Thursday, February 21, 2013

HITIMISHO LA ZIARA YA KIBAKI.


 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini, wakisiliza taarifa ya pamoja ikisomwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 
Vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini wakisimama kupokea heshima wakati nyimbo za taifa zikipigwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 
Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini akiagana na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali aliye pamoja na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda pamoja na viongozi wengine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 PICHA NA IKULU

Tuesday, February 19, 2013

ALICHOKIANDIKA ZITO KUHUSIANA NA MATOKEO MABOVU YA KIDATO CHA NNE.



                                                              Zitto Kabwe

MATOKEO ya Kidato cha Nne ya namna hii (zaidi ya nusu ya wahitimu kupata sifuri) na takriban asilimia 90 kufeli kwa kupata daraja la nne na daraja la sifuri sasa ni mwaka wa tatu mfululizo.
Matokeo yakitoka tunasema weeee mpaka povu linatoka. Baada ya wiki tumeshasahau na hakuna hatua yeyote.
Lazima Uwajibikaji utokee. kwanza Waziri Shukuru Kawambwa lazima awajibike na Naibu wake na Katibu Mkuu na Kamishna.
Najua kuwa haina uhusiano wa moja kwa moja maana matatizo ya elimu ni makubwa sana nchini.
Lakini ni lazima kitu fulani kitokee ili kufanya mabadiliko.
Uwajibikaji ni njia mojawapo inayoleta nidhamu na uharaka katika utendaji kazi.
Tumwambie Rais aichukue Wizara ya Elimu, yaani Waziri wa Elimu awe yeye (kuwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Elimu).
Tumwambie matokeo yakibaki hivi mwakani na yeye atatoka. Najua wa mwakani ndio wako kidato cha nne sasa na wana msingi mbaya tayari lakini sio jukumu letu kujipa majibu bali ni jukumu letu kuiambia serikali hapana. Tuipe masharti. Vinginevyo haya yatakwisha na mwakani yatarudia tena.
Hawa watoto wanakwenda wapi? Mwaka jana tulisema mpango wa kujenga vyuo vya ufundi kila halmashauri ya wilaya uanze mara moja.
Katika Bajeti Kivuli mwaka 2011 tulipiga hesabu kwamba tunahitaji sh 720 bilioni katika kipindi cha miaka mitano ijayo kujenga vyuo vya ufundi vya VETA kila wilaya.
Tukawaambia badala ya kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kulipana posho ni vema tukope kuwekeza kwenye elimu maana elimu ni hifadhi ya jamii.
Elimu yetu ya sasa inazalisha matabaka kwenye jamii na ni hatari sana kwa uhai wa taifa.
Tunaweza kujidai kujenga madaraja na miji mipya. Tunaweza kujidai kujenga mabomba ya gesi na kusambaza umeme kila kijiji mpaka kwenye vyoo.
Kama hakuna elimu haya yote ni bure kabisa. Hata kukosa uvumilivu wa kiimani sasa hali itakuwa mbaya zaidi unapokuwa na taifa la mbumbumbu.
Waziri Kawambwa na wenzake watoke na watoke sasa.
SOUURCE Tanzania Daima

Mwandishi wa makala hii ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

MTOTO ALIYENUSURIKA KIFO BAADA YA NYUMBA ALIYOKUWA KUTEKETEA KWA MOTO.


 Mtoto Ombeni Mbeula ambae ameungua kwa moto vibaya kama anavyoonekana anahitaji msaada  wako.Wadau samahani kwa picha hizi

 

                                      Mama wa mtosto Kilaudia Kigailaakiwa na mwanae huyo.
HUJAFA hujaumbika bado mtoto Ombeni Mbeula amenusurika kifo baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuteketea kwa moto  wakati mtoto huyo akiwa ndani baada ya mama wa  mtoto huyo kuwaacha watoto hao na kwenda shamba eneo  Chitemo wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma.
Imedaiwa kuwa moto huo ulitokea wakati mvua inanyesha ghafla nyumba ilibomoka na wakati huohuo walikuwa watoto wawili walikuwa jikoni ndani ya hiyo nyumba na ndipo  kijana huyo alipotetekea kwa moto
Baada ya tukio hilo kutokea   ikafanyika uokoaji kwenye nyumba hiyo maeneo ya Chitemo na kufanikisha   kuokoa watoto wote wawili kati ya mmoja aliumia kwa kuangukiwa na udongo wa nyumba hiyo na huyu Ombeni Mbeula aliangukia kwenye moto mpaka kuungua hivi unavyoona kwenye picha lakin hali zao ni salama kwa wote.
Baada ya uokoaji waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospitali ya Mima iliyoko Mpwapwa ikashindikana madaktari wakamuagiza aende hospitali ya Mpwapwa hapo hospitalini wakakaa siku mbili katika hospitali ya mpwapwa  na siku ya tatu wakaambiwa waende hospitali ya rufaa iliyoko Dodoma Mjini ambayo ni inajulikana General kwa matibabu zaidi.
Walipofika katika hospitali ya mkoa wa Dodoma wakaanza matibabu lakini uwezo wa kipato cha wazazi wake sio kizuri inahitajika msaada kwa matibabu maana hata dawa hajapatiwa na pesa kwa ajili ya matibabu  haikuweza kupatikana paka sasa
Kama umeguswa kutoa ni moyo sio utajiri muokoe mtoto huyu maana hata kula anashindwa mpaka kuona anaona kwa mbali sana.
Mama yake hana simu lakini anatumia simu ya  ndugu yake Ekiria Paskali
Kwa yeyote atakayependa kumchangia mtoto huyo atume chochote kwenye namba hii au atumie M- pesa kwenye namba hii 0757 498336
PICHA KWA HISANI YA PAMOJAPURE BLOG

ZIKIWA ZIMEPITA SIKU CHACHE TANGU KUUAWA KWA PADRE MUSHI WATU WANAOSIOJULIKANA WASHAMBULIA NA KUCHOMA KANISA. NA PICHA ZAKE JINSI LILIVYOTEKETEA


 





Hapa ni mabaki ya vitu mbalimbali vilivyoungua kwa ndani.

 Ikiwa ni siku chache zimepita tangu kuuwawa kwa risasi kwa padre Evarist Mushi huko Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadae kulichoma moto kanisa la Walokole la Shaloom lililoko Kiyanga kwa Sheha mkoa wa kusini Unguja Zanzibar.

Kamanda wa polisi mkoa wa kusini Unguja Agustino Ulomi amesema hilo tukio limetokea jana saa tisa na nusu usiku, ambapo huo moto ulianza kuwaka baada ya vijana watatu walioonekana karibu na kanisa, baadae kidogo ndio mlinzi akaanza kusikia mawe yakirushwa juu ya bati.

Baada ya mlinzi kuona hatari ilibidi akajifiche lakini kwa mbali akawa anaona kinachoendelea, moto ukiendelea ndio akampigia simu kiongozi wa kanisa ambae aliwapigia polisi, wakaja wakawa wanashirikiana na wananchi kuuzima japo tayari ulikua umeshaunguza samani mbalimbali za kanisa hilo, kilichosaidia kanisa hilo kutoungua lote ni vifaa imara vilivyotumika kulijenga.

Katika ripoti hii ambayo imeripotiwa na mwandishi wa habari Cathbert Kajuna wa kajunason.blogspot.com bado hajakamatwa mtu yeyote mpaka sasa, polisi wamesema pia wanaanza utaratibu wa ulinzi wa makanisa kutokana na vitisho vilivyopo sasa hivi.

Hakuna mtu yeyote aliejeruhiwa katika tukio hilo lililotokea saa tisa usiku wa kuamikia leo,

Monday, February 18, 2013

KWA MATOKEO HAYA KWA NINI WIZARA HUSIKA ISIJIUZULU?

Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806. “Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.
Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67 lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na asilimia 95.44, wengine 21,820 (asilimia 4.55) hawakufanya mtihani.
Alisema watahiniwa wa shule (school candidates) walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57, miongoni mwao, 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo utoro, ugonjwa na vifo.
Ufaulu kwa madaraja
Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni 1,641, wavulana wakiwa 1,073 na wasichana 568, daraja la pili ni 6,453, wavulana wakiwa 4,456 na wasichana 1,997.

Waliopata daraja la tatu ni 15,426, wavulana 10,813 na wasichana 4,613, waliopata wa daraja la nne 103,327, wavulana 64,344 na wasichana 38,983 huku waliopata sifuri wakiwa 240,903, wavulana 120,664 na wasichana 120,239.
Shule 20 bora
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wizara ilitaja shule 20 zilizofanya vizuri badala ya 10 kama ilivyozoeleka, kati yake 18 zilikuwa za watu binafsi na mashirika ya dini na mbili za Serikali.

Shule hizo ni pamoja na St.Francis Girls ya Mbeya, Marian Boys ya Pwani, Feza Boys ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Rosmini ya Tanga, Canossa ya Dar es Salaam, Jude Moshono ya Arusha, St. Mar’s Mazinde Juu ya Tanga, Anwarite Girls ya Kilimanjaro na Kifungilo Girls ya Tanga.
Nyingine ni Feza Girls ya Dar es Salaam, Kandoro Sayansi Girls ya Kilimanjaro, Don Bosco Seminary ya Iringa, St. Joseph Millenium ya Dar es Salaam, St. Iterambogo ya Kigoma, St. James Seminary ya Kilimanjaro, Mzumbe ya Morogoro, Kibaha ya Pwani, Nyegezi Seminary ya Mwanza na Tengeru Boys ya Arusha.
Shule 10 za Mwisho
Kwa upande wa shule 10 za mwisho, iliyofanya vibaya zaidi ni Mibuyuni ya Lindi, Ndame ya Unguja, Namndimkongo ya Pwani, Chitekete ya Mtwara, Maendeleo ya Dar es Salaam, Kwamndolwa Tanga, Ungulu Morogoro, Kikale ya Pwani, Mkumba na Tongoni za Tanga.

Matokeo yaliyofutwa
Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na udanganyifu na kuandika matusi.

Baadhi ya udanganyifu huo ni karatasi za majibu kuwa na mfanano usio wa kawaida, kukamatwa na simu za mkononi kwenye chumba cha mtihani, kukutwa na karatasi au madaftari pamoja na kubadilishana karatasi za majibu.
Dk Kawambwa alisema matokeo ya watahiniwa 28,582 yamezuiwa kwa sababu ya kutolipa ada ya mtihani na wanatakiwa kulipa fedha hizo ndani ya mwaka mmoja.
Matokeo ya QT
Dk Kawambwa alisema waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Maarifa (QT) walikuwa 21,310, wasichana 13,134 na wavulana 8,176 na waliofanya ni 17,137 sawa na asilimia 80.42… “Watahiniwa 5,984 kati ya 17,132 waliofanya mtihani huo wamefaulu.”…read more
Source: Mwananchi

MAMA SALMA: RAIS KIKWETE ANA HASIRA, WANAOSEMA MPOLE HAWAMJUI

salma pps
NA BASHIR NKOROMO, LINDI
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCN, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoboa siri kwamba mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura yake kujawa haiba ya ucheshi wa mara kwa mara lakini kwa tabia ana hasira.
Amesema, Rais Kikwete hukasirika sana anapoona au kusikia mtu au mtendaji katika Chama au serikali anafanya mambo ya hovyo au ya kizembe hasa katika masuala ya kazi.
Mama Salma Kikwete ametoboa siri hiyo, leo Februari 18, 2013, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa katika ziara ya kukagua, kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua kuwa mjumbe wao wa NEC.
“Siyo kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete siyo mkali, japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ni ana hasira, tena  sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo ya hovyo ay ya kizembe katika kazi za Chama au serikali yake”, alisema Mama Salma Kikwete.
Mama Kikwete akitoa ufafanuzi, baada ya mshereheshaji mmoja kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Lindi mjini Muhsin Ismail, kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete ni mpole wa kupindukia na kuuliza umati wa wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo kwamba je ni nani amewahi kumuona amenuna.
“Natoa ofa kama hapa kuna mtu aliyewahi kumuona mpendwa wetu, Rais Kikwete amenuna anyooshe mkono. Akitokea ntampa sh. elfu moja hapa hapa… Kwa mara ya kwanza, ya pili unaona hakuna”, alisema Muhsini.
Wakati akiendelea kusema hivyo, mtu mmoja kwenye mkutano huo alinyoosha mkono, lakini Muhsin akakataa kumpa zawadi yake kama alivyokuwa ameahidi. “Aaa wewe sikupi zawadi”, alisema Muhsini lakini papo hapo akakatishwa na Mama Mama Kikwete.
“Hata kama humpi hiyo zawadi, sawa. lakini Siyo kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete hakasiriki na siyo mkali. Japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ana hasira, tena  sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo ya hovyo ay ya kizembe…” alisema Mama Kikwete.

KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012.


TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF



tff_LOGO1
SIMBA YAINGIZA MIL 134/-, AZAM MIL 34/-
PAMBANO la Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Libolo FC ya Angola lililofanyika jana (Februari 17 mwaka huu) limeingiza sh. 133,795,000 wakati lile la Kombe la Shirikisho kati ya Azam na El Nasir ya Sudan Kusini lililochezwa juzi (Februari 16 mwaka huu) limeingiza sh. 34,046,000.
 Watazamaji 22,469 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Simba kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Simba ilipoteza pambano hilo kwa bao 1-0.
 Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za waamuzi sh. 24,926,500, gharama za tiketi sh. 7,410,000, asilimia 15 ya uwanja baada ya kuondoa gharama za waamuzi na tiketi ilikuwa sh. 15,218,775, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 10,145,850 na asilimia 75 iliyokwenda klabu ya Simba ni sh. 76,093,875.
 Mechi ya Azam iliyomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 ilishuhudiwa na watazamaji 13,431 kwa viingilio vya sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000. Mgawo katika mechi hiyo ulikuwa kama ifuatavyo;
 Gharama za tiketi sh. 4,779,000, asilimia 15 ya uwanja baada ya kuondoa gharama za tiketi ilikuwa sh. 4,390,050, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 2,926,700 na asilimia 75 iliyokwenda Prime Time Promotions (Azam) ni sh. 29,267,00.
 PONGEZI KWA UONGOZI MPYA SPUTANZA, FRAT
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Wachezaji Mpira wa Miguu Tanzania (SPUTANZA) na wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) uliochaguliwa wiki iliyopita.
 Uongozi wa FRAT ulichaguliwa Februari 13 mwaka huu mjini Morogoro wakati wa SPUTANZA ulichaguliwa jana (Februari 17 mwaka huu) katika uchaguzi uliofanyika Kigamboni, Dar es Salaam.
 Waliochaguliwa kuongoza SPUTANZA na hawakuwa na wapinzani ni Musa Kissoky (Mwenyekiti) na Said George (Katibu Mkuu) wakati Ali Mayai aliwashinda Isaac Mwakatika na Hakim Byemba katika nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF.
 Kusianga Kiata na Charles Mngodo walichaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya SPUTANZA. Katika uchaguzi huo uliohudhuriwa na wapiga kura 17, Mhazini na nafasi moja ya mjumbe wa Kamati ya Utendaji zitajazwa baadaye kutokana na kukosa wagombea.
 Kwa upande wa FRAT viongozi waliochaguliwa ni Said Nassoro (Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu Mkuu) na Kamwanga Tambwe (mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF).
 Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza vyama hivyo unaonesha jinsi wapiga kura walivyo na imani kubwa kwao, na TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya FRAT na SPUTANZA.
 Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba zao pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yao.
 Pia tunatoa pongezi kwa kamati za uchaguzi za FRAT na SPUTANZA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi umeendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

MSIGWA ATOA TENA NAMBA ZA SPIKA MAKINDA.

SOKONI bfa35
Akiwahutubia wananchi na wapenzi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo katika mkutano wa hadhara uliofanyikia eneo la sokokuu  manispaa ya iringa.
Mchungaji Peter Msigwa akiongea na wananchi alisema wameamua kuongea lugha itakayo eleweka kwa spika na wabunge wa ccm wakiwabungeni ili wafikishe ujumbe waliotumwa na wananchi.

Akifafanua zaidi kuhusu hilo kasema   wao wabunge  kutoka Chadema hawana tena mtindo wa kutoka Bungeni pindi wanaponyimwahaki ya kikatiba wawapo Bungeni. kwapamoja wanawasha vipazasauti na kusimama kwapamoja kuhakikisha matakwayao yakimsingi yanasikilizwa.
Moja ya mamboyalio kera sana katika Bunge lililo isha hivi kalibuni ni kufutwa kwa Hojabinafsi zilizo tarajiwa kuwasilishwa pomoja yakuwa vigezona mashariti walikamilisha hukuyeye akiwana Hojayake inayohusu Maliyaasili yetu juu ya Uwindaji haramu na nanamna vyombo vya Dola vinavyohusika na Ujangili.

Mh Msigwa alisema tofauti iliopo katiya wabunge wa ccm na wao wa chadema nihii ccm wanafikilia miaka mitano kumi ijayo kwa mipango ya matumbo mbele maendeleo nyuma.
Wakati Chadema wanafiri miaka hamsini au mia ijayo kwamaendeleo ya vizazi vijavyo huku wakisititiza nguvu ya umma ilete mabadiliko katika nchihii.

Sambamba na hilo alisema anashangaa wanasiasa wa ccm wanafikilia uchaguzi wa 2015 wakatiyeye  anashughulikia namnayakuwakilisha hoja na shida za wananchi wajimbo la Iringa.
 Akiongeakwa uchungu anasema hayupotayali kuwamtii kwayeyote wa ngaziyoyote kwa mambo ambayo yanawakandamiza wananchi katikanchihii.
 Kwaniyeye aliaminiwa na wananchi na kamwe aliahidi hatowaangusha kwakuenda Bugeni na kukaa kimya akiangalia mamboyanavyoendasivyo.

Mwisho alikaribisha maswali kutokakwa wananchi na akawatajia namba za simu zote za Mh Spikawa Bunge la Jamuhuli ya Muungano la Tanzania Anne Makinda pamoja naza naibu spika wa Bunge Ndg Jobu Ndugai. Nakutahadhalisha sio kwa kuwatukana kwakuwa hato husika ila kwamatumizi ya msingi kwamaendeleo ya nchi.

KIPANYA CHA LEO.









kp18022013 f446b
Wakati Bunge letu likiendelea kuyumba kwa kuwepo kwa malalamiko mbalimbali embu angalia kwa makini katuni hii.



CHADEMA KUITIKISA ARUSHA LEO


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo kinafanya mkutano mkubwa wa hadhara Arusha,ambao pia utatumika kuzindua utekelezaji wa sera yake ya utawala wa majimbo kwa kuzindua Jimbo la Kaskazini.
Katibu wa Muda wa Kamati ya Uratibu Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema mkutano huo utafanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro na utahudhuriwa na wabunge wote wa Chadema kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini na kuhutubiwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe. Kwa mujibu wa Golugwa, Kanda ya Kaskazini inajumuisha mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.
“Tunazindua Kanda ya Kaskazini kutekeleza uamuzi wa Baraza Kuu lililoagiza mfumo na shughuli za uendeshaji wa chama ushuke hadi ngazi ya majimbo ambayo ndiyo sera ya Chadema,” alisema Golugwa.
Kabla ya mkutano wa leo, viongozi zaidi ya 200 wa Chadema kutoka mikoa na majimbo 30 ya Kanda ya Kaskazini wakiwamo wabunge, wenyeviti, makatibu, wenyeviti na mameya wa Halmashauri zinazoongozwa na Chadema,walifanya vikao vya ndani kuweka mikakati na mfumo wa utendaji kikanda. Kwa mujibu wa Golugwa, ambaye pia ni Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, kikao cha ndani pia kilihudhuriwa na mwasisi na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei.
Mbowe ambaye ni mmoja wa wajumbe waliohudhuria vikao vya ndani, ndiye atakuwa mgeni rasmi na mzungumzaji mkuu kwenye mkutano wa hadhara ambao pia utatumika kuwatambulisha wajumbe wa timu ya uratibu ya Kanda ya Kaskazini.
Mkutano huo ni wa pili kwa Chadema ndani ya wiki mbili zilizopita baada ya kufanya mkutano mkubwa Dar es Salaam uliotumika kuueleza umma udhaifu wa mhimili wa Bunge na ukandamizaji  unaodaiwa kufanywa dhidi ya wabunge wa chama hicho na uongozi wa mhimili huo wa dola.
Katika mkutano huo, viongozi wa Chadema waliutangazia umma namba za simu za Spika Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai ili wananchi wawapigie au kuwatumia ujumbe mfupi kuwashinikiza kufuata Katiba, Sheria na Kanuni za bunge katika uendeshaji na maamuzi ya chombo hicho.

UJANGILI WACHAFUA SIFA YA TANZANIA KWA NCHI ZA ULAYA NA ASIA.

Picha kwa Hisani ya Maktaba.


SERIKALI ya Tanzania inahusishwa na vitendo vya ujangili na uuzaji wa meno ya tembo nje ya nchi.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wake na wadau wa sekta ya utalii kwenye ukumbi wa hoteli ya Mount Meru jijini Arusha alisema tatizo hilo limeichafua nchi.

Alisema kwa nchi za Marekani na barani Asia sifa ya Tanzania kwa suala la ujangili ni mbaya kwa kuwa inahusishwa na vitendo hivyo vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya watu wa ndani na nje ya nchi.

“Hatuwezi kukubali kubeba sifa mbaya hiyo.. wanatusema sana wenzetu huko nje…hata wadau wa sekta ya utalii kwenye kikao wamesema…wakihusisha baadhi ya watendaji wa serikali na mtandao huo”alisema.

Kagasheki alisema mtandao wa ujangili ni mkubwa tena unatumia silaha za kivita ambazo zinatishia uhai wa askari wa hifadhi hizo na kuwa tayari mkakati wa kuunganisha nguvu za pamoja umekamilika ili kuhakikisha wanatokomeza mtandao huo.

“Ni mtandao mkubwa lakini hautatushinda lazima utokomezwe maana tusipofanya hivyo sifa tulizopata kwa vivutio vyetu kushinda kwenye mashindano ya vivutio bora vya asili Afrika hautakuwa na maana …lazima tulinde raslimali hizi zinazochangia pato kuwa kwa taifa”alibainisha.

Aliwaonya baadhi ya watumishi wanaoshirikiana na wahujumu uchumi kuwa hatua kali zitachukuliwa kwao,huku akisisitiza kuwa wanakusudia kurekebisha sheria ili ziwe kali kwa wanaokamatwa kwenye makosa hayo.

Kuhusu suala la silaha zinazotumiwa na majangili alisema zinatishia usalama wan chi kwa kuwa wanatumia silaha kali za kivita ambazo zinatakiwa kudhibitiwa.

Alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa idara yake imejipanga kusafisha watendaji wasiokuwa waadilifu kwa kuwa baadhi ya wadau wa sekta ya utalii wameishapoteza imani na idara hiyo kutokana na urasimu wa watendaji kitendo alichosema atakikomesha mara moja.

Februari 11 mwaka huu Vivutio vya Mlima Kilimanjaro,Bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti zilitangazwa kuwa washindi kwa vivutio vya maajabu saba ya asili.

Mbali na hivyo pia mto Nile kwa Uganda,maporomoko ya Zambia,Jangwa la Sahara vilikuwa miongoni mwa vilivyoshinda ,mashindano yaliyoandaliwa na shirika la Seven Natural Wonders of Afrika la Taxes Nchini Marekani ,ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikabidhi tuzo kwa washindi.
          Na Anthony Mayunga-Arusha.
 
Mwisho.

Sunday, February 17, 2013

AARYAN A SEVEN YEARS OLD BOY WHO BECOME A YOUNGEST MOUNTAINEER AFTER SUCCESSFUL TO CLIMB MOUNT EVAREST UP TO BASE CAMP,CLIMB MOUNT KILIMANJARO TODAY.




Speaking in an interview with Journalist in Tanzania(are not in the picture) yesterday Child Aaryan Balaji (7)from India who put the history of mountain climbing longest in the world, Mount Everest prevailing in Nepal and succesefully to reach the top, today has begun the journey to climb Mount Kilimanjaro via the Lemosho existing District Siha.

A group of more than eight people out of which six will ascend Mount Kilimanjaro, (right are the parents of son Aryan) Balaji and mum Riki and three from the right is the son Aaryan who is a child under the age of 7 years, who shall ascend the mountain Kilimanjaro after successfully climbing Mount everest few months years.

Director of tourism company based in Arusha Easy Travel ltd, Musaddiq Gulamhussein(left side)and (midle)is  the Child Aaryan Balaji (7)from India who put the history of mountain climbing longest in the world, Mount Everest prevailing in Nepal and succesefully to reach the top,(right side)is the tour gaide of the easy travel safari.



                                                                         Rodrick Mushi.
 Child Aaryan Balaji (7)from India who put the history of mountain climbing longest in the world, Mount Everest prevailing in Nepal and successfully to reach the top, today has begun the journey to climb Mount Kilimanjaro via the Lemosho existing District Siha.

Speaking in an interview with reporters yesterday about the child Aaryan said the trip to climb Mount Kilimanjaro has organized properly to make sure he reaches the top, although he knows he will face difficult weather conditions, as was the case with Mount Everest.

Aaryan said that is not an easy task to climb the mountain, which is the longest in Afrika, but because he has committed shall endeavor as much as he will be able to achieve its goals to up to heights as he wrote a history of the first child to climb Mount Everest to reach the top.

He said the trip of Mount Everest  facing various challenges including large ice and rock climbing and sleeping in tents, but he managed to reach the top due to the contribution which he had received from his parents, especially given the exercises together and encouraged.

"I'm very happy to see when I was seven years old only I could write the history of the world to climb Mount Everest, which is the world's longest, I wish every child will realize they can everything if their parents helping them, "he said Aryan

"My father Balaji, has been taught various exercises before I climbed Mount Kilimanjaro Evarest and now I have enough practice with my mom encouragement that every good thing I did sight there is a way to success," he added Aryan.

By his mother's side of Aryan had accompanied him in favor of a trip to climb Mount Kilimanjaro, Riki Balaji said that the aim of his son to climb Mount Kilimanjaro is to encourage other parents to see their children can achieve their goals of talent.

Riki said some parents do not have time to spend with their children and listen to their needs and goals, including encouraging in various fields in order to achieve all that they expect in their lives.

And the director of tourism company based in Arusha Travel Easy, Musaddiq Gulam hussein said the trip was cordinated with his company in partnership with G.Adveture company based in Canada.

Musaddiq said this trip is for six people will climb for  ten days, where they are fully prepared to do enough exercise, and explained that the issue of reach heights depends on the weather, where the leader of the expedition from the company of Easy Travel Philemini Chacha who is familiar with tourist guides.

SENPAI SAMWEL KUTOKA KUNYANYUA VYUMA HADI KUMILIKI GYM.


Mcheza kareta na mkufunzi wa karate Senpai  Samueli (48)ambaye kwa sasa  ni mmiliki wa  Gym inayoitwa Sempay Fitness akifanya mazoezi kwenye gym yake iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.


Mwalimu wa kufundisha mazoezi kwenye gym ya Sempay Fitness Bonface Mutesa(kulia)akitoa maelezo kwa mwanachama ambaye anafanya 

SENPAI AELEZA UMUHIMU WA MICHEZO KWA MWILI WA BINADAMU.

Mazoezi yana umuhimu sana kwenye mwili wa binadamu,na inapendeza zaidi mtu anapoyafanya bila kusubiri kupewa maelekezo na daktari.

Wengi wanaopewa  maelekezo na daktari wanafanye mazoezi kwa sababu fulani za kiafya  unakuta wanafanya kama  adhabu na siyo kwa kupenda wenyewe.

Ni maneno ya mcheza kareta na mkufunzi wa karate Senpai  Samueli (48)ambaye kwa sasa  ni mmiliki wa  Gym(sehemu maalumu ya kufanyia mazoezi) inayoitwa Sempay Fitness iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Senpai hayuko mbali na tafiti mbalimbali ambazo zilikwishafanywa na wataalamu mbalimbali ambapo Dr. Jason na Nor Farah wa Chuo kikuu cha Glasgow  katika utafiti wake anasema kuwa mazoezi kwa ujumla wake yana umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu, hasa kama yakiambatana na lishe bora.

Mazoezi huweza kuzuia magonjwa sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo, kansa na shinikizo la damu, pia kwa kufanya mazoezi unaweza kuongeza kipato kwa kuwa unaweza kufanya kazi muda mrefu kuliko asiye fanya mazoezi.

Kwa jamii ambazo zimekuwa zikizingatia mazoezi zimekuwa familia bora na za mfano kuanzia kwenye maadili hadi kipato kwani kwa kufanya mazoezi familia zao zimeeza kujiepusha na magonjwa ambayo siyo ya lazima.

Kufanya mazoezi kila mara kuna faida nyingi ambazo haziwezi kuonekana kwa haraka, kama vile kuimarisha hali ya kiakili, ambayo matokeo yake ni kuwa na furaha,pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi.
Mazoezi  yanasaidia kuzalishwa kwa wingi kwa kemikali aina ya endorphins wakati wa kufanya mazoezi ambayo husaidia kwenye mapambano ya sonono (depression) na hivyo kumfanya mfanya mazoezi kuwa na furaha zaidi.

Kwenye jamii kumekuwa na upokeaji  tofauti juu ya  umuhimu wa mazoezi,huku wengi wakihusisha mazoezi kuwa ni kwa watu wenye pesa,wenye miili minene kitu ambacho Senpai anasema kuwa mazoezi ni kwa mtu yeyeyote yule ambaye anapenda kuimarisha mwili wake.
 “Ukifanya mazoezi unakuwa hauna muda wa kukaa kwenye makundi mabaya,na kuanza kujadili mambo ambayo hayana maana,mimi marafiki zangu wengine niliokuwa nao wamefariki na magonjwa mbalimbalimbali na  hii ni kutokana na kuwa kwenye makundi mabaya”Anasema Senpai

Wazo la kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi(GYM).
Senpai anasema kuwa alikuwa na wazo la kuanzisha gym kutokana na kupenda mazoezi lakini kuwepo kwa changamoto kubwa ya kutokuwepo kwa sehemu maalumu kwa ajili ya kufanyia mazoezi,na baadhi sehemu zilikuwepo kutokuwa na sifa kwa kutokuwa na waalimu pamoja na vifaa vya mazoezi.

Anasema kuwa yeye amefanya mazoezi ya kunyanyua vyuma na kucheza mchezo wa boksing  na hatimaye kuwa mwalimu wa karate tangu mwaka 1988 ambapo kwa sasa hivi ana mkanda mweusi.

“Mimi nilianza kwa kunyanyua tu vyuma mtaani lakini nikawa na wazo la kuanzisha gym yangu kwa ajili ya kuwafundisha watu mazoezi mbalimbali ila nilikuwa nikiwaza mbali zaidi kuwa nianzishe gym ya kisasa ambayo itakuwa na vigezo na mwalimu mwenye taaluma hiyo”Alisema.

Anasema wakati ananyanyua vyuma mtaani jamii nyingi hususani vijana waliamini kuwa kufungua gym au kufanya mazoezi ni kunyanyua vyuma pekee lakini yeye lengo lilikuwa ni kuweza kutoa huduma kwa rika zote kwa kuwa na mazoezi ya kila aina.

Kwa sasa anamiliki gym itwayo Sempay Fitness jina ambalo anasema kuwa linatokana na cheo alichonacho cha mwalimu au mkufunzi wa karante.

Gym ya Sempay fitness ipo uwanja wa saba saba Manispaa ya Moshi  ambayo inatoa mazoezi mbalimbali kwa rika zote ikiwemo vijana kwa wazee ambapo pia wapo wagonjwa wanaofika kwa kufanya mazoezi kama sehemu ya tiba.

Aina ya mazoezi yanayotolewa na Gym ya Sempay.
Uzuri wa gym mteja afike aweze kupata huduma aliyokuwa anahitaji kama alikuwa anataka kujenga mwili wake basi akute mashine hizo kama ni kupunguza mwili,au mazoezi ya kawaida basi aweze kupata mashine hizo.

Senpai anasem kuwa kwenye gym yake anatoa mazoezi mbalimbali kama  ya kujenga mwili(body bulding)Aerobics,Physical exercise,na mazoezi ya Cardio Machine ambayo yanaambatana na mazoezi yanayotumia mashine kama tradmill,upright Bicycle cross carble na four station machine ambazo mtu hufanya mazoezi kama anaendesha baiskeli na kukimbia.

Pia kuna mazoezi yanayoitwa Sauna,ni mazoezi ya kipekee kwani huwa na chumba chake maalumu na mitambo yake na unapoingia huko na kufungiwa basi mtu anatokwa na jasho bila kufanya mazoezi.

Aina hii ya mazoezi pia inapendwa na watu wengi kwani imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa kwa watu wanaofanya mazoezi hayo kutoka jasho ambalo huondoa uchafu mwilini.

Mazoezi mengine ni kama Stream bath ambayo pia kidogo ingefanana na sauna lakini yenyewe inatoa jasho lenye unyevunyevu pia bila kufanya mazoezi.

Mazoezi ya sauna na Stream bath yanapendwa na rika zote kutokana na mtu anapofanya mazoezi hayo anapojisikia vizuri kutokana na kusaidia kuondoa uchafu mwilini kwa njia ya vinyoleo.

Changamoto za kuanzisha Gym.
Senpai anasema kuwa changamoto kubwa baada ya kukamisha vifaa vyote vya mazoezi pamoja na nyumba yenye nafasi ya kutosha changamoto kubwa kwake ilikuwa ni mwalimu wa kufundisha mazoezi.

“Nilipoanza nilipata shida kwenye mwalimu,japo mimi mwenyewe ni mwalimu mzuri lakini nikawa ninakabiliwa na majukumu mengine hivyo ikanilazimu kuwa na mwalimu wa ha watu mazoezi”Anasema.

Anasema kuwa walimu wa mazoezi ambao wana taaluma hiyo wanapatikana kwa shida,ambapo mwalimu wa kwanza alimtoa Jijini Dar es Salaam,lakini hakuweza kukaa nae kwa muda mrefu baada ya kujiingiza kwenye makundi mbaya na kushindwa kufuata taratibu za kazi.

Changamoto nyingine ni pamoja na kutokuwepo kwa wataalamu wa kutengeza mashine ambazo zinatumika kwa ajili ya kufanyia mazoezi.
Lakini awali kabisa changamoto kubwa ilikuwa ni watu wengi kutohamasika kufanya mazoezi,tena kwa kulipa wanaona kuwa wanatumia garama kubwa,lakini kwa sasa wapo watu ambao wameelimika na kuhamasika kutumia pesa na muda wao kufanya mazoezi.
Senpai anasema kuwa biashara ya gym imekuwa ngumu kwani ni biashara ngeni ambayo wachache ndio wanauelewa juu yake pamoja na umuhimu wake.
Samuel kwenye gym yake kuna wateja wa rika tofauti lakini rika la watu wazima ndio wamehamasika zaidi ambao idadi yake ni kubwa ya wanaofika kufanya mazoezi kwenye gym hiyo.

Malengo ya baaday baada ya kuanzisha gym.
Senpai anasema kuwa malengo yake ya baadae baada ya kuanzisha gym ni kuanisha darasa la karate kwa watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 7-14 kwani kufundisha vijana wakubwa huwa na changamoto mbalimbali.

Anasema kuwa analazimika kuanza darasa la vijana wenye umri huo kwani anaweza kuanza nao tangu wakiwa darasa la kwanza hadi la saba,lakini kufundisha wenye umri zaidi ya hapo inakuwa vigumu kwani wakishajiunga na elimu ya sekondari hupangiwa sehemu za mbali.

Lakini anatoa wito kwa jamii kujijengea tabia ya kufanya mazoezi hata kwa wale wanaobanwa na majukumu ya kikazi kujitengea muda kidogo kwa ajili ya kufanya mazoezi ambayo pia husaidia kuongeza ufanini kazini kwa kuongeza uwezo wa akili kufanya kazi na kufikiri.