Tuesday, May 22, 2012

WANANCHI WACHANGA SHILINGI MILLION 12 KWA AJILI YA UKARABATI WA BARABARA AMBAO HAIJAWAHI KUJENGWA TANGU UHURU..
Wananchi wa Kijiji ch mahime Kata ya Old Moshi Mashariki wakitandaza moramu kwenye barabara inayotoka kiboroloni hadi old moshi kidia baada ya kutopitika kwa muda mrefu hususani kipindi cha masika.

Wakijadiliana jambo na Diwani wa Kata hiyo ya Old Moshi Mashariki Aunwilfred Ringo aliyevaa tishrt nyeupu wa tatu kutoka kulia ambaye aliokuwa anawaongoza wananchi katika zoezi hilo la kukarabati barabara ambapo ni wiki ya 12 sasa wakifanya zoezi hilo.
Wananchi wa Kijiji cha Mahome Kata ya Old Moshi Mashariki wamechoshwa na ahadi ambazo wamekuwa wakiahidi viongozi akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Cyril Chami na kuamua kuchanga fedha zao mfukoni zaidi ya Shilingi million 12 kwa ajili ya ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilometa 4.7 ambayo imekuwa haipitiki kwa muda mrefu.
Wakizungumza na waandishi wa habari wakiwa kwenye zoezi la ukarabati wa barabara hiyo inayotoka eneo la kiboroloni kuelekea  Old Moshi Kidia  imekuwa haipitiki kwa muda  mrefu lakini pia imekuwa ikisababisha vifo vya akina mama na wagonjwa pamoja na wagonjwa wenye hali mbaya kwa kushidnwa kufikishwa hospitali kubwa kwa wakati.
Mmoja wa wananchi wa  Fatael Ulomo kutoka kwenye kijiji hicho alisema kuwa wakina mama wajawazito wamekuwa wakipoteza  maisha hususani wakati wa masika,licha ya kuwepo kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwenye kata hiyo  na taasisis zaidi ya tano zinazotegemea barababara hiyo.
Regnald Maro ambye ni mwenyekiti wa Mtaa alisema kuwa wananchi waliamua kuchaganga zaidi ya shilingi 10,000 kila mmoja na wengine kutoa hadi 300,000 baada ya  kuachoshwa na ahadi za uongo kutoka kwa viongozi mbalimbali  hivyo kuamua kuachana na siasa na kutumia feha zao wenyewe.
Kwa upande wa diwani wa Kata ya Old Moshi Mashariki Aunwilfred Ringo alisema kuwa wananchi wa Kata hiyo wameamua kujitokeza kwa kujitolea fedha zao pamoja na nguvu zao baada ya kuchoshwa na ahadi za viongozi wanaowachagua pamoja na Serikali kuahidi bila kuwepo na mafanikio kwenye ukarabati wa barabara hiyo.
Ringo alisema kuwa licha ya wananchi kuchanga kiasi hicho cha fedha lakini wana zaidi ya jumapili 12 wakijitokeza barabarani kwa ajili ya kuusambaza moramu ambao umemwagiwa barabarani ili kuweza kufanya shughuli zao za maendeleo pamoja na kuwaponywa wagonjwa ambao wamekuwa wakifariki kutokana na barabara hiyo kuwatopitika.
Hata hivyo Ringo alisema kuwa barabara hiyo haijawahi kutengewa fedha na halmashauri licha ya kuwa chini ya Halmashauri ya Moshi Vijijini,ambapo alibanisha kuwa kwenye bajeti iliyopitishwa na 2011/12 barabara hiyo imeombewa million 65 kwa ajili ya ukarabati wake.

Mwisho

No comments:

Post a Comment