Tukio hilo
la kusikitisha limetokea Aprili 22 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi baada
ya mtoto huyo kufikishwa katika Zahanati binafsi, akiwa na jipu katika makalio
ndipo Daktari alipompokea na kumtoza shilingi 20,000 baba mzazi wa marehemu Rataniel
Mtajiha (45), ili apewe huduma.
Sababu ya
kuchomwa sindano ya ganzi ni kutokana na mtoto huyo kuonaonekana ni mwoga hivyo
achomwe sindano hiyo, na baada ya kuchomwa mtoto huyo alifariki papo
hapo.Wakati huo huo baba mzazi Mtajiha, amesema hakutegemea mwanae
kufikwa na mauti kwani, muda wote alikuwa anacheza licha ya kuwa na jipu hilo.
KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA MBEYA ADVOCATE NYOMBI
Sindano ya ganzi yamsababishia mauti
mtoto Tumaini Rataniel Mtajiha (5), mkazi wa Kijiji cha Hagomba Kata ya Itaka
baada ya kuchomwa na daktari wa zahanati binafsi ya Sisika, inayomilikiwa na
mwalimu mmoja katika Mtaa wa Ichenjezya, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.
Baada ya tukio hilo Mtajiha alitoa taarifa Kituo cha Polisi Vwawa, ambapo
walifika na kumchukua Daktari huyo (Jina linahifadhiwa), mwili wa mtoto na
jalada lake pamoja na sampuli ya dawa
alizotumia hadi kwenye Hospitali ya Wilaya ili kufanyiwa uchunguzi majira ya
saa 10:00 jioni.
Aidha, baada ya kutafakari kwa kina Hospitali hiyo ya wilaya, walitoa
taarifa mkoani na kuagiza mwili ufanyiwe uchunguzi Aprili 23 mwaka huu, baada
ya jopo la mkoani kuwasili wilayani Mbozi ili kufanya uchunguzi wa kina.
Kamanda
wa Polisi mkoani Mbeya hakuweza kupatikana kuthibitisha tukio hili, na hivi
sasa Daktari wa Zahanati hiyo anashikiliwa na Kituo cha polisi Vwawa akisubiri
uchunguzi kufanyika.
|
No comments:
Post a Comment