali yake, ilichukua hatua kumfukuza Amin.

“Alijitangazia sehemu ile ni mali ya Uganda hutegemei nchi ikae kimya, hutegemei Watanzania wanyamaze wakati nchi yao imetekwa, tulichukua hatua tukamfukuza hadi nchini kwake.”

 
Lowassa alisema Kamati ya Bunge inajua madhara ya kiuchumi yaliyotokana na Vita ya Idd Amin na kwamba vita yoyote ikipiganwa lazima kunakuwa na madhara ya kiuchumi.

Hata hivyo, alisema anaamini mgogoro huo hautafika huko na kusisitiza kuwa, lakini ikibidi JWTZ ni moja kati ya majeshi bora duniani na ni jeshi lililojiandaa vizuri kwa lolote.

 
“Wako tayari sisi ni moja kati ya jeshi lililojiandaa vizuri na jeshi bora duniani na la kujivunia. Tuko imara kiakili na kivifaa tena vya kisasa,” alisema Lowassa.

Alisema kamati yake inaunga mkono msimamo ulitolewa bungeni juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuhusu mgogoro huo na kwamba ndiyo kauli rasmi ya Serikali.

 
Juzi, Waziri Membe alizionya kampuni za kigeni za Malawi zilizoingia katika ardhi ya Tanzania eneo la Ziwa Nyasa kutafiti mafuta na gesi kusitisha mara moja.

Akiwasilisha makadirio ya wizara yake, Membe alisema upo ushahidi kuwa ndege tano za utafiti za Malawi ziliruka anga la Tanzania na kutua katika Ziwa Nyasa upande wa Tanzania.Membe alisema pamoja JWTZ kutoruhusu ndege hizo za Malawi kuingia na kutua eneo hilo la Ziwa Nyasa, bado ziliingia na kutua kinyume kabisa cha sheria za kimataifa.

“Wenzetu wa Malawi wanadai Ziwa Nyasa lote lipo Malawi na msingi wa madai yao ni mkataba wa Heligoland wa mwaka 1890 na sisi tunasema mpaka uko katikati ya Ziwa.”

Membe alisema hata mgogoro wa mpaka kati ya Cameroon na Nigeria ulitatuliwa na Mahakama Kuu ya Dunia kuwa mpaka baina ya nchi hizo mbili upite katikati ya Ziwa Chad.

Juzi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Patrick Kabambe alikaririwa na Redio Sauti ya Ujerumani akisema wataendelea na utafutaji mafuta licha ya onyo hilo la Tanzania.

Waziri huyo alisema ziwa hilo linaitwa Malawi na siyo Ziwa Nyasa na kwamba utafutaji wa mafuta na gesi utaendelea na hakuna wa kuwasimamisha. Alihoji, iweje Tanzania ishtuke sasa

Wabunge waridhia hoja ya marekebisho mafao‏

 Dodoma:
WABUNGE wameridhia hoja ya kutaka yafanyike marekebisho ya Sheria namba 5 ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2012 baada ya Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo (CCM) kuiwasilisha bungeni jana.

Katika hoja hiyo iliyoungwa mkono na wabunge, Mbunge huyo ametaka Serikali katika Mkutano ujao wa Bunge, iwasilishe muswada wa sheria kwa hati ya dharura kwa ajili ya kuweka vifungu vya sheria vinavyoweka fao la kujitoa katika mifuko hiyo kwa wafanyakazi wanaoacha kazi kwa sababu wafanyakazi wana haki ya kuacha au kuendelea na kazi.

“Wakati tunasubiri kuleta muswada Serikali itoe waraka wa maelekezo kwa mifuko ya jamii kuendelea kuwalipa mafao watumishi walioachishwa kazi au walioacha kazi,” alisema Mbunge huyo.

Ametaka pia katika muswada huo, Serikali iondoe vifungu vinavyomtaka mtumishi kuwasilisha maombi ya  kupata msamaha kwa fao la kujitoa.

Aidha, ametaka Serikali iagize kampuni za madini kutosimamisha wafanyakazi waliohoji kwa kina juu ya mafao yao baada ya kupata mshituko wa taarifa ya kutoruhusiwa kuchukua mafao.

Aliitaka Serikali iangalie kanuni inayotumika kukokotoa mafao ya wafanyakazi na kutaka watumishi wote wanaolipa kodi kupitia mishahara yao wapewe TIN namba wajulikane ni walipa kodi halali.
Mbunge huyo alisema Serikali isipowasilisha muswada huo wa marekebisho ya sheria, atawasilisha muswada binafsi ili wabunge wote walete marekebisho hayo kama alivyoyapendekeza.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo, wanachama walifaidika na kujitoa na kulipwa mafao kwa kuwa uliwawezesha kupata kianzio cha maisha yao baada ya kuacha kazi ikizingatiwa kwamba wafanyakazi nchini wanaishi maisha ya kuungaunga.

Alisema kutokuwapo kifungu hicho cha sheria kutaleta athari kwa watumishi wanaoachishwa kazi kabla ya umri wa kustaafu kwa kushindwa kuendesha maisha.
Alisema jambo hilo limekuwa tete na kuathiri uzalishaji katika sekta hususan katika madini ambako katika baadhi ya migodi, baadhi ya wafanyakazi walitishia kuandamana.

Spika Anne Makinda alisema leo Waziri wa Kazi na Ajira huenda akazungumzia suala hilo katika hotuba yake, lakini akataka Kamati ya Uongozi kuangalia upya muswada huo kabla ya kuwasilishwa kama hati ya dharura.

Sunday, August 5, 2012

       HOTEL YA KNCU ILIYOPO MINI MOSHI YANUSURIKIA KUTEKETEA KWA MOTO
Hivi ndivyo lilivyoonekana jengo la hoteli ya KNCU inayomilikiwa na chama kikuu cha ushirika mkoani Kilimanjaro Kncu wakati ilipoanza kuwaka moto.

Wananchi mbalimbali wakiwa wamefika kwenye hoteli ya KNCU kushuhudia tukio hilo.


Licha ya wananchi kulalamikia zima moto,lakini kwa siku ya jana waliweza kuwahi na kufanikiwa kuuzima moto uliokuwa umeshaanza kusambaa jengo zima,huku ofisi ya Bumaco Insurance ikionekana kuadhiriwa zaidi na moto huo na kuteketeza baadhi ya vifaa kama computa na vifaa vingine vilivyokuwepo kwenye chumba hicho

Friday, August 3, 2012

RAISI ATOA NG'OMBE KWA WANANCHI WA MONDULI AMBAO MIFUGO YAP ILIKUFA KWA UKAME.


Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

SERIKALI itakuwa inagawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha karibu mifugo 800,000 iliyopotea kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Ahadi hiyo imetolewa leo, Alhamisi, Agosti 2, 2012 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipozindua Mradi wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo kwa waliopotelewa mifugo yote katika Wilaya ya Monduli kwenye sherehe iliyofanyika Makuyuni wilayani humo.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiwemo wakuu wa wilaya na wabunge wa mkoa huo, Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa kundi la kwanza la wananchi ikiwa ni mitamba minne na dume moja la kisasa kwa kaya 16 za mwanzo.Uzinduzi huo ni wa pili kufanywa na Rais Kikwete chini ya Mradi huo wa kwanza wa aina yake kubuniwa na Serikali katika historia na wenye thamani ya sh. Bilioni 12.9.

Februari 19, mwaka huu, Rais Kikwete alizindua Mradi kama huo katika Wilaya ya Loliondo kwenye sherehe zilizofanyika mjini Loliondo. Kesho Agosti 3, 2012 Rais Kikwete anatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika mji wa Loliondo
                         MAHAKAMA YAAGIZA WAALIMU KUREJEA MASHULENI.
Mwanafunzi wa darasa tano katika shule ya msingi Kihesa Herieth Kitunduru .

WALIMU nchini wazidi kubanwa baada ya mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Kazi imesitisha mgomo wa walimu na kuwataka kurudi kazini mara moja.

Mahakama hiyo pia imeuagiza uongozi wa Chama cha Walimu (CWT) kuandaa taarifa kwa umma, kutangaza kusitishwa kwa mgomo huo kama walivyowatangazia wanachama wake wakati ulipoanza.

Mahakama hiyo ilisitisha mgomo huo jana wakati ilipotoa uamuzi wa maombi yaliyowasilishwa mahakamani na Serikali. Jaji Sophia Wambura aliyekuwa akisikiliza maombi hayo, alisema mgomo huo ni batili kwa kuwa haukukidhi masharti ya Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini.

Katika uamuzi wake, mahakama hiyo pia imekitaka CWT kulipa hasara za kifedha au kuwafidia wanafunzi vipindi vya masomo walivyovikosa, hususan wale wa darasa la saba. Mahakama hiyo ilikwenda mbali zaidi na kuwaonya walimu na Serikali kwa kitendo cha kuzungumzia suala hilo wakati tayari lilikuwa mahakamani.

Jaji Wambura alisema kitendo hicho ni uvunjaji wa Ibara ya 4 na ya 107 A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyokwisha kurekebishwa mara kadhaa.

“Vinginevyo, hakukuwa na haja ya kuja hapa mahakamani kabisa. Kama kila mmoja ataachwa awe jaji, itakuwa ni kero na uvunjaji wa utawala wa sheria,” alisema Jaji Wambura.

Jaji huyo alizitaka pande zote kurudi kwenye meza ya mazungumzo na kushauri kuwa, ikiwezekana zialike watu wenye ujuzi wa masuala ya sheria za kazi na uhusiano kazini kuwasaidia ili kufikia makubaliano kwa amani.

“Chini ya Masharti ya Kifungu cha 81 (1) (2) cha Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini, natamka kuwa mgomo ambao umekuwa ukiendelea kwa siku tatu sasa ni kinyume cha sheria. Ninaamuru usitishwe na walimu wote warudi kazini mara moja,” aliagiza Jaji Wambura.

Jaji Wambura alirejea hoja zilizowasilishwa na pande zote, waombaji wakiwakilishwa na Mawakili wa Serikali Wakuu, Obadia Kameya na Pius Mboya na wajibu maombi (CWT) wakiwakilishwa na Wakili Gabriel Mnyele.

Alisema baada ya kupitia hoja zote na vielelezo vilivyoambatanishwa kwenye hati za viapo pamoja na majibu husika, amebaini kuwa na kuridhika kuwa mgomo huo haukufuata sheria.

Alisema CWT hawakufuata masharti ya kifungu cha 80 (1), cha Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini na kwamba kulikuwa na dosari kwani kura zilizopigwa zilipotosha wanachama , kwa sababu hazikuwa za kuunga mkono mgomo, bali madai ya walimu.

Jaji huyo alisema upigaji kura ulikuwa ni batili kwani walimu hawakufahamishwa matokeo ya mgomo huo na kwamba haukuzingatia taratibu.

Pia alisema taarifa ya mgomo iliyowasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi Julai 27, 2012 saa 9:00 alasiri wakati mchakato wa upigaji kura ukiwa unaendelea, pia ilikuwa ni batili.

Dosari nyingine ni kutoeleza kikomo cha mgomo na kutokubainisha kama watawalipa wanachama wake wakati wa mgomo.

Aliongeza kwamba, CWT kwa kushindwa kutimiza masharti ya kanuni ya 42 na 43 za sheria husika, kulisababisha kero zisizo za lazima.

Alisisitiza kuwa kitendo cha CWT kuwasilisha taarifa ya mgomo Ijumaa saa 9:00 wakidai mgomo unaanza Jumatatu, hali wakijua kuwa Jumamosi na Jumapili hazikuwa siku za kazi, ni kinyume cha kanuni na kilifanywa kwa nia mbaya.

Wakili wa CWT, Mnyele alisema anasubiri maelekezo ya wateja wake, lakini Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema watatoa tamko leo.

CAMERA YETU LEO IPO VIWANJA VYA NANE NANE      ARUSHA.


BAADA ya kamera yetu kupata taarifa ya Tanzania kuongeza nguvu kwenye KILIMO KWANZA na kukosa sehemu ya kuona mikakati hiyo kwa vitendo isipokuwa kwenye makablasha tu liliamua kwenda kujione lenyewe mikakati ya kuinua uchumi wa nchi hii hususani kupitia kilimo pamoja na kuboresha hali ya maisha ya wakulima kwenye  maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wakulima Tanzania (nane nane).
BAADHI YA WENYE MABANDA WAKIWA KATIKA HATUA ZA MWISHO MWISHO KATIKA KUREKEBISHA MABANDA YAO KATIKA VIWANJA VYA NANE NANE ARUSHA

MMOJA WA WADAU AKIANGALIA BIDHA ZA KILIMO KATIKA MOJA YA BANDA KATIKA VIWANJA VYA NANE NANE ARUSHA



Moja ya vivutia vikubwa hilikuwa mashamba ambayo yalikuwa yamelimwa lakini akukuwa na mtu yoyote wa kutoa maelekezo jambo ambalo lililishangaza Jicho Letu na kulifanya liwatafute wausika.
HAPA NI BAADHI YA MASHAMBA AMBAYO JICHO LETU ILIJIONEA KATIKA VIWANJA VYA NANE NANE ARUSHA 2012

SEHEMU YA MASHAMBA DARASA KWENYE VIWANJA VYA NANE NANE ARUSHA 2012


 
Sherehe za Nane Nane huandaliwa na kuratibiwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika pamoja Chama cha Wakulima Tanzania (TASO).