Mcheza kareta na mkufunzi wa karate
Senpai Samueli (48)ambaye kwa sasa ni mmiliki
wa Gym inayoitwa Sempay Fitness akifanya mazoezi kwenye gym yake
iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
|
Mwalimu wa
kufundisha mazoezi kwenye gym ya Sempay Fitness Bonface Mutesa(kulia)akitoa
maelezo kwa mwanachama ambaye anafanya
SENPAI AELEZA UMUHIMU WA MICHEZO KWA MWILI WA BINADAMU.
Mazoezi yana umuhimu sana kwenye
mwili wa binadamu,na inapendeza zaidi mtu anapoyafanya bila kusubiri kupewa
maelekezo na daktari.
Wengi wanaopewa
maelekezo na daktari wanafanye mazoezi kwa sababu fulani za kiafya
unakuta wanafanya kama adhabu na siyo kwa kupenda
wenyewe.
Ni maneno ya mcheza kareta na
mkufunzi wa karate Senpai Samueli (48)ambaye kwa sasa
ni mmiliki wa Gym(sehemu maalumu ya kufanyia mazoezi)
inayoitwa Sempay Fitness iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani
Kilimanjaro.
Senpai hayuko mbali na tafiti
mbalimbali ambazo zilikwishafanywa na wataalamu mbalimbali ambapo Dr. Jason na
Nor Farah wa Chuo kikuu cha Glasgow katika utafiti wake anasema
kuwa mazoezi kwa ujumla wake yana umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu, hasa kama
yakiambatana na lishe bora.
Mazoezi huweza kuzuia magonjwa
sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo, kansa na shinikizo la damu, pia kwa
kufanya mazoezi unaweza kuongeza kipato kwa kuwa unaweza kufanya kazi muda mrefu
kuliko asiye fanya mazoezi.
Kwa jamii ambazo zimekuwa
zikizingatia mazoezi zimekuwa familia bora na za mfano kuanzia kwenye maadili
hadi kipato kwani kwa kufanya mazoezi familia zao zimeeza kujiepusha na magonjwa
ambayo siyo ya lazima.
Kufanya mazoezi kila mara kuna
faida nyingi ambazo haziwezi kuonekana kwa haraka, kama vile kuimarisha hali ya
kiakili, ambayo matokeo yake ni kuwa na furaha,pamoja na kuongeza ufanisi wa
kazi.
Mazoezi yanasaidia
kuzalishwa kwa wingi kwa kemikali aina ya endorphins wakati wa kufanya
mazoezi ambayo husaidia kwenye mapambano ya sonono (depression) na hivyo
kumfanya mfanya mazoezi kuwa na furaha zaidi.
Kwenye jamii kumekuwa na
upokeaji tofauti juu ya umuhimu wa mazoezi,huku
wengi wakihusisha mazoezi kuwa ni kwa watu wenye pesa,wenye miili
minene kitu ambacho Senpai anasema kuwa mazoezi ni kwa mtu yeyeyote yule ambaye
anapenda kuimarisha mwili wake.
“Ukifanya mazoezi
unakuwa hauna muda wa kukaa kwenye makundi mabaya,na kuanza kujadili mambo
ambayo hayana maana,mimi marafiki zangu wengine niliokuwa nao wamefariki na
magonjwa mbalimbalimbali na hii ni kutokana na kuwa kwenye makundi
mabaya”Anasema Senpai
Wazo la kuanzisha sehemu ya kufanyia
mazoezi(GYM).
Senpai anasema kuwa alikuwa na wazo
la kuanzisha gym kutokana na kupenda mazoezi lakini kuwepo kwa changamoto kubwa
ya kutokuwepo kwa sehemu maalumu kwa ajili ya kufanyia mazoezi,na baadhi sehemu
zilikuwepo kutokuwa na sifa kwa kutokuwa na waalimu pamoja na vifaa vya mazoezi.
Anasema kuwa yeye amefanya mazoezi ya
kunyanyua vyuma na kucheza mchezo wa boksing na hatimaye kuwa
mwalimu wa karate tangu mwaka 1988 ambapo kwa sasa hivi ana mkanda
mweusi.
“Mimi nilianza kwa kunyanyua tu vyuma
mtaani lakini nikawa na wazo la kuanzisha gym yangu kwa ajili ya kuwafundisha
watu mazoezi mbalimbali ila nilikuwa nikiwaza mbali zaidi kuwa nianzishe gym ya
kisasa ambayo itakuwa na vigezo na mwalimu mwenye taaluma
hiyo”Alisema.
Anasema wakati ananyanyua vyuma
mtaani jamii nyingi hususani vijana waliamini kuwa kufungua gym au kufanya
mazoezi ni kunyanyua vyuma pekee lakini yeye lengo lilikuwa ni kuweza kutoa
huduma kwa rika zote kwa kuwa na mazoezi ya kila aina.
Kwa sasa anamiliki gym itwayo Sempay
Fitness jina ambalo anasema kuwa linatokana na cheo alichonacho cha mwalimu au
mkufunzi wa karante.
Gym ya Sempay fitness ipo uwanja wa
saba saba Manispaa ya Moshi ambayo inatoa mazoezi mbalimbali kwa
rika zote ikiwemo vijana kwa wazee ambapo pia wapo wagonjwa wanaofika kwa
kufanya mazoezi kama sehemu ya tiba.
Aina ya mazoezi yanayotolewa na Gym
ya Sempay.
Uzuri wa gym mteja afike aweze kupata
huduma aliyokuwa anahitaji kama alikuwa anataka kujenga mwili wake basi akute
mashine hizo kama ni kupunguza mwili,au mazoezi ya kawaida basi aweze kupata
mashine hizo.
Senpai anasem kuwa kwenye gym yake
anatoa mazoezi mbalimbali kama ya kujenga mwili(body
bulding)Aerobics,Physical exercise,na mazoezi ya Cardio Machine ambayo
yanaambatana na mazoezi yanayotumia mashine kama tradmill,upright Bicycle cross carble na four station machine
ambazo mtu hufanya mazoezi kama anaendesha baiskeli na kukimbia.
Pia kuna mazoezi yanayoitwa Sauna,ni
mazoezi ya kipekee kwani huwa na chumba chake maalumu na mitambo yake na
unapoingia huko na kufungiwa basi mtu anatokwa na jasho bila kufanya
mazoezi.
Aina hii ya mazoezi pia inapendwa na
watu wengi kwani imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa kwa watu wanaofanya mazoezi
hayo kutoka jasho ambalo huondoa uchafu mwilini.
Mazoezi mengine ni kama Stream bath
ambayo pia kidogo ingefanana na sauna lakini yenyewe inatoa jasho lenye
unyevunyevu pia bila kufanya mazoezi.
Mazoezi ya sauna na Stream bath
yanapendwa na rika zote kutokana na mtu anapofanya mazoezi hayo anapojisikia
vizuri kutokana na kusaidia kuondoa uchafu mwilini kwa njia ya
vinyoleo.
Changamoto za kuanzisha
Gym.
Senpai anasema kuwa changamoto kubwa
baada ya kukamisha vifaa vyote vya mazoezi pamoja na nyumba yenye nafasi ya
kutosha changamoto kubwa kwake ilikuwa ni mwalimu wa kufundisha
mazoezi.
“Nilipoanza nilipata shida kwenye
mwalimu,japo mimi mwenyewe ni mwalimu mzuri lakini nikawa ninakabiliwa na
majukumu mengine hivyo ikanilazimu kuwa na mwalimu wa ha watu
mazoezi”Anasema.
Anasema kuwa walimu wa mazoezi ambao
wana taaluma hiyo wanapatikana kwa shida,ambapo mwalimu wa kwanza alimtoa Jijini
Dar es Salaam,lakini hakuweza kukaa nae kwa muda mrefu baada ya kujiingiza
kwenye makundi mbaya na kushindwa kufuata taratibu za kazi.
Changamoto nyingine ni pamoja na
kutokuwepo kwa wataalamu wa kutengeza mashine ambazo zinatumika kwa ajili ya
kufanyia mazoezi.
Lakini awali kabisa changamoto kubwa
ilikuwa ni watu wengi kutohamasika kufanya mazoezi,tena kwa kulipa wanaona kuwa
wanatumia garama kubwa,lakini kwa sasa wapo watu ambao wameelimika na kuhamasika
kutumia pesa na muda wao kufanya mazoezi.
Senpai anasema kuwa biashara ya gym
imekuwa ngumu kwani ni biashara ngeni ambayo wachache ndio wanauelewa juu yake
pamoja na umuhimu wake.
Samuel kwenye gym yake kuna wateja wa
rika tofauti lakini rika la watu wazima ndio wamehamasika zaidi ambao idadi yake
ni kubwa ya wanaofika kufanya mazoezi kwenye gym hiyo.
Malengo ya baaday baada ya kuanzisha
gym.
Senpai anasema kuwa malengo yake ya
baadae baada ya kuanzisha gym ni kuanisha darasa la karate kwa watoto wadogo
wenye umri kati ya miaka 7-14 kwani kufundisha vijana wakubwa huwa na changamoto
mbalimbali.
Anasema kuwa analazimika kuanza
darasa la vijana wenye umri huo kwani anaweza kuanza nao tangu wakiwa darasa la
kwanza hadi la saba,lakini kufundisha wenye umri zaidi ya hapo inakuwa vigumu
kwani wakishajiunga na elimu ya sekondari hupangiwa sehemu za mbali.
Lakini anatoa wito kwa jamii
kujijengea tabia ya kufanya mazoezi hata kwa wale wanaobanwa na majukumu ya
kikazi kujitengea muda kidogo kwa ajili ya kufanya mazoezi ambayo pia husaidia
kuongeza ufanini kazini kwa kuongeza uwezo wa akili kufanya kazi na
kufikiri.
TAFADHALI, ninaomba e-mail ya Senpai Samwel
ReplyDeletechizzymorento20026@gmail.com
TAFADHALI, ninaomba e-mail ya Senpai Samwel
ReplyDeletechizzymorento20026@gmail.com