Monday, April 23, 2012

MKWAWA IRINGA WANANCHUO,WANANCHI,WAFUNGA BARABARA NA KUCHIMBA BARABARA. 

Wanafunzi chuo cha Mkwawa wakiwa wameziba barabara Iringa - Pawaga kwa mawe

Hapa askari zaidi wakiruka katika gari hilo ili kunusuru maisha ya dereva na msajili baada ya kuvamiwa na wanafunzi hao wakati akitoka maeneo ya Pawaga

Wananchuo wa Mkwawa na wananchi wakishangilia na kuzomea.

Wanachuo Mkwawa Iringa wakiwa wamechimba barabara kushinikiza matuta 


Vurugu za kutaka wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADs) kuweka matuta katika lango la chuo cha elimu Mkwawa Iringa bado zinaendelea huku diwani wa kata hiyo ya Mkwawa Thoabias Kikula na askari wa FFU waliokuwa katika gari la msajili wa Mahakama kanda ya Iringa wakifanyiwa vurugu kwa kutaka kuchezea kichapo wao na dereva .

Diwani Kikula ambaye kwa sasa ameokolewa kutoka eneo hilo la vijana wa CCM ili kunusuru kuchezea kichapo ameunga na askari polisi walikuwepo eneo hilo kwenda kwa mkuu wa chuo hicho ili kuangalia uwezekano wa kwenda TANROADs .

Wanafunzi wa chuo cha elimu Mkwawa Iringa hivi sasa wameziba barabara kuu ya Iringa -Pawaga barabara inayosimamiwa na wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADs) wakishinikiza kuwekwa matuta katika eneo la lango kuu la chuo hicho cha Mkwawa kutokana na ajali za mara kwa mara .

Wanafunzi hao zaidi ya 200 wameziba barabara hiyo eneo la Kuingia chuoni huku wakimtaka diwani wa kata hiyo ya Mkwawa Thobias Kikula .a.k.a MC Kikulacho kushirikiana nao kuibomoa barabara hiyo ili kuweka matuta kuanzia sasa.

Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com mbele ya diwani huyo wanafunzi hao wamesema kuwa wamelazimika kuziba barabara hiyo baada ya kuwepo kwa matukio ya mara kwa mara kwa wanafunzi wanaovuka barabara hiyo kugongwa kutokana na madereva kuendesha magari yao kwa mwendo mkali zaidi.

Hivyo kutokana na ajali hizo wamemtaka diwani huyo kuungana nao katika kuchimba barabara hiyo ya lami ili kuweka matuta kuanzia sasa zoezi ambalo limekuwa gumu kwa diwani Kikulacho kuungana kulitekeleza .

Akijaribu kuwatuliza jazba wanafunzi hao bila mafanikio diwani Kikulacho alisema kuwa anaomba kupewa muda ili suala hilo aweze kulifikisha kwa wahusika kwa maana ofisi ya Tanroads mkoa na baraza la madiwani.

Hadi sasa hali ni tete na diwani bado amezungukwa na wanafunzi hao ambao wanaimba nyimbo za kama si juhudi zetu wenyewe diwani ungefikaje leo hapo huku polisi wakionyesha kuvuta subira kuwatawanya

 habari, picha na francis Godwin-blog.


No comments:

Post a Comment