Wednesday, March 6, 2013

TAKUKURU MBEYA WAMNASA MWALIMU AKIPOKEA RUSHWA KUTOKA KWA MWANAFUNZI YA SHILINGI 200


MWALIMU Faustin wa shule ya sekondari ya Forest iliyopo Jijini Mbeya amejikuta akitiwa mbaroni baada ya muda mrefu kuwaomba na kupokea rushwa ya Sh.200 kutoka kwa wanafunzi wake wanaochelewa na kuvaa viatu ambavyo havina kamba.
Arobaii za mwalimu huyo zilitimia jana baada ya maafisa wa Takukuru mkoa wa Mbeya kuinyaka issue hiyo na kutege mtego uliofanikisha kumnasa mwalimu huyo kinara wa rushwa shuleni hapo.
Mwalimu huyo alikutwa na maafisa wa Takukuru akiwa tayari amekusanya kiasi cha Sh.64,000 huku msaidizi wa ulaji rushwa hiyo Mwalimu Mwasote akifanikiwa kuwazidi mbio maafisa wa Takukuru kisha kutokomea kusikojulikana.
Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na kikosi kazi cha mtandao wa kalulunga.com kilipofika shuleni hapo walisema kuwa wamefurahishwa na Takukuru kumkamata mwalimu huyo mwenye urefu usiozidi futi tno na nusu huku akiwa na kitambi.
Walisema kuwa mwalimu huyo lich ya kuwatoza Sh.200 wanafunzi wanaochelewa au kuwa na makosa mbalimbali shuleni hapo, pia alikuwa akiwavua viatu wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo wa kununua viatu vya kamba na kuwatoza kati ya Sh.500-2000 endapo wanafunzi wakishindwa kumpa rushwa hiyo alikuwa akivipeleka viatu vyao kwenye matanuru ya matofali ili kuwashia moto.
Sanjari na hayo mwalimu Faustine, anatuhumiwa na wanafunzi kuwatesa kwa kuwainamisha miguu juu kichwa chini bila kujali jinsia zao wala mavazi na ambao wanashindwa anawaambia watoe Sh.200 na kwamba ofisi ya walimu inaitwa Gwantanamo!
Shule hiyo ni ile ambayo Mkuu wa shule ambaye ni mwanamke aliwahi kuwaambia wazazi kuwa watoto wao wa kike wote ni wake za watu baada ya kuwapima na kutofanikia kumkuta hata mmoja na usichana wake.

No comments:

Post a Comment