Friday, April 27, 2012

   Tundu Lissu ashinda kesi ya kupinga ubunge wake

Tundu Lisu.

Tumeshafika mahakamani, wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa, wananchi wa Singida, na waandishi wa habari wapo wengi sana katika eneo la mahakama.

Polisi ni wengi sana, ndani na nje ya mahakama. Kilicho cha ajabu kidogo leo getini maofisa wote wakubwa wa jeshi la polisi wapo pale na kikosi maalumu kwa ajili ya kumkagua kila anayeingia mahakamani, tunapekuliwa hasa, hadi wabunge wanaoingia.

Kuna baadhi walikatazwa kuingiza magari yao mahakamani lakini baada ya vuta nikuvute, magari yapo mahakamani, na watu wamtinga ndani tunasubiri yatakayojiri.......... tutawajuza, leo kamanda nipo gado, Mungu amenijalia afya
.



Kesi ya chaguzi uliofanyika tarehe 31/10/2010, walalamikaji ni Shabani selema, na Paskali Halu. Walileta mashahidi 24, na vielelezo saba, wanawakilishwa na Wasonga. Kupinga uteuzi wa Lissu kuwa mbunge wa Jimbo la Singida mashariki, kwa madai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.

 Wakidai kuwa kulikuwa na dosari zilizofanya uchaguzi usiwe huru na haki, hivyo kumfanya Mgombea wao wa CCM asishinde.

Walalamikiwa, mlalamikiwa wa kwanza walisema kuwa yeye hakuwemo, au hakuwa mshirika wa tuhuma zilizofanywa. Walalamikiwa wote pamoja wanasema hakuna kitu cha msingi kinachoweza kuifanya mahakama itengue matokeo.

Haijabishaniwi kuwa mgombea alishinda kupitia CHADEMA, kupitia jimbo la singida mashariki, na kumshinda mgombea wa CCM Bw. Njau ambaye alipata nafasi ya pili. Tofauti ya Kura kati ya Lissu na Njau ilikuwa kura 1626.

Mlalamikiwa wa pili, anaunganishwa katika kesi kama necessary paty, kwa kuwa mlalamikiwa wa pili ni Msimamizi wa uchaguzi.

Hoja katika kesi zilikuwa 11.ambapo Mgombea wa walalamikaji (CCM) alikataa kusaini matokeo.


No comments:

Post a Comment