Sunday, March 25, 2012



Uongozi wa Elimu Jimbo Katoliki la Moshi,waeleza kusikitishwa na mmonyoko wa maadili kwa wanafunzi.

MKURUGENZI WA ELIMU JIMBO KATOLIKI LA MOSHI(KULIA)FATHER WILLIUM RUAICHI.

MWEZESHAJI KWENYE SEMINA HIYO,WANAOONEKANA NI WAALIMU WAKUU,WAKUU WASAIDIZI,NA WAALIMU WA NIDHAMU KUTOKA SHULE 31 ZA SEKONDARY ZINAZOMILIKIWA NA KANISA KATOLIKI..


 Uongozi wa Elimu Jimbo Katoliki la Moshi,umeeleza kusikitishwa na mmonyoko wa maadili kwa vijana hususani wanafunzi,huku wakisema kuwa hawapo tayari kulifumbia macho suala hilo bali wataanza kwa kuwawajibisha baadhi ya waalimu ambao wamekuwa wakikikua maadili,ikiwemo uvaaji wanapokuwa makazini ikifuatiwa na wanafunzi.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa elimu Jimbo katoliki la Moshi,Fatha Willium Ruaichi wakati wa semina iliyofanyika kwenye jimbo hilo kwa lengo la kuwawezesha wakuu wa shule za sekondari,wasaidizi wao,pamoja na waalimu wa nidhamu kwa shule zinazomilikiwa na kanisa katoliki.

Hata hivyo kutokana na mmonyoko wa maadili kuongezeka kwa kasi,ambapo pia waalimu nao walilalamikiwa kwenye semina hiyo kwa kuvaa nguo ambazo haziendani na maadili,Mkurugenzi huyo alisema Waalimu ambao watakuwa wanakinzana na taratibu za mavazi zilizowekwa na uongozi wa kanisa basi basi watasitishiwa mikataba yao.

Ruaichi alisema katika kusimamia madili ya wanafunzi waalimu wana nafasi kubwa kuhakikisha wao wanakuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi hao,ndipo kuweza kuwawajibisha wanafunzi ambao wamekuwa wakivaa sare za shule ambazo haziendani na maadili yaliyowekwa na kanisa hilo.

Alisema kuwa uvaaji wa waalimu unatakiwa kufuata maadili ya shule,kutokana na maadili ya shule kutotofautiana na yale ya Wizara ya elimu,ili kuweza kupiga vita uvaaji mbovu kwa wanafunzi ambao zinawaacha sehemu ya miili yao wazi ambao wamekuwa wakiadhiriwa na utandawazi.

“Shule za dini tunatakiwa kuwa mfano wa kuiga katika mambo ya maadili,na suala hili tumekuwa tukilitilia mkazo sana,lakini wakati mwingine wakuu wa shule wamekuwa wakituangusha katika usimamizi”Alisema Ruaichi.

Mwisho

No comments:

Post a Comment