Saturday, April 28, 2012

MAFUNZO YA SIKU NNE YA  UCHAMBUZI WA SERA NA BAJETI YALIYOKUWA YANAFANYIKA KWA WAANDISHI MKOANI KILIMANJARO YAMALIZIKA LEO.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Adam Ndokeji akifafanua  jambo na waandishi wa vyombo mbalimbali waliohudhiria mafunzo hayo
washiriki kwenye mafunzo hayo wakimsikiliza mwezeshaji kwa makini


Mmiliki wa Mtandao huu wa www.tanzania-leo.blogsport.com odrick Mushi akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo




Friday, April 27, 2012

KAMATI KUU YA CCM YAKUBALIANA KUUNDWA UPYA KWA BARAZA LA MAWAZIRA ..
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi.


 Kamati Kuu iliyokutana leo tarehe 27/04/2012  chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine imefanya maamuzi kadhaa ikiwemo kumridhia Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri.

Ifuatayo ni taarifa Kamili kama ilivyosomwa kwa Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye.


Rais amepokea taarifa na maazimio ya Kamati ya wabunge wa CCM na Kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM juu ya kilichotokea kwenye bunge lililopita mjini Dodoma.


Taarifa hizo zimewasilishwa kwenye kamati kuu na kujadiliwa. Pamoja na taarifa hizo kamati Kuu imepokea taarifa ya jinsi Rais alivyojipanga kuchukua hatua za kuwawajibisha mawaziri na watendaji wa serikali na wale wa mashirika ya umma waliobainika kuhusika na ubadhirifu ulioinishwa na  taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, Kamati za kudumu za bunge na wabunge bungeni.


Kamati Kuu imeamua yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatambua na kuheshimu haki na wajibu wa wabunge kujadili utendaji wa serikali yao.Inapongeza juhudi za serikali kuhakikisha kuwa ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali inajadiliwa kwa uwazi na hivyo kuibua mapungufu yaliyojadiliwa.


2.Kamati Kuu imeridhika na imebariki uamuzi wa Rais   KULISUKA UPYA BARAZA LA MAWAZIRI na taasisi zingine zilizoanishwa katika ripoti hizo. Imesisitiza utekelezaji wa uamuzi huo ufanywe mapema iwezekanavyo.


Aidha kamati Kuu imeipongeza Kamati Teule ya baraza la wawakilishi Zanzibar iliyoundwa kuchunguza utendaji katika sekta mbalimbali kwenye serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa taarifa yao.


Kamati Kuu inawapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa jinsi walivyojadili taarifa hiyo na pia Kamati Kuu inaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuipokea taarifa na kuanza kuifanyia kazi.


A. UTEUZI
Kamati Kuu imeteua wafuatao kuwa makaimu Katibu wa mikoa. Vituo vyao vya kazi vitapangwa baadae. Uteuzi huu unatokana na kuwepo kwa mikoa wazi mitano, mikoa hiyo ni;


Geita,Njombe,Simiyu,Katavi,Magharibi.


Hivyo wafuatao wameteuliwa kuwa makaimu Katibu wa CCM wa Mikoa.


1. Ndg. Hilda Kapaya


2. Ndg. Shaibu Akwilombe


3. Ndg. Hosea Mpangile


4. Ndg. Alphonce Kinamhala


5. Ndg. Aziz Ramadhani Mapuri


Imetolewa na
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi.

mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm,Arusha ajiunga na chadema 

 mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm, Taifa Ally Bananga akitangaza kujiunga na chadema jana anasema amechoka kufanywa karai la zege na fagio ambalo kazi ikimalizika dhamani yake huisha

Hapa akikumbatiana na Godbless Lema.

Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM mkoani Arusha Ally Bbananga akitangaza kukihama chama hicho na kujinga na Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) leo kwenye hoteli ya kitalii ya Kibo palace , Kushoto aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini, Godbless lema Kulia Katibu wa Chadema mkoa wa Kinondoni, Hendry Kilewo

Habari,picha na Grace Macha Blog



 

 

 

 


   Tundu Lissu ashinda kesi ya kupinga ubunge wake

Tundu Lisu.

Tumeshafika mahakamani, wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa, wananchi wa Singida, na waandishi wa habari wapo wengi sana katika eneo la mahakama.

Polisi ni wengi sana, ndani na nje ya mahakama. Kilicho cha ajabu kidogo leo getini maofisa wote wakubwa wa jeshi la polisi wapo pale na kikosi maalumu kwa ajili ya kumkagua kila anayeingia mahakamani, tunapekuliwa hasa, hadi wabunge wanaoingia.

Kuna baadhi walikatazwa kuingiza magari yao mahakamani lakini baada ya vuta nikuvute, magari yapo mahakamani, na watu wamtinga ndani tunasubiri yatakayojiri.......... tutawajuza, leo kamanda nipo gado, Mungu amenijalia afya
.



Kesi ya chaguzi uliofanyika tarehe 31/10/2010, walalamikaji ni Shabani selema, na Paskali Halu. Walileta mashahidi 24, na vielelezo saba, wanawakilishwa na Wasonga. Kupinga uteuzi wa Lissu kuwa mbunge wa Jimbo la Singida mashariki, kwa madai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.

 Wakidai kuwa kulikuwa na dosari zilizofanya uchaguzi usiwe huru na haki, hivyo kumfanya Mgombea wao wa CCM asishinde.

Walalamikiwa, mlalamikiwa wa kwanza walisema kuwa yeye hakuwemo, au hakuwa mshirika wa tuhuma zilizofanywa. Walalamikiwa wote pamoja wanasema hakuna kitu cha msingi kinachoweza kuifanya mahakama itengue matokeo.

Haijabishaniwi kuwa mgombea alishinda kupitia CHADEMA, kupitia jimbo la singida mashariki, na kumshinda mgombea wa CCM Bw. Njau ambaye alipata nafasi ya pili. Tofauti ya Kura kati ya Lissu na Njau ilikuwa kura 1626.

Mlalamikiwa wa pili, anaunganishwa katika kesi kama necessary paty, kwa kuwa mlalamikiwa wa pili ni Msimamizi wa uchaguzi.

Hoja katika kesi zilikuwa 11.ambapo Mgombea wa walalamikaji (CCM) alikataa kusaini matokeo.


Wednesday, April 25, 2012


Real pay the penalty

Germans progress after 3-1 shoot-out win as Ronaldo misses





 


Bayern Munich will face Chelsea in the UEFA Champions League final on their own turf after beating Real Madrid on penalties at the Bernabeu.

The German side confirmed their place in the Munich final after the semi-final second leg itself finished 2-1 to home side Real, making it 3-3 on aggregate.

And when the game went to spot-kicks, Bayern were nerveless under pressure.
Bastian Schweinsteiger sealed a 3-1 shoot-out win after three Real players missed from the spot - including Cristiano Ronaldo.
It looked as though it might be a straightforward night for Real when they were two goals up courtesy of a Ronaldo brace inside the first quarter-of-an-hour.
David Alaba's handball from Angel Di Maria's shot allowed Ronaldo to score from the spot before Mesut Ozil slotted the Portuguese star in for his second after 14 minutes.

But Bayern always looked a threat at the other end, with Arjen Robben side-footing over from point-blank range early on.
And the Dutchman soon made amends, pulling one back from the spot after Pepe had grabbed Mario Gomez as he tried to head home Toni Kroos' cross.


But Bayern looked strong throughout and when it came to penalties, Manuel Neuer proved the hero, saving from Ronaldo and Kaka to help the visitors into a 2-0 lead.
Kroos and Philipp Lahm then had efforts saved by Iker Casillas but just when Real looked to be back in it, Sergio Ramos horribly skied his effort and it was left to Schweinsteiger to finish matters.

Real had erased their 2-1 deficit from the first leg within five minutes as Alaba was somewhat harshly punished for handling Di Maria's shot and Ronaldo slotted home the resulting penalty.

The visitors responded positively, though, and should have been level within minutes as Alaba nearly made amends for conceding the penalty with a brilliant run and cross but somehow former Chelsea star Robben scuffed the ball over the bar from only yards out.

Franck Ribery was then denied by a brilliant saving challenge from Sami Khedira after Casillas had spilled a Gomez shot from 20 yards but only 15 minutes had passed when Ronaldo doubled his tally and Madrid's advantage on the evening as he raced on to a brilliant through-ball from Ozil and stroked the ball past Neuer from the edge of the area.

The tie was back on a knife-edge 12 minutes later, though, as Pepe was penalised for a push on Gomez as he tried to get on the end of Kroos' cross.

Robben had missed a significant penalty in the Bundesliga title decider against Borussia Dortmund a fortnight ago but the former Real player stepped up again and his spot-kick just sneaked past Casillas who got a hand to the ball.
source skysport.


TGNP YAITAKA SERIKALI KUWAWAJIBISHA MAWAZIRI WANAODAIWA KUFUJA FEDHA ZA UMMA.
 

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) imeitaka Serikali kuwawajibisha mara moja mawaziri, manaibu waziri na watendaji wakuu wa Serikali na mashirika ya umma ambao wametajwa kuhusika na matumizi mabaya ya fedha za umma ama kushindwa kusimamia rasilimali za taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Anna Kikwa katika taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari. Aidha amemtaka mkuu wa nchi awafute kazi watendaji wanaotumia vibaya fedha za umma na kuwaongezea wananchi umasikini, ili iwe fundisho kwa watendaji wa Serikali wenye tabia kama hiyo na wachukuliwe hatua za kisheria.

Hata hivyo TGNP imeishauri Serikali kuboresha mifumo ya kusimamia rasilimali za nchi yetu ili wananchi wote waweze kufaidi keki ya taifa kwa sababu mara zote Serikali imekuwa ikisema Tanzania hatuna rasilimali lakini hali halisi ni kwamba rasilimali za taifa zinaliwa na mafisadi wachache wa ndani na nje ya nchi.
Katika hatua nyingine, mtandao huo umetoa pongezi kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu, Ardhi Maliasili na Utalii kwa kusimamia vema na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali zinazotokana na walipa kodi na kuwasilisha ripoti zao Bungeni ambazo zimeibua uozo mkubwa na kujenga mjadala mpana unaotaka uwajibikaji kwa wanaohusika.
“Tunawapongeza pia baadhi ya wabunge  walioshiriki katika mijadala  kwa kuzijadili ripoti hizo kwa undani bila kujali urafiki, itikadi za kisiasa, hasa ile ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa  kuibua  uozo uliojificha na kusimamia maslahi ya Taifa.” amesema Bi. Kikwa katika taarifa hiyo.
“Tumeshuhudia mara kadhaa kupitia vyombo vya habari  wabunge wakiacha itikadi zao za kisiasa na kusimamia kwa dhati dhana ya kushinikiza uwajibikaji katika vyombo vinavyohusika kutokana na ufisadi kama Richmond, Dowans nk. Hata hivyo, TGNP kwa muda mrefu tumekuwa tukipinga ubadhirifu wa fedha za umma  na kudai haki ili kutokomeza ufisadi uliokithiri, lakini bado ufisadi umezidi kushamiri hasa katika Wizara na taasisi za umma.
“Sisi kama wanaharakati tunasema kuendelea kwa ufisadi ni aibu kwa serikali iliyoko madarakani, TGNP tuko mstari wa mbele  kushinikiza rasilimali za taifa ziwanufaishe wananchi wote, hasa walioko pembezoni, kamwe hatutanyamazia aina yoyote ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya wananchi zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.” Imesema taarifa hiyo.
"Tumeshuhudia wanawake na wasichana wakiendelea kuwa maskini na kukumbana na mifumo kandamizi kwa kukosa haki za kufikia huduma za msingi kama vile maji, barabara, afya, elimu, kilimo, utawala bora n.k. Fedha zinazopotea zinatokana na kodi za wananchi na jamii ina haki ya kuhoji uwajibikaji na wahusika wanatakiwa kuchukuliwa  hatua za kisheria," imeongeza taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.
Vilevile tunawapongeza wabunge wote walioshiriki kwa dhati katika zoezi la kusaini kusudio la kutaka viongozi waliotajwa/kutuhumiwa  kwenye ripoti hizo kuwajibika. Ili kuonesha dhana ya uwajibikaji na utawala bora unaozingatia misingi ya haki za binadamu.

Na mwandishi wetu.

MAFUNZO YA UFUATILIAJI WA SERA NA BAJETI YAFANYIKA KWA WANDISHI WA HABARI MKOANI KILIMANJARO

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa makini kimsikiliza mwezeshaji wa mafunzo hayo ya ufuatiliaji wa sera na Bajeti yaliyofanyika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kwenye hotel ya KNCU.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Adam Ndokeji akijadiliana jambo na waandishi wa vyombo mbalimbali waliohudhiria mafunzo hayo

Waandishi waliohudhuria mafunzo hayo

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Adam Ndokeji akijadiliana jambo na waandishi wa vyombo mbalimbali waliohudhiria mafunzo hayo

Waandishi wakiwa makini kuendelea kusikiliza mafunzo ya ufuatiliaji wa sera na Bajeti
 Mmilikiwa mtandao huu wa www.tanzania-leo.blogsport.com wa kwanza kushoto akiwa na mwandishi nguli wa michezo Henry Lyimo wa Moshi fm kwenye mafunzo ya hayo ya ufuatiliaji wa Sera na Bajeti.

 


Tuesday, April 24, 2012

SINDANO YA GANZI YAMSABABISHIA MAUTI MTOTO BAADA YA KUCHOMWA KATIKA ZAHANATI BINAFSI, MZAZI AILIPIA SHILINGI 20,000.    


Tukio hilo la kusikitisha limetokea Aprili 22 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi baada ya mtoto huyo kufikishwa katika Zahanati binafsi, akiwa na jipu katika makalio ndipo Daktari alipompokea na kumtoza shilingi 20,000 baba mzazi wa marehemu Rataniel Mtajiha (45), ili apewe huduma. 

Sababu ya kuchomwa sindano ya ganzi ni kutokana na mtoto huyo kuonaonekana ni mwoga hivyo achomwe sindano hiyo, na baada ya kuchomwa mtoto huyo alifariki papo hapo.Wakati huo huo baba mzazi  Mtajiha, amesema hakutegemea mwanae kufikwa na mauti kwani, muda wote alikuwa anacheza licha  ya kuwa na jipu hilo.

KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA MBEYA ADVOCATE NYOMBI

Sindano ya ganzi yamsababishia mauti mtoto Tumaini Rataniel Mtajiha (5), mkazi wa Kijiji cha Hagomba Kata ya Itaka baada ya kuchomwa na daktari wa zahanati binafsi ya Sisika, inayomilikiwa na mwalimu mmoja katika Mtaa wa Ichenjezya, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.

Baada ya tukio hilo Mtajiha alitoa taarifa Kituo cha Polisi Vwawa, ambapo walifika na kumchukua Daktari huyo (Jina linahifadhiwa), mwili wa mtoto na jalada lake pamoja na  sampuli ya dawa alizotumia hadi kwenye Hospitali ya Wilaya ili kufanyiwa uchunguzi majira ya saa 10:00 jioni.

  Aidha, baada ya kutafakari kwa kina Hospitali hiyo ya wilaya, walitoa taarifa mkoani na kuagiza mwili ufanyiwe uchunguzi Aprili 23 mwaka huu, baada ya jopo la mkoani kuwasili wilayani Mbozi ili kufanya uchunguzi wa kina.

 

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya hakuweza kupatikana kuthibitisha tukio hili, na hivi sasa Daktari wa Zahanati hiyo anashikiliwa na Kituo cha polisi Vwawa akisubiri uchunguzi kufanyika.

AU sasa yaonya Sudan na Sudan kusini

 
Muungano wa Afrika umezitaka Sudan na Sudan Kusini kutekeleza mkataba wa amani kwa muundo mpya wa AU.
Kamishna wa baraza la usalama wa AU, Ramtane Lamamra amesema muungano huo utachukua hatua zinazostahili iwapo mojawapo ya nchi hizo itashindwa kutekeleza mpango wa amani uliopendekezwa katika muda uliopangwa.

Baada ya kuwa kimya kwa muda, hatimae sauti ya Afrika inasikika kufuatia mzozo huo kati ya Sudan na Sudan kusini ambao sasa unatishia kuwa chanzo cha vita kati ya majirani hao.
Wajumbe wa baraza la usalama la umoja huo walimaliza kikao chao cha dharura kuhusu utata huo kwa kutoa maagizo mazito na kukariri njia ya kufuatwa ili kudhibiti hali mara moja.
Baada ya kupokea ripoti za wawakilishi wa serikali husika na hata mjumbe wa kamati maalum ya kuhusu utekelezaji wa mikataba ya amani kati ya nchi hizo, Umoja wa afrika umetaka pande zote mbili ziondoe majeshi yao katika mipaka hiyo inayo zozaniwa na wasitishe mashambulio mara moja.

Umoja huo pia umependekeza kuwa ujumbe maalum wa waangalizi wa mipaka pamoja na kikosi cha walinda amani cha umoja wa mataifa kitumwe katika maeneo hayo katika kipindi cha wiki moja ijayo.
Viongozi wa Sudan na Sudan kusini wametakiwa kuacha kutoa matamshi yanayochochea uhasama kati yao na kusambaza propaganda ambazo zinachochoea mzozo huo.
Baraza hilo la usalama ya Umoja wa Afrika pia limeamua kuunda kamati itakayo chunguza malalamishi kutoka pande zote mbili hizi na kubaini ukweli kamili kuhusu masuala wanayosema kuwa yanazua utata huo.
Pamoja na hilo serikali zote mbili zimeonywa dhidi ya kuwasiadia waasi walioko kwenye maeneo yanayozozaniwa.
Hili ndilo agizo kali zaidi kutolewa na umoja huo tangu mzozo huo uanze na umepata kuungwa mkono na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo pia lilikuwa na kikao chao jana.
Mwenyekiti wa baraza hilo balozi Susan Price kutoka Marekani, amesema kuwa hii ni hatua muhimu ya uongozi kutoka Afrika na kuwa baraza hilo halitasita kuchukulia serikali hizo hatua ikiwa zitapuuza maagizo hayo.

Kaluli hii imetolewa saa chache tuu baada ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, ambaye yuko ziarani nchini China kusema mashambulizi yaliotekelezwa na ndege ya kijeshi za sudan katika mipaka yao ni sawa na nchi hiyo kutangaza vita dhidi yao.

Kumekuwa na harakati chungu nzima za kidiplomasia kujaribu kuzuia vita kuzuka upya kati ya nchi hizi, na msukumo wa hivi karibuni umetoka kwa Rais Hu jing Tao wa China, ambaye amewataka viongozi hao wasitishe ugomvi huo.

Kauli ya Rais Hu Jing Tao ni muhimu sana kwa kuwa serikali yake inaushawishi mkubwa sana katika pande zote kwenye mzozo huo.
VISEMAVYO VICHWA VYA MAGAZETI KWA SIKU YA LEO..





Monday, April 23, 2012

CWT YALIA NA MADAI YA WAALIMU KILIMANJARO 
Katibu wa Chama cha waalimu Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro Nadhanael Mwandete akizungunza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na amadai ya waalimu.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari,wa kwanza kushoto,Charles Lyimo Nipashe,aanayefuata Rehema matowo wa Mwananchi,Enos Masanja wa Star tv,Samwel Shayo wa Radio Sauti ya Injili ,aliyevaa t shirt ya njano ni Zephania Reanatus na Mpiga picha wa Itv aliyesimama Roberth Minja.

Kuanzia kushoto,Charles Lyimo nipashe,Enos Masanja Star tv,Reehema matowo Mwananchi,Samweli Shayo,zephania Renatus na Mpiga picha wa itv Robrth Minja wakimsikiliza Katibu wa CWT hayupo pichani.



Waalimu wa Mkoani Kilimnjaro wamelelamikia kutolipwa malimbikizo ya madai yao ya mishahara na yasiyo ya mishahara zaidi ya shilingi billion 2.6 huku Wilaya ya Same ikiongoza kwa Wilaya ambazo waalimu hawajalipwa kabisa madai yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Chama cha waalimu Tanzania(CWT)Mkoa wa Kilimanajro Nadhanael Mwandete alisema kuwa madai hayo yalikwisha lipwa kwa mara ya kwanza lakini hayakuwa na tija huku baadhi ya Wilaya Kama Same zikisahaulika kulipwa.

Alisema kuwa maadai hayo kwa walimu Wilayani Same ni zaidi ya shilingi milioni 978 ambayo yanahusisha madai ya mishahara na yasiyo ya mishara,kwa walmu 107 huku Wilaya ya Moshi Vijijini ikidai zaidi ya million528.

Madai wanayodai walimu ni pamoja na makato ya mishahara,waalimu kupanda madaraja na kuendelea kulipwa mishahara ya zamani,likizo,matibabu pamoja na wanapoamishwa  sehemu zao za kazi,madai ambayo hadi February mwaka huu yangepaswa yawe yamelipwa.
               
Mwandete alisema kuwa Serikali ilikwisha hakikisha madai hayo ya walimu kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Kilimanjaaro kwa kushirikiana na Makatibu wa CWT lakini cha kushangaza wapo walimu ambao madai  yao hadi sasa hayajalipwa.

“Serikali ililipa madai ya walimu yanayohusiana na mishahara tena kidogo lakini yale ambayo hayahusiani na mishahara yakiwa bado ambapo hata billion 2 haikufika,na mimi nikiwa kama Katibu wa chama cha waalimu nimekuwa nikipokea malalamiko kila kukicha wakilalamikia hali ngumu”Alisema Mwandete.

Alisema kuwa sababu ambayo Serikali imekuwa ikijitetea kutokana na kutolipa madai hayo ni baada ya kuruka ukurasa wa Wilaya ya Same,lakini pia wapo ambao wamekuwa wakikatwa mishahara tangu miezi ya oktoba hadi February wamekuwa wakipunjwa mishahara yao.

Alisema waalimu ambao wamekatwa mishahara kwa kupunjwa wanafika 19 ambao wanatoka wilaya ya Moshi Manispaa na Hai ambapo tangu mwezi oktoba hado February hawajalipwa mishahara yao yote,kama wanaolipwa laki 7 kujikuta wanalipwa laki 3.

Alisema kuwa tatizo la madai ya waalimu ya mishahara na yasiyo ya mishahara yapo kila Wilaya lakini Wilaya ya Same ndo limekuwa tatizo kubwa zaidi.

Alisema kuwa hali hiyo itawafanya waalimu waichukie serikali yao kutokana na kutoijali licha ya huduma ambayo imekuwa ikiyoa kwa Serikali.

Hata hivyo alisema  Mkoa wa Kilimanjaro umekuwa ukisifiwa sana kwenye suala la maendeleo ya elimu hivyo sababu kama za madai ya malimbikizo ya walimu n zinaweza kuchangia kushuka kwa kiwangp cha elimu kwa sababu madai waalimu wanayodai ni ya msingi.

KATIKA PITAPITA KAMERA YETU IKAKUTANA NA MAPAPARAZI WALIOPO FIELD RADIO BOMA,WAPO PIA WANAOTOKA ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE.
Hapa wakiwa kwenye mapumziko baada ya kutembea sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuska  News

Hapa wanabadilishana mawazo zaidi


WAANDAMANA NUSU UCHI KULALAMIKIA POLISI

Wanawake wa uganda
Kundi la wanawake wamevua nguo, nusu uchi kulalamikia kitendo cha polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kingono mwanasiasa wa upinzani.

 Kanda ya video imeonyesha polisi akimtomasatomasa matiti Bi Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) baadaya kumkamata kuzuia maandamano ya wiki jana.

Naibu kamishina wa polisi Andrew Kaweesa ameomba radhi na kuahidi kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo. Tangu uchaguzi mkuu mwaka 2011 ambapo rais Yoweri Museveni alishinda Uganda imeshuhudia maandamano ya upinzani ambapo wafuasi wengi wameishia celi za polisi.

Tukio la wiki jana lilipelekea kuwepo ghadhabu ya umma ambapo pia lalama zilitanda kupinga kukamatwa kwa Bi Turinawe ambaye ni kiongozi wa tawi la wanawale katika chama cha FDC kinachoongozwa na Kizza Besigye.

Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango amesema wanawake hao waliandamana hadi kituo cha polisi wakiwa vifua wazi na kupeperusha mabango yaliokuwa na maandishi,''utahisi vipi ikiwa sehemu zako nyeti zitafinywa''.Wanawake sita walikamatwa baada ya kukataa kufunika vifua vyao, lakini wakaachiwa huru bila masharti yeyote.

                                       source bbc

 


MKWAWA IRINGA WANANCHUO,WANANCHI,WAFUNGA BARABARA NA KUCHIMBA BARABARA. 

Wanafunzi chuo cha Mkwawa wakiwa wameziba barabara Iringa - Pawaga kwa mawe

Hapa askari zaidi wakiruka katika gari hilo ili kunusuru maisha ya dereva na msajili baada ya kuvamiwa na wanafunzi hao wakati akitoka maeneo ya Pawaga

Wananchuo wa Mkwawa na wananchi wakishangilia na kuzomea.

Wanachuo Mkwawa Iringa wakiwa wamechimba barabara kushinikiza matuta 


Vurugu za kutaka wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADs) kuweka matuta katika lango la chuo cha elimu Mkwawa Iringa bado zinaendelea huku diwani wa kata hiyo ya Mkwawa Thoabias Kikula na askari wa FFU waliokuwa katika gari la msajili wa Mahakama kanda ya Iringa wakifanyiwa vurugu kwa kutaka kuchezea kichapo wao na dereva .

Diwani Kikula ambaye kwa sasa ameokolewa kutoka eneo hilo la vijana wa CCM ili kunusuru kuchezea kichapo ameunga na askari polisi walikuwepo eneo hilo kwenda kwa mkuu wa chuo hicho ili kuangalia uwezekano wa kwenda TANROADs .

Wanafunzi wa chuo cha elimu Mkwawa Iringa hivi sasa wameziba barabara kuu ya Iringa -Pawaga barabara inayosimamiwa na wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADs) wakishinikiza kuwekwa matuta katika eneo la lango kuu la chuo hicho cha Mkwawa kutokana na ajali za mara kwa mara .

Wanafunzi hao zaidi ya 200 wameziba barabara hiyo eneo la Kuingia chuoni huku wakimtaka diwani wa kata hiyo ya Mkwawa Thobias Kikula .a.k.a MC Kikulacho kushirikiana nao kuibomoa barabara hiyo ili kuweka matuta kuanzia sasa.

Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mbele ya diwani huyo wanafunzi hao wamesema kuwa wamelazimika kuziba barabara hiyo baada ya kuwepo kwa matukio ya mara kwa mara kwa wanafunzi wanaovuka barabara hiyo kugongwa kutokana na madereva kuendesha magari yao kwa mwendo mkali zaidi.

Hivyo kutokana na ajali hizo wamemtaka diwani huyo kuungana nao katika kuchimba barabara hiyo ya lami ili kuweka matuta kuanzia sasa zoezi ambalo limekuwa gumu kwa diwani Kikulacho kuungana kulitekeleza .

Akijaribu kuwatuliza jazba wanafunzi hao bila mafanikio diwani Kikulacho alisema kuwa anaomba kupewa muda ili suala hilo aweze kulifikisha kwa wahusika kwa maana ofisi ya Tanroads mkoa na baraza la madiwani.

Hadi sasa hali ni tete na diwani bado amezungukwa na wanafunzi hao ambao wanaimba nyimbo za kama si juhudi zetu wenyewe diwani ungefikaje leo hapo huku polisi wakionyesha kuvuta subira kuwatawanya

 habari, picha na francis Godwin-blog.