ZIKIWA ZIMEPITA SIKU CHACHE TANGU KUUAWA KWA PADRE MUSHI WATU WANAOSIOJULIKANA WASHAMBULIA NA KUCHOMA KANISA. NA PICHA ZAKE JINSI LILIVYOTEKETEA
Hapa ni mabaki ya vitu mbalimbali vilivyoungua kwa ndani.
Ikiwa
ni siku chache zimepita tangu kuuwawa kwa risasi kwa padre Evarist
Mushi huko Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na
baadae kulichoma moto kanisa la Walokole la Shaloom lililoko Kiyanga kwa
Sheha mkoa wa kusini Unguja Zanzibar.
Kamanda wa polisi mkoa
wa kusini Unguja Agustino Ulomi amesema hilo tukio limetokea jana saa
tisa na nusu usiku, ambapo huo moto ulianza kuwaka baada ya vijana
watatu walioonekana karibu na kanisa, baadae kidogo ndio mlinzi akaanza
kusikia mawe yakirushwa juu ya bati.
Baada ya mlinzi kuona hatari ilibidi akajifiche lakini kwa mbali akawa
anaona kinachoendelea, moto ukiendelea ndio akampigia simu kiongozi wa
kanisa ambae aliwapigia polisi, wakaja wakawa wanashirikiana na wananchi
kuuzima japo tayari ulikua umeshaunguza samani mbalimbali za kanisa
hilo, kilichosaidia kanisa hilo kutoungua lote ni vifaa imara
vilivyotumika kulijenga.
Katika ripoti hii ambayo imeripotiwa
na mwandishi wa habari Cathbert Kajuna wa kajunason.blogspot.com bado
hajakamatwa mtu yeyote mpaka sasa, polisi wamesema pia wanaanza
utaratibu wa ulinzi wa makanisa kutokana na vitisho vilivyopo sasa hivi.
Hakuna mtu yeyote aliejeruhiwa katika tukio hilo lililotokea saa tisa usiku wa kuamikia leo,
No comments:
Post a Comment