Tuesday, May 22, 2012

SHRI SWAMINARAYAN MANDIR WAFUNGUA MSIKITI ARUSHA

Muonekano wa msikiti huo kwa nje.


 apa afisa uhusiano wa Shri  Swaminarayan Mandir akifafanua jambo kuhusiana na mkubwa wao mbele ya waandishi wa habari

Dini ya hindu kupitia dhebhebu la shri swaminaraya imeahidi kutoa elimu kwa waumini wake pamoja wananchi wasiowahumini kuhusiana na sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika mapema mwezi agosti.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisa uhusiano wa dhehebu hilo Kaushik Vasan alisema kuwa dini yao ipo tayari kutoa ushauri kwa waumini wao pamoja na wananchi kwa ujumla ili kuweza kubaini nini maana ya sensa ambapo pia watawahamasisha wananchi hao kushiriki zoezi hili siku hiyo.

Alisema kuwa pia kwa kutumia sherehe hizi za uzinduzi wa jengo lao la msikiti wao ambao wameujenga jijini hapa ambao wanatarajia kuzindua jana (leo) watahamasisha watu wote ambao watahudhuria sherehizo  kushiriki zoezi hili.

Vasan alisea kuwa kutokana na umuhimu wa sensa hiyo ya watu na makazi wataisaida serikali katika kuhamasisha waumini wake na wakazi wa jiji hili kwa ujumla juu ya umuhimu wa kujiandiksha kwakati wa sensa.

Aongelea uzinduzi wa msikiti huo alisema kuwa mgeni rasmia anatarajiwa kuwa Ghanshyam Charan Swami ambaye ni mmoja wa wasaidizi wa kiongozi wao mkuu wa dini hiyo ambaye ni HDH,Pramukh Swami Maharaj(91) aishiye nchini India.

Alibainisha kuwa katika uzinduzi huo wanatarajia zaidi ya wageni 800 kutoka  nje ya nchi ambao watafika kusherekeapamoja zoezi hilo ,huku akibainisha kuwa mbali na masuala ya kiima  wanajikita pia katika kusaidia jamii ikiwepo kupanda miti kwa ajili ya mazingira ,kutoa huduma mbalimbali za kijamii kama vile kusaidia hospitali mbalimbali vifaa ,pamoja na kuwasomesha watoto yatima na wale ambao wanaishi katika mazingira hatarishi



                                         Habari kwa hisani ya Libeneke la Kaskazini  

 

No comments:

Post a Comment