Tuesday, June 19, 2012

          M4C yavua magamba wanaccm 70 arumeru Magharibi

HARAKATI za mabadiliko zinazoendeshwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kauli mbiu ‘Vua Gamba Vaa Gwanda’ imezidi kushika kasi mkoani Arusha baada ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 70 wilayani Arumeru kuamua kukikimbia chama hicho.

Katibu wa Chadema mkoani hapa, Amani Golugwa 
Wanachama hao walipokelewa june 16, mwaka huu na katibu wa Chadema mkoani hapa, Amani Golugwa kwenye ofisi zao za mkoa zilizopo maeneo ya Ngarenaro ambapo viongozi mbalimbali wa mkoa walishiriki akiwemo Mwenyekiti wa BAVICHA , Ephata Nanyaro, Mwenyekiti wa BAWACHA, Ceccilian Ndossi na Mwenyekiti wa Chadema, Arumeru Magharibi.



 Wanachama hao walipatiwa kadi za uanachama huku kiongozi wao, Vivian Lebulu akikabidhiwa katiba ya Chadema, bendera ambapo mwenyekiti wa Bawacha alivisha skafu yenye rangi za chama hicho.


Akiongea kwa niaba ya wenzake, Lebulu alisema kuwa wameamua kuachana na CCM baada ya kuona kwa kipindi kirefu imekuwa madarakani huku ikishindwa kutatua kero za wananchi huku akitolea mfano kwenye jimbo hilo asilimia 35 ya wanafunzi wa shule za msingi hukaa chini kwa kukosa madawati.
Alisema kuwa waliamua kujiunga Chadema ili kushiriki kikamilifu harakati ya kuking’oa madarakani chama hicho kupitia sanduku la kura mwaka 2015 kutokana na imani kubwa waliyonayo kuwa chama hicho makini kina sera nzuri za kuwakomboa wanyonge.



Kwa upande wake katibu wa Chadema mkoa, kabla na baada ya kuwapatia Wanachama hao kadi aliwasomea haki na wajibu alionao mwanachadema popote alipo huku akiweka msisitizo umuhimu wa kupinga uonevu na kupigania haki na kulinda utu wa watu wote kwa gharama yoyote.
Aidha alisema kuwa operesheni hiyo itahamia rasmi wilayani Monduli Juni 24, mwaka huu wanapotarajia kuvuna wanachama wengi hasa kutokana na maombi ya muda mrefu ya wananchi wa maeneo hayo ambao wamekuwa wakiwaomba waende ili waweze kurudisha kadi za CCM na wachukue za Chadema.
Golugwa alisema kuwa wakati wa operesheni hiyo wanatazamia kuzindua mashina ya wakereketwa, ofisi za chama na kufanya mikutano ya hadhara ambapo harakati hizo zitaongozwa na viongozi wa mkoa na wilaya.
Kwa upande wao wenyeviti wa mkoa wa BAVICHA, Nanyaro  na BAWACHA, Ndossi waliwataka wanachama hao wapya kujiunga na mabaraza hayo ambayo ni haki ya kila mwachadema kwani yatawawezesha kushiriki kikamilifu katika  harakati za kuleta mabadiko hapa nchini.
Habari na Grace macha.


ASKARI WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA ALIYEKUWA MSANIFU MAJENGO NA MCHORA RAMANI ARUSHA WAACHIWA HURU..


ASKARI wawili waliodaiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa msanifu wa majengo na mchora ramani wa manispaa ya Arusha, Mussa msofe, wameachiwa huru, baada ya Mahakama Kuu kanda ya moshi kutomkuta na hatia mshtakiwa wa kwanza na Mkurugenzi wa mshtaka nchini DPP, kuondoa mashtaka shidi ya mshtakiwa wa pili.

Awali wakili wa serikali, osca ngole, aliieleza mahakama hiyo kuwa dpp, chini ya kifungu namba 91 910 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20, ambacho kinampa mamlaka kumfutia mashtaka mshtakiwa yoyote, ameondoa mashtaka dhidi ya Ex 1089 pc isaya.
Aidha, baada ya taarifa hiyo, wakili huyo alisoma maelezo ya awali ya kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili mshtakiwa kwa kwanza , Ex 7027, Pc James Marwa, ambaye alikiri kutenda kosa hilo, ambapo katika maelezo hayo ilielezwa kuwa tukio la mauaji hayo lilitokea Januari 23, mwaka 2004 katika eneo la makutano ya barabara ya KIA.

Alidai kuwa marehemu alitokea mkoani Arusha na kufika kwenye eneo hilo katika baa ya Rose, ambapo polisi wane walifika baada ya muda mfupio na kuuliza mwenye gari lakini hakujitokeza hadi walipochukua uamuzi wa kulifunga gari lake na ndipo alipojitokeza akiwa na sime.

Alidai palitokea kurupushani baina yao na ndipo marehemu alipokimbilia ndani na kujifungia kwenye moja ya vyumba vyenye mlango wa grili, na kutishia kuua yoyote atakayemsogelea, na ndipo askari hao walipoomba msaada kwa aliyekuwa mkuu wa kituo cha polisi cha kia,saimon haule, kwa madai kuwa kuna jambazi wanapambana nalo ambaye alifika akiwa na askari wengine akiwemo mshtakiwa wa kwanza, alimsihi marehemu kufungua mlango na kumuhakikishia usalama wake alkini alikataa.

Ngole alidai askari hao walipata ufunguo wa ziada na kisha kumpa mkuu huyo wa kituo ambaye alifungua bila marehemu kujua na askari walivamia ndani, na yalianza mapambano na katika mapambana hoyo ndipo risasi moja ilitoka kwenye bunduki aliyokuwa nayo mshtakiwa wa pili Pc isaya na kumpata marehemu eneo la tumbo na kufariki dunia muda mfupi kabla ya kufika hospitali ya mkoa wa kilimanjatro ya mawenzi.

Baada ya maelezo hayo, jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, stella mugasha, alisema haoni haja ya kumtia hatiani mshatkiwa marwa kwa kuwa alikuwa katika harakjati za kumsaidia pc isaya na ndipo risasi ilifyatuka kwa bahati mbaya.

“Nimepitia maelezo ya mshtakiwa na mashahidi ambao wanapaswa kutoa ushahidi kwenye kesi hii, ambao ni mshala, honest na amini sijaona mahali ambako wanamtia hatiani mshatkiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia na mshtakiwa hakuwepo kwenye tukio bali alikuja baadaye” alisema

Hata hivyo, baada ya kusomwa kwa maamuzi hayo, mke wa marehemu msofe, eling msofe, akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, alisema wanakusudia kukata rufaa kwenye mahakama ya rufaa kutokana na kutotrendewa haki.
Mwisho.

ALICHOKIANDIKA KWENYE UKARASA WAKE WA FACEBOOK MH MNYIKA BAADA YA KUFUKUZWA 
BUNGENI..

 
          John Mnyika
Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu!

Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!



Hapa Mnyika akwia nje ya viwanja vya Bunge baada ya kutole ndani ya Bunge na Naibu Spika Job Ndugai.
                                                                      

Monday, June 18, 2012

SALAAM ZA RAMBI RAMBI ZA MH RAIS KWA MSIBA WA MHARIRI WA JAMBO LEO WILLY EDWARD




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Fenella Mukangara kuomboleza kifo cha Mhariri Mtendaji wa Gazeti la JamboLeo, Ndugu Willy Edward Ogunde kilitokea usiku wa kuamkia jana, Jumapili, Juni 17, 2012  mjini Morogoro.
Katika salamu zake za rambirambi, Mheshimiwa Rais Kikwete amesema kuwa ameshtushwa na kusikitishwa na kifo cha ghafla cha Ndugu Willy Edward Ogunde ambaye amepoteza maisha akiwa bado kijana ingawa tayari alikuwa amekwishakutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya tasnia ya habari kutokana na umakini wake, uzingatiaji  wa weledi kikamilifu na misingi mingine mikuu ya uandishi wa habari.
“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi kifo cha ghafla cha Ndugu Willy Edward Ogunde ambaye nimejulishwa kuwa kilitokea usiku wa kuamkia jana, Jumapili, huko Morogoro ambako alikuwa amekwenda kikazi. Ndugu Willy Edward Ogunde amepoteza maisha akiwa bado kijana sana hata kama ni kweli katika muda mfupi wa maisha ametokea kuwa mfano wa kuigwa katika tasnia ya habari kwa mchango wake wa kudumisha weledi na misingi mingine mikuu ya uandishi wa habari.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Nakutumia wewe Mheshimiwa Waziri salamu za dhati ya moyo wangu za rambirambi kuomboleza kifo cha kijana huyu wetu na mwanataaluma wako. Aidha, kupitia kwako nakuomba uniwasilishie salamu zangu kwa wanataaluma wote wa tasnia ya habari nchini kwa kuondokewa na mwenzao. Lakini zaidi, nakuomba unifikishe salamu zangu nyingi kwa wanafamilia, ndugu na jamaa wa Marehemu Willy Edward Ogunde.”
“Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa kwa sababu msiba wao ni msiba wangu pia. Naelewa machungu yao katika kipindi hiki kigumu cha kufiwa na mpendwa wao. Nawaombea subira na uvulivu. Aidha, wajulishe kuwa naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya Marehemu Will Edward Ogunde. Amina,” amesisitiza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
18 Juni, 2012
DAR ES SALAAM

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWANA WA MFALME NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SAUDIA, PIA MWENYEKITI WA ARIGATOU INTERNATIONAL, PIA NAIBU WAZIRI MKUU WA KENYA IKULU LEO


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana naMwana wa Mfalme na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mhe. Abdulaziz Bin Abullah Bin Abdul Aziz Al Saudi
 leo Juni 18, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifanya mazungumzo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana akimsinidikisa Mwana wa Mfalme na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Mhe. Abdulaziz Bin Abullah Bin Abdul Aziz Al Saudi leo Juni 18, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifanya mazungumzo
Rais Jakaya Kikwete akimsindikiza Naibu Waziri Mkuu wa Kenya ambaye pia ni Waziri wa Serikali za Mitaa Mhe. Musalia Mudavadi baada ya mnaongezi yao Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mchungaji Keishi Miyamoto, Rais wa Arigatou na Mwenyekiti wa Bodi ya Myochikai na Mlezi-Mwenza wa Kongamano la Mtandao wa Kimataifa wa Dini kwa Watoto(Global Network of Religions for Children)  leo Juni 18, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifanya mazungumzo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara (hayupo pichani) na viongozi wa chama cha riadha alipokutana nao kwa mazungumzo na kupanga mikakati ya namna ya kufufua mchezo wa riadha nchini. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Riadha nchini William Kallaghe, Mkurugenzi wa Michezo Bw. Thadei na kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Riadha Suleiman Nyambui.PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara aliyekaa kulia (pichani) na viongozi wa chama cha riadha alipokutana nao kwa mazungumzo na kupanga mikakati ya namna ya kufufua mchezo wa riadha nchini. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Riadha nchini William Kallaghe, Mkurugenzi wa Michezo Bw. Thadei na kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Riadha Suleiman Nyambui.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini Dionis Malinzi baada ya kukutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na viongozi wa chama cha riadha alipokutana nao kwa mazungumzo na kupanga mikakati ya namna ya kufufua mchezo wa riadha nchini. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw Sethi Kamuhanda.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais wa Kamati ya Olimpiki Filbert Bayi ionis Malinzi baada ya kukutana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na viongozi wa chama cha riadha alipokutana nao kwa mazungumzo na kupanga mikakati ya namna ya kufufua mchezo wa riadha nchini. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw Sethi Kamuhanda.
AJALI YAUA WATANO NA KUJERUHI 14 KILIAMANJARO..
 
Watu watano  wamefariki dunia huku wengine 14 wakijeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafira kuacha njia na na kupinduka.

Akitoa taarifa ya ajali hiyo Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani Kiliamanjaro Ramadhani Ng’anzi alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 7:00 asubuhi katika eneo la Mbosho barabara ya kware Nguni Kata ya Masama Wilayani Hai.

Alisema kuwa  ajali hiyo ilitokea jana june 17 baada ya gari lenye namba T 179 AAX Toyota Hiace  kuacha  njia gafla na kupunduka,huku dereva aliyekuwa akiendesha akitorokea kusikojulikana.

Nga’nzi Alisema kuwa gari hilo lilikuwa likitokea kware kuelekea boma na watu wote waliokuwa wamepanda kwenye gari hilo walikuwa ni abiria,waliokuwa wanaelekea boma,ambapo watu watatu walipoteza uhai eneo la ajali.

Kamanda Ng’anzi aliwataja  waliopteza maisha kwenye ajali hiyo kuwa ni Eliliwanga lema(90)mkazi wa isuki,Fred Tarimo(23) Mkazi wa masama,Rafael kimaro(66)mkazi wa losaa,Richard Munuo(55)mkazi wa nguni,pamoja na Baraka Nko(45) Mkazi wa Arusha.

Waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo Oscar Siao (45),Alesinda Traeli (50) Leinard munis (32),Husen abdi (63),Amin adabu  Munuo (49) Richard Arnold (18)Devid Joshua (36), Mary witness (44),Walter Rabiel(37),Noel onesmo (9), Elena ngunda (60) Oisael anankya (70)  wilinad amos(37)wengi wao wakiwa ni wakazi wa Hai.

Kamanda alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi,uliodababisha gari hilo kupoteza mwelekeo na kupinduka.

Hata hivyo alisema kuwa uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea,huku miili ya marehemu ikiwa imehifadhiwa hospitali ya kibongoto na majeruhi wakiendelea kupata matibabu hospitali ya rufaa ya KCMC.
Mwisho.

Sunday, June 17, 2012

MWILI WA MAREHEMU WILLY EDWARD WAHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.

Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concerpts Beny Kisaka na Juma Pito wakimfariji mdogo wake na marehemu Willy Edward mara baada ya kuwasili katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako mwili wa marehemu umehifadhiwa, Willy Edward alifariki usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro ambako alikuwa akihudhuria semina  ya Sensa kwa matatizo ya Moyo, Mwili wa marehemu Willy Edward utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Mugumu Serengeti mkoani Mara kwa mazishi
Mwili wa marehemu Willy Edward ukipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jioni ya leo.
Ndugu jamaa na marafiki wa marehemu wakishusha mwili wa marehemu Willya Edward kwenye gari baada ya kuwasili katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhiwa
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akimfariji Kulwa Karedia mhariri wa magazeti ya Mtanzania ambaye alikuwa mmoja wa marafiki nda ndugu waliouleta mwili wa marehemu kutoka mkoani Morogoro., Habari na Fullshangwe. 
            USAFIRI WA BODABODA UNAVYOKATISHA  MAISHA YA WANANCHI..
Wananchi wakimtazama mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda baada ya kugongwa na gari eneo Endask Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara gari la abiria,hata hivyo mmiliki wa blogi hii aliweza kushuhudia ajali hiyo kutokana na gari hilo alilokuwa amepanda kumgonga mwendesha bodaboda huyo.

Sehemu ambayo pikipiki hiyo iliingia kwa upande wa gari kwa mbele na kusababisha kushindwa kuendelea na safari kwa masaa kadhaa hivi.

Hapa askari wa usalama barabarani wakiwa kazini.

Ajali hii ilikuwa mbaya sana asikwambie mtu,watumiaji wa vyombo vya moto hususani pikipiki wanatakiwa kuwa makini sana pindi wanavyotumia vyombo hivyo,kwani ajali hii ilisababishwa na mwendesha pikipiki kuingia barabarani huku akiwa anazungumza na simu na kusababisha kugongwa.

MATUKIO MBALIMBALI YA KAMERA YA TANZANIA LEO NDANI YA MANYARA.
Hapa kamera yetu ilifanikiwa kumnasa kijana mmoja ambaye hakuweza kutambulika jin lake mara moja aliyevalia shati la pinki akipepesuka na kuanguka ovyo baada ya kubugia pombe majira ya saa 7:00 kamili eneo la Kateshi Wilaya ya Hananga Mkoani Manyara.

Hapa wananchi wasamaria wema wakitoa msaada kwa mlevi huyo,ambaye wanenyeji wa eneo hilo walisema kuwa atakuwa amekunywa pombe za kienyeji zinazopatikana maeneo hayo kama Buza na Gongo.

Hapa hata kutembea alikuwa hawezi,lakini vijana tukiendekeza pombe namna hiyo hatutaweza kufanya shughuli za mandeleo,hivyo ni vyema tukajipanga au kuwa na muda maalumu wa kunywa pombe,ama kweli pombe ni nooma


WANANCHI WATAABIKA IPIMAJI WA MALARIA SAME
MKUU WA WILAYA SAME.
                                                                

WANANCHI wa kijiji cha Kizungo kata ya Vumari katika wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro wanatembea umbali wa hadi 20km kufika katika hospitali ya wilaya hiyo kwa ajili ya kupima vimelea vya ugonjwa wa malaria licha ya kuwepo kwa darubini katika zahanati ya kijiji.

Darubini ambayo haitumiki kwa zaidi ya miaka mitano tangu kununuliwa, kutokana na kukosekana kwa mtaalamu, ilinunuliwa na kutolewa kwa wananchi hao na mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Dr David Matayo kwa ajili ya kuwapunguzia wananchi hao adha ya kufuata huduma hiyo umbali mrefu.


Hatahivyo darubini hiyo tangu ikabidhiwe kwa kijiji hicho imehifadhiwa katika zahanati ya Kijiji hai wakati huu, huku wananchi wakiendelea kutaabika.


Mwenyekiti wa kijiji hicho, Kabaka Mndeme aliwaambia waandishi wa habari kijijini hapo juzi kuwa kukosekana kwa huduma hiyo wakati kifaa kinachohitajika kipo ni hatua ya makusudi kwa serikali kuwaataabisha kutafuta huduma hiyo mbali na kijiji chao.


Mndeme alisema wananchi wa kijiji hicho wanaiomba halmashauri na serikali kwa ujumla wake kuwapatia mtaalamu wa kupima ugonjwa huo ili malengo ya mbunge wao wa kuwaletea huduma karibu iweze kufikiwa.


Akitaja changamoto nyingine za kijamii zinazokikabil kijiji hicho  aliseama ni pamoja na mindombinu mibovu ya barabara kutokana na barabara yao iliyomuhimu kiuchumi na kijamii ya Kizungo-Mgagao kutofanyiwa ukarabati hivyo kuathiri kabisa shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.


Aliongeza kuwa kukosekana kwa mtaalamu huyo wa kutumia darubini kunaenda sambamba na kukosekana kwa wataamu wa kada ya elimu hasa katika shule za msingi za Dido na Mbono hali ambayo alisema kunaathiri kiwango cha elimu kwa watoto wao.