WAANDAMANA NUSU UCHI KULALAMIKIA POLISI
Wanawake wa uganda |
Kundi la wanawake wamevua nguo, nusu uchi kulalamikia
kitendo cha polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kingono
mwanasiasa wa upinzani.
Kanda ya video imeonyesha polisi
akimtomasatomasa matiti Bi Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha
Forum for Democratic Change (FDC) baadaya kumkamata kuzuia maandamano ya
wiki jana.
Naibu kamishina wa polisi Andrew Kaweesa ameomba
radhi na kuahidi kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo. Tangu
uchaguzi mkuu mwaka 2011 ambapo rais Yoweri Museveni alishinda Uganda
imeshuhudia maandamano ya upinzani ambapo wafuasi wengi wameishia celi
za polisi.
Tukio la wiki jana lilipelekea kuwepo ghadhabu
ya umma ambapo pia lalama zilitanda kupinga kukamatwa kwa Bi Turinawe
ambaye ni kiongozi wa tawi la wanawale katika chama cha FDC
kinachoongozwa na Kizza Besigye.
Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango amesema wanawake
hao waliandamana hadi kituo cha polisi wakiwa vifua wazi na kupeperusha
mabango yaliokuwa na maandishi,''utahisi vipi ikiwa sehemu zako nyeti
zitafinywa''.Wanawake sita walikamatwa baada ya kukataa kufunika vifua
vyao, lakini wakaachiwa huru bila masharti yeyote.
source bbc
No comments:
Post a Comment