Monday, November 26, 2012


bAADA YA kupata ajali iliyopelekea kifo chake.







 
Mwaka mmoja haujaisha, bado mioyo ya watanzania wapenda burudani ikiwa bado njia panda ikitafakali yaliyokwisha kutokea, kukutwa na matukio magumu ya kihistoria kuikumba sanaa ta Tanzania.

Nasikitika kusema Sharo Milione hatunae kwasasa, baada ya kupata ajali ya gari mkoani Tanga wakati akitokea Dar es salaam akiwa mwenyewe ndani ya gari. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na mwili wa marehemu uko mochwali mkoani Tanga.

Ushuda wa Majonzi: Mara ya mwisho Anna Peter wa East Africa Radio Alhamis iliyopita alifanya nae mahojiano na hivi ndivyo alivyoeleza jinsi alivyoghubikwa na majonzi.....
"Wiki hata haijapita alifanya Interview yake ya kwanza na ya mwisho East Africa Radio, kama ulisikiliza utakumbuka nilimtania marehemu Sharomilionea kuwa mimi na yeye tuna historia yetu ambayo watu wengi hawajui....
Tulifanya nae movie ya 'Kimela' mwaka 2006 na yeye alikuwa anashika boom mic ana akawa anapenda kuwa karibu na mimi coz alikua anajua mimi mtangazaji(kipindi hicho Times Fm).
 Alikuwa akinambia Dada Anna mimi napenda kuimba,napenda kutangaza na iko siku nitatoka.
Tangu mwaka 2006 kwa mara ya kwanza Alhamisi tarehe 22 ndo nilifanya nae interview ya kwanza na yeye tho alishanipigia simu kama mara 2 akitaka interview na akinikumbusha kuwa tuliwahi kuonana, but mimi nikawa sina kumbukumbu mpaka tulipokuja kuonana Ana kwa ana.
Tulivyoanana Akanikumbusha kuwa Dada Anna uliwahi kusema utanisaidia, na kweli umethibitisha maneno yakoo.....Nataka kujaribu kukumbuka tulivyozungumza kwenye ile interview but siwezii ....#RIP kweli kifo hakichagui mtu......Poleni ndugu jamaa na marafiki pia".
 
 

Friday, November 23, 2012

KWA WALE WAPENZI WASOMAJI WA HADITH HABARI MPYA KWAO.



MAADHIMISHO MIAKA MITATU YA TAASISI YA WAKUGUZI FOUNDATION KUTOKA AJTC YALIKUWA HIVI...
Hapa kundi la Wakaguzi wakiwa kazini.

Ilikuwa bomba ile mbaya.

Kila aina ya sanaa ilikwepo.

Leacturer Andrew Ngobole akimlisha madamNeema  keki kwenye hafla hiyo


Moda na Dj Samboto nao walikuwepo pia hawa ni wakufunzi wa chuo cha arusha Journalism.




Mgeni Rasmi kwenye hafla hiyo akiwa kwenye meza kuu.


Hapa wakaguzi wakizindua t,shirt zao mpya.

Waziri Prof. Jumanne Maghembe azindua mradi mkubwa wa maji Kata ya Endagile Babati Vijijini