CWT YALIA NA MADAI YA WAALIMU KILIMANJARO
Katibu wa Chama cha waalimu Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro Nadhanael Mwandete akizungunza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na amadai ya waalimu. |
Kuanzia kushoto,Charles Lyimo nipashe,Enos Masanja Star tv,Reehema matowo Mwananchi,Samweli Shayo,zephania Renatus na Mpiga picha wa itv Robrth Minja wakimsikiliza Katibu wa CWT hayupo pichani.
Waalimu wa Mkoani Kilimnjaro wamelelamikia kutolipwa malimbikizo ya madai yao ya
mishahara na yasiyo ya mishahara zaidi ya shilingi billion 2.6 huku Wilaya ya
Same ikiongoza kwa Wilaya ambazo waalimu hawajalipwa kabisa madai yao.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Chama cha
waalimu Tanzania(CWT)Mkoa
wa Kilimanajro Nadhanael Mwandete alisema kuwa madai hayo yalikwisha lipwa kwa
mara ya kwanza lakini hayakuwa na tija huku baadhi ya Wilaya Kama Same
zikisahaulika kulipwa.
Alisema kuwa maadai hayo kwa walimu Wilayani Same ni
zaidi ya shilingi milioni 978 ambayo yanahusisha madai ya mishahara na yasiyo
ya mishara,kwa walmu 107 huku Wilaya ya Moshi Vijijini ikidai zaidi ya million528.
Madai wanayodai walimu ni pamoja na makato ya
mishahara,waalimu kupanda madaraja na kuendelea kulipwa mishahara ya zamani,likizo,matibabu
pamoja na wanapoamishwa sehemu zao za
kazi,madai ambayo hadi February mwaka huu yangepaswa yawe yamelipwa.
Mwandete alisema kuwa Serikali
ilikwisha hakikisha madai hayo ya walimu kwenye Wilaya zote za Mkoa wa
Kilimanjaaro kwa kushirikiana na Makatibu wa CWT lakini cha kushangaza wapo
walimu ambao madai yao hadi sasa hayajalipwa.
“Serikali ililipa madai ya walimu yanayohusiana na
mishahara tena kidogo lakini yale ambayo hayahusiani na mishahara yakiwa bado ambapo
hata billion 2 haikufika,na mimi nikiwa kama
Katibu wa chama cha waalimu nimekuwa nikipokea malalamiko kila kukicha
wakilalamikia hali ngumu”Alisema Mwandete.
Alisema kuwa sababu ambayo Serikali imekuwa ikijitetea
kutokana na kutolipa madai hayo ni baada ya kuruka ukurasa wa Wilaya ya Same,lakini
pia wapo ambao wamekuwa wakikatwa mishahara tangu miezi ya oktoba hadi February
wamekuwa wakipunjwa mishahara yao.
Alisema waalimu ambao wamekatwa mishahara kwa kupunjwa
wanafika 19 ambao wanatoka wilaya ya Moshi Manispaa na Hai ambapo tangu mwezi
oktoba hado February hawajalipwa mishahara yao
yote,kama wanaolipwa laki 7 kujikuta wanalipwa
laki 3.
Alisema kuwa tatizo la madai ya waalimu ya mishahara na
yasiyo ya mishahara yapo kila Wilaya lakini Wilaya ya Same ndo limekuwa tatizo
kubwa zaidi.
Alisema kuwa hali hiyo itawafanya waalimu waichukie serikali yao kutokana na kutoijali licha ya huduma ambayo imekuwa ikiyoa kwa Serikali.
Hata hivyo alisema
Mkoa wa Kilimanjaro umekuwa ukisifiwa sana
kwenye suala la maendeleo ya elimu hivyo sababu kama
za madai ya malimbikizo ya walimu n zinaweza kuchangia kushuka kwa kiwangp cha
elimu kwa sababu madai waalimu wanayodai ni ya msingi.
No comments:
Post a Comment