Friday, August 10, 2012

WANANCHI WALALAMIKIA ITIKADI ZA KISIASA KUGEUKA KISIKI CHA MAENDELEO.
Hapa Diwani wa Kata ya Kimochi,Anamenyisa Macha akishauri kuairishwa kwa mkutano wa wananchi baada mtendaji kushindwa kufika.

Mwananchi akitoa hoja ya kusikitishwa kushindwa kufika kwa mtendaji huyo wa Kijiji kwenye Mkutano.

Mkutano huo ilibidi ufunguliwe na kufungwa.
Wananchi wa kijiji cha mdawi Kata ya Kimochi,Wilaya ya moshi vijijini wamemlalamikia Mtendaji wa kijiji hicho Lenard Mende kwa kushindwa kuwepo ofisi siku za kazi,pamoja na kuwa mtoro kwenye mikutano ya Serikali,ambayo inakuwa na lengo la kujadili shughuli za maendeleo ya kijiji hicho.

Akizungumza baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo na kuahirishwa bila kujadili agenda yoyote wananchi walikuwa wamefika kwenye mkutano huo walisema kuwa hiyo ni mara ya pili kushindwa kufanyika kwa  mkutano baada ya mkutano uliofanyika jula 8 mwaka huu,mtendaji huyo kuondoka baada ya kuulizwa swali na mmoja wa wananchi.

Mkti wa kijiji cha mdawi Rumisha Kinyaa aliwaeleza wananchi waliokuwa wamefika kwenye mkutano huo ambao ulihairishwa agusti 4 mwaka huu, kuwa walikuwa wamempa taarifa ya uwepo wa Mkutano huo Mtendaji wa Kijiji,lakini hadi kufika muda wa mkutano hakufika.

Alisema kuwa hawataweza kuendelea na Mkutano huo,ilihali muwakilishi wa Mkurugenzi hayupo,hivyo agenda mbalimbalimbali ambazo zingejadiliwa kwa siku hiyo ingekuwa ni kazi bure kama wangefanya bila kuwepo kwa Mtendaji.

“Miongoni mwa mambo ambayo wananchi walikuwa wahoji kwenye mkutano huo ni pamoja na kutokufika kwa mtendaji huyo ofisini siku za kazi,jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wananchi wa kijiji,wakati yeye ameletwa kwa ajili ya kushirikiana na wananchi kuleta maendeleo”Alisema Kinyaa.

Kwa  wake Diwani wa Kata ya Kimochi,Anamenyisa Macha alisema kuwa changamoto nyingi zinazotokea kwenye kijiji hicho zinatokana na itikadi za kisiasa ambazo zinasababishwa na mvutano wa vyama vya siasa,pamoja na wananchi kupingana na kugawa kwa kijiji cha Mdawi.

Alisema kuwa kinachotakiwa ni wananchi na viongozi kuondoa itikadi zao na kuwatumikia wananchi,ili kuweza kuleta maendeleo,pamoja na kuchunguza malalamiko yalipo kwa wananchi kuwa hawakuhusishwa katika ugawaji wa kijiji hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi alipuulizwa kuhusiana 
na tatizo lililopo kwenye kijiji hicho cha Mdawi,alisema kuwa amebanwa na shughuli za mbio za Mwenge ambao ulikwua Mkoani Kilimanjaro,huku akiahidi kulifuatilia baada ya kumalizika kwa mbio za Mwenge.

No comments:

Post a Comment