Sunday, February 17, 2013

SENPAI SAMWEL KUTOKA KUNYANYUA VYUMA HADI KUMILIKI GYM.


Mcheza kareta na mkufunzi wa karate Senpai  Samueli (48)ambaye kwa sasa  ni mmiliki wa  Gym inayoitwa Sempay Fitness akifanya mazoezi kwenye gym yake iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.


Mwalimu wa kufundisha mazoezi kwenye gym ya Sempay Fitness Bonface Mutesa(kulia)akitoa maelezo kwa mwanachama ambaye anafanya 

SENPAI AELEZA UMUHIMU WA MICHEZO KWA MWILI WA BINADAMU.

Mazoezi yana umuhimu sana kwenye mwili wa binadamu,na inapendeza zaidi mtu anapoyafanya bila kusubiri kupewa maelekezo na daktari.

Wengi wanaopewa  maelekezo na daktari wanafanye mazoezi kwa sababu fulani za kiafya  unakuta wanafanya kama  adhabu na siyo kwa kupenda wenyewe.

Ni maneno ya mcheza kareta na mkufunzi wa karate Senpai  Samueli (48)ambaye kwa sasa  ni mmiliki wa  Gym(sehemu maalumu ya kufanyia mazoezi) inayoitwa Sempay Fitness iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Senpai hayuko mbali na tafiti mbalimbali ambazo zilikwishafanywa na wataalamu mbalimbali ambapo Dr. Jason na Nor Farah wa Chuo kikuu cha Glasgow  katika utafiti wake anasema kuwa mazoezi kwa ujumla wake yana umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu, hasa kama yakiambatana na lishe bora.

Mazoezi huweza kuzuia magonjwa sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo, kansa na shinikizo la damu, pia kwa kufanya mazoezi unaweza kuongeza kipato kwa kuwa unaweza kufanya kazi muda mrefu kuliko asiye fanya mazoezi.

Kwa jamii ambazo zimekuwa zikizingatia mazoezi zimekuwa familia bora na za mfano kuanzia kwenye maadili hadi kipato kwani kwa kufanya mazoezi familia zao zimeeza kujiepusha na magonjwa ambayo siyo ya lazima.

Kufanya mazoezi kila mara kuna faida nyingi ambazo haziwezi kuonekana kwa haraka, kama vile kuimarisha hali ya kiakili, ambayo matokeo yake ni kuwa na furaha,pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi.
Mazoezi  yanasaidia kuzalishwa kwa wingi kwa kemikali aina ya endorphins wakati wa kufanya mazoezi ambayo husaidia kwenye mapambano ya sonono (depression) na hivyo kumfanya mfanya mazoezi kuwa na furaha zaidi.

Kwenye jamii kumekuwa na upokeaji  tofauti juu ya  umuhimu wa mazoezi,huku wengi wakihusisha mazoezi kuwa ni kwa watu wenye pesa,wenye miili minene kitu ambacho Senpai anasema kuwa mazoezi ni kwa mtu yeyeyote yule ambaye anapenda kuimarisha mwili wake.
 “Ukifanya mazoezi unakuwa hauna muda wa kukaa kwenye makundi mabaya,na kuanza kujadili mambo ambayo hayana maana,mimi marafiki zangu wengine niliokuwa nao wamefariki na magonjwa mbalimbalimbali na  hii ni kutokana na kuwa kwenye makundi mabaya”Anasema Senpai

Wazo la kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi(GYM).
Senpai anasema kuwa alikuwa na wazo la kuanzisha gym kutokana na kupenda mazoezi lakini kuwepo kwa changamoto kubwa ya kutokuwepo kwa sehemu maalumu kwa ajili ya kufanyia mazoezi,na baadhi sehemu zilikuwepo kutokuwa na sifa kwa kutokuwa na waalimu pamoja na vifaa vya mazoezi.

Anasema kuwa yeye amefanya mazoezi ya kunyanyua vyuma na kucheza mchezo wa boksing  na hatimaye kuwa mwalimu wa karate tangu mwaka 1988 ambapo kwa sasa hivi ana mkanda mweusi.

“Mimi nilianza kwa kunyanyua tu vyuma mtaani lakini nikawa na wazo la kuanzisha gym yangu kwa ajili ya kuwafundisha watu mazoezi mbalimbali ila nilikuwa nikiwaza mbali zaidi kuwa nianzishe gym ya kisasa ambayo itakuwa na vigezo na mwalimu mwenye taaluma hiyo”Alisema.

Anasema wakati ananyanyua vyuma mtaani jamii nyingi hususani vijana waliamini kuwa kufungua gym au kufanya mazoezi ni kunyanyua vyuma pekee lakini yeye lengo lilikuwa ni kuweza kutoa huduma kwa rika zote kwa kuwa na mazoezi ya kila aina.

Kwa sasa anamiliki gym itwayo Sempay Fitness jina ambalo anasema kuwa linatokana na cheo alichonacho cha mwalimu au mkufunzi wa karante.

Gym ya Sempay fitness ipo uwanja wa saba saba Manispaa ya Moshi  ambayo inatoa mazoezi mbalimbali kwa rika zote ikiwemo vijana kwa wazee ambapo pia wapo wagonjwa wanaofika kwa kufanya mazoezi kama sehemu ya tiba.

Aina ya mazoezi yanayotolewa na Gym ya Sempay.
Uzuri wa gym mteja afike aweze kupata huduma aliyokuwa anahitaji kama alikuwa anataka kujenga mwili wake basi akute mashine hizo kama ni kupunguza mwili,au mazoezi ya kawaida basi aweze kupata mashine hizo.

Senpai anasem kuwa kwenye gym yake anatoa mazoezi mbalimbali kama  ya kujenga mwili(body bulding)Aerobics,Physical exercise,na mazoezi ya Cardio Machine ambayo yanaambatana na mazoezi yanayotumia mashine kama tradmill,upright Bicycle cross carble na four station machine ambazo mtu hufanya mazoezi kama anaendesha baiskeli na kukimbia.

Pia kuna mazoezi yanayoitwa Sauna,ni mazoezi ya kipekee kwani huwa na chumba chake maalumu na mitambo yake na unapoingia huko na kufungiwa basi mtu anatokwa na jasho bila kufanya mazoezi.

Aina hii ya mazoezi pia inapendwa na watu wengi kwani imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa kwa watu wanaofanya mazoezi hayo kutoka jasho ambalo huondoa uchafu mwilini.

Mazoezi mengine ni kama Stream bath ambayo pia kidogo ingefanana na sauna lakini yenyewe inatoa jasho lenye unyevunyevu pia bila kufanya mazoezi.

Mazoezi ya sauna na Stream bath yanapendwa na rika zote kutokana na mtu anapofanya mazoezi hayo anapojisikia vizuri kutokana na kusaidia kuondoa uchafu mwilini kwa njia ya vinyoleo.

Changamoto za kuanzisha Gym.
Senpai anasema kuwa changamoto kubwa baada ya kukamisha vifaa vyote vya mazoezi pamoja na nyumba yenye nafasi ya kutosha changamoto kubwa kwake ilikuwa ni mwalimu wa kufundisha mazoezi.

“Nilipoanza nilipata shida kwenye mwalimu,japo mimi mwenyewe ni mwalimu mzuri lakini nikawa ninakabiliwa na majukumu mengine hivyo ikanilazimu kuwa na mwalimu wa ha watu mazoezi”Anasema.

Anasema kuwa walimu wa mazoezi ambao wana taaluma hiyo wanapatikana kwa shida,ambapo mwalimu wa kwanza alimtoa Jijini Dar es Salaam,lakini hakuweza kukaa nae kwa muda mrefu baada ya kujiingiza kwenye makundi mbaya na kushindwa kufuata taratibu za kazi.

Changamoto nyingine ni pamoja na kutokuwepo kwa wataalamu wa kutengeza mashine ambazo zinatumika kwa ajili ya kufanyia mazoezi.
Lakini awali kabisa changamoto kubwa ilikuwa ni watu wengi kutohamasika kufanya mazoezi,tena kwa kulipa wanaona kuwa wanatumia garama kubwa,lakini kwa sasa wapo watu ambao wameelimika na kuhamasika kutumia pesa na muda wao kufanya mazoezi.
Senpai anasema kuwa biashara ya gym imekuwa ngumu kwani ni biashara ngeni ambayo wachache ndio wanauelewa juu yake pamoja na umuhimu wake.
Samuel kwenye gym yake kuna wateja wa rika tofauti lakini rika la watu wazima ndio wamehamasika zaidi ambao idadi yake ni kubwa ya wanaofika kufanya mazoezi kwenye gym hiyo.

Malengo ya baaday baada ya kuanzisha gym.
Senpai anasema kuwa malengo yake ya baadae baada ya kuanzisha gym ni kuanisha darasa la karate kwa watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 7-14 kwani kufundisha vijana wakubwa huwa na changamoto mbalimbali.

Anasema kuwa analazimika kuanza darasa la vijana wenye umri huo kwani anaweza kuanza nao tangu wakiwa darasa la kwanza hadi la saba,lakini kufundisha wenye umri zaidi ya hapo inakuwa vigumu kwani wakishajiunga na elimu ya sekondari hupangiwa sehemu za mbali.

Lakini anatoa wito kwa jamii kujijengea tabia ya kufanya mazoezi hata kwa wale wanaobanwa na majukumu ya kikazi kujitengea muda kidogo kwa ajili ya kufanya mazoezi ambayo pia husaidia kuongeza ufanini kazini kwa kuongeza uwezo wa akili kufanya kazi na kufikiri.

2 comments:

  1. TAFADHALI, ninaomba e-mail ya Senpai Samwel
    chizzymorento20026@gmail.com

    ReplyDelete
  2. TAFADHALI, ninaomba e-mail ya Senpai Samwel
    chizzymorento20026@gmail.com

    ReplyDelete