AJALI YAUA WATANO NA KUJERUHI 14 KILIAMANJARO..
Watu
watano wamefariki dunia huku wengine 14
wakijeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafira kuacha njia na na
kupinduka.
Akitoa
taarifa ya ajali hiyo Kaimu Kamanda wa polisi Mkoani Kiliamanjaro Ramadhani Ng’anzi
alisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 7:00 asubuhi katika eneo la Mbosho
barabara ya kware Nguni Kata ya Masama Wilayani Hai.
Alisema
kuwa ajali hiyo ilitokea jana june 17
baada ya gari lenye namba T 179 AAX Toyota Hiace kuacha
njia gafla na kupunduka,huku dereva aliyekuwa akiendesha akitorokea
kusikojulikana.
Nga’nzi
Alisema kuwa gari hilo lilikuwa likitokea kware kuelekea boma na watu wote
waliokuwa wamepanda kwenye gari hilo walikuwa ni abiria,waliokuwa wanaelekea
boma,ambapo watu watatu walipoteza uhai eneo la ajali.
Kamanda
Ng’anzi aliwataja waliopteza maisha
kwenye ajali hiyo kuwa ni Eliliwanga lema(90)mkazi wa isuki,Fred Tarimo(23) Mkazi
wa masama,Rafael kimaro(66)mkazi wa losaa,Richard Munuo(55)mkazi wa nguni,pamoja
na Baraka Nko(45) Mkazi wa Arusha.
Waliojeruhiwa
kwenye ajali hiyo Oscar Siao (45),Alesinda Traeli (50) Leinard munis (32),Husen
abdi (63),Amin adabu Munuo (49) Richard Arnold
(18)Devid Joshua (36), Mary witness (44),Walter Rabiel(37),Noel onesmo (9), Elena
ngunda (60) Oisael anankya (70) wilinad
amos(37)wengi wao wakiwa ni wakazi wa Hai.
Kamanda
alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi,uliodababisha gari hilo
kupoteza mwelekeo na kupinduka.
Hata
hivyo alisema kuwa uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea,huku miili ya marehemu
ikiwa imehifadhiwa hospitali ya kibongoto na majeruhi wakiendelea kupata
matibabu hospitali ya rufaa ya KCMC.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment