ASKARI WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA ALIYEKUWA MSANIFU MAJENGO NA MCHORA RAMANI ARUSHA WAACHIWA HURU..
ASKARI wawili waliodaiwa kuhusika
na mauaji ya aliyekuwa msanifu wa majengo na mchora ramani wa manispaa ya
Arusha, Mussa msofe, wameachiwa huru, baada ya Mahakama Kuu kanda ya moshi
kutomkuta na hatia mshtakiwa wa kwanza na Mkurugenzi wa mshtaka nchini DPP,
kuondoa mashtaka shidi ya mshtakiwa wa pili.
Awali wakili wa serikali, osca
ngole, aliieleza mahakama hiyo kuwa dpp, chini ya kifungu namba 91 910 cha
sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20, ambacho kinampa mamlaka
kumfutia mashtaka mshtakiwa yoyote, ameondoa mashtaka dhidi ya Ex 1089 pc isaya.
Aidha, baada ya taarifa hiyo,
wakili huyo alisoma maelezo ya awali ya kesi ya kuua bila kukusudia
inayomkabili mshtakiwa kwa kwanza , Ex 7027, Pc James Marwa, ambaye alikiri
kutenda kosa hilo, ambapo katika maelezo hayo ilielezwa kuwa tukio la mauaji
hayo lilitokea Januari 23, mwaka 2004 katika eneo la makutano ya barabara ya
KIA.
Alidai kuwa marehemu alitokea
mkoani Arusha na kufika kwenye eneo hilo katika baa ya Rose, ambapo polisi wane
walifika baada ya muda mfupio na kuuliza mwenye gari lakini hakujitokeza hadi
walipochukua uamuzi wa kulifunga gari lake na ndipo alipojitokeza akiwa na
sime.
Alidai palitokea kurupushani
baina yao na ndipo marehemu alipokimbilia ndani na kujifungia kwenye moja ya
vyumba vyenye mlango wa grili, na kutishia kuua yoyote atakayemsogelea, na
ndipo askari hao walipoomba msaada kwa aliyekuwa mkuu wa kituo cha polisi cha kia,saimon
haule, kwa madai kuwa kuna jambazi wanapambana nalo ambaye alifika akiwa na
askari wengine akiwemo mshtakiwa wa kwanza, alimsihi marehemu kufungua mlango
na kumuhakikishia usalama wake alkini alikataa.
Ngole alidai askari hao walipata
ufunguo wa ziada na kisha kumpa mkuu huyo wa kituo ambaye alifungua bila
marehemu kujua na askari walivamia ndani, na yalianza mapambano na katika
mapambana hoyo ndipo risasi moja ilitoka kwenye bunduki aliyokuwa nayo
mshtakiwa wa pili Pc isaya na kumpata marehemu eneo la tumbo na kufariki dunia
muda mfupi kabla ya kufika hospitali ya mkoa wa kilimanjatro ya mawenzi.
Baada ya maelezo hayo, jaji
mfawidhi wa mahakama hiyo, stella mugasha, alisema haoni haja ya kumtia hatiani
mshatkiwa marwa kwa kuwa alikuwa katika harakjati za kumsaidia pc isaya na
ndipo risasi ilifyatuka kwa bahati mbaya.
“Nimepitia maelezo ya mshtakiwa
na mashahidi ambao wanapaswa kutoa ushahidi kwenye kesi hii, ambao ni mshala,
honest na amini sijaona mahali ambako wanamtia hatiani mshatkiwa kwa kosa la
kuua bila kukusudia na mshtakiwa hakuwepo kwenye tukio bali alikuja baadaye”
alisema
Hata hivyo, baada ya kusomwa kwa
maamuzi hayo, mke wa marehemu msofe, eling msofe, akizungumza na waandishi wa
habari nje ya mahakama, alisema wanakusudia kukata rufaa kwenye mahakama ya
rufaa kutokana na kutotrendewa haki.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment