Monday, March 19, 2012

NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE AKIBIDHI CHETI CHA  UTOAJI HUDUMA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA KWA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA MOSHI(MUWSA).
MEZA KUU,(kulia)MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA MUWSA ANTONY KASONTA,(kushoto kwake)MKUU WA WILAYA YA MOSHI MUSA SAMIZI,aliyevaa suti ya kaki NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE,ANAFUATIWA NA MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA HIYO.
NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE AKIONYESHA  CHETI CHA UTOAJI UTOAJI HUDUMA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA(ISO)KILICHOTOLEWA  KWA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA MJINI MOSHI MKOANI KILIMANJARO.
NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE AKISOMA HOTUBA YAKE.
NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE AKIKABIDHI VYETI KWA WADAU WA MATUMIA MAJI.
 PICHA YA PAMOJA NA NAIBU WAZIRI,NA VIONGOZI MBALIMBALI.
 
NAIBU WAZIRI WA MAJI GERSON LWENGE AMEKABIDHI CHETI CHA UTOAJI UTOAJI HUDUMA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA(ISO) KWA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA MJINI MOSHI MKOANI KILIMANJARO.

Akuzungumza kwenye hafla ya kukabodhi Cheti hicho alizungumzia mafaniko mbalimbali yaliyopatikana kwenye mamlaka hiyo ikiwemo utendaji,Utaoji wa huduma,ukaguzi wa mahesabu pamoja na ukusanyaji wa maduhuli.

Alisema kuwa watu wanaopata maji safi na majitaka kwa Manispaa ya Moshi ni asilimia 97,na wanaopata huduma ya maji taka ni asilimia 46 kwa wakazi wote wa manispaa hiyo.

Lwenge alisema kuwa suala la huduma ya maji lipo kwenye mkakati wa kitaifa wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini(MKUKUTA)hivyo mamlaka zote nchini zinapaswa kutoa hudama hiyo na kuhakikisha zinapata cheti cha utoaji huduma bora kitaifa.

Hata hivyo alisema kuwa mamlaka zinajitahidi na kuendelea kutoa huduma,ambapo hivi sasa zimefika mamlaka 3 nchini rusha,Tanga na Moshi na kutaka mamlaka nyingine kuiga kwa ambazo zinafanya vizuri..

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Anthony Kasonta alisema kuwa tangu kuanza kutunukiwa cheti hicho katika mamlaka hiyo wameshaboresha mapungufu yaliyokuwepo ikiwemo ununuzi wa jenereta kwa ajili ya kutumika kuweka dawa ya kutibu maji kwenye vyanzo vya maji pindi umeme wa Tanesco unapokatika.

Kasonta alisema kuwa yapo mambo mengi ambayo yana umuhimu wa kuboreshwa lakiniutekelezaji wake unahitaji muda mrefu,kama kuboresha jingo la huduma kwa wateja,ofisi ya mfumo wa kukusanya maoni pamoja na mawasiliano kwa wateja na wadau.

                           Picha na habari zimewekwa na Rodrick Mushi wa tanzania leo

No comments:

Post a Comment