Monday, June 11, 2012

Rais Dkt.Jakaya Kikwete ashiriki kumuaga Muasisi wa CHADEMA Bob Makani katika viwanja vya Karimjee leo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal pamoja na Mama Salma Kikwete leo waliungana na viongozi wa CHADEMA na viongozi wengine wa kitaifa kutoa heshima zao za mwisho kwa mmoja wa waasisi wa CHADEMA marehemu Bob Makani ambayepia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo ya Naibu Gavana wa Benki kuu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.(picha zote na Freddy Maro)
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe wakati wa kuaga mwili wa Muasisi wa chama cha CHADEMA marehemu Bob Makani
Rais Dkt.Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wakibeba jeneza la marehemu Bob Makani
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za Mwisho
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiteta jambo na mjumbe wa tume ya kukusanya maoni juu ya katiba Prof.Mwesiga Baregu katika viwanja vya Karimjee leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa katika viwanja vya Karimjee kufuatia msiba wa muasisi wa Chama hicho Bob Makani

No comments:

Post a Comment