Sunday, April 28, 2013
SUALA LA USAFI WA MOSHI LISICHUKULIWE KISIASA...
SAKATA LA MACHINGA KUTII KAULI YA MBUNGE MSIGWA , LACHUKUA SURA MPYA IRINGA
polisi Iringa wakiwa katika eneo la Mashine tatu ,kuondoa mawe na magogo ambayo yalitumika kuziba barabara hiyo kama sehemu ya kushinikiza serikali kuwaruhusu kuendelea kufanya kazi ya umachinga eneo hilo lisiloruhusiwa |
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ikiwa imekutana mchana huu kwa kikao cha dharula kufuatia Machinga kutekeleza kauli ya mbunge Msigwa ya kuvunja sheria |
Hii ndio hali halisi iliyopo eneo la mashine tatu baada ya machinga kurejea eneo hilo leo
KAULI
mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kuwataka
wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) kurejea kufanya kazi katika
eneo la barabara ya Mashine tatu
nusuru asababishe machafuko makubwa eneo hilo kati ya polisi na Machinga.
Msigwa ambae aliitoa kauli hiyo mwanzoni mwa wiki iliyopita katika
mkutano wa wabunge wa chadema waliosimamishwa bungeni ,mkutano
uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa,kwa kuwataka
Machinga kurejea eneo hilo na iwapo mtu atafika kuwanyanyasa basi
wana----!!!?
Machinga
hao jana wameitikia kauli hiyo kwa kurejea eneo hilo na kupelekea
askari wa kutuliza ghasia (FFU) kutanda eneo hilo na kushindwa kutumia
nguvu zaidi ya kuwataka wafanyabiashara hao kuendelea na shughuli zao
eneo hilo .
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio wafanyabiashara hao walisema kuwa wamelazimika kurejea katika eneo hilo baada ya mbunge wao Mchungaji Msigwa kuwaruhusu kufanya biashara katika eneo hilo ambalo mwanzoni walihamishwa na kupelekwa Mlandege .
Hivyo walisema ilikuwa ni vigumu kwao kuondolewa na polisi katika eneo hilo ambalo mbunge kama mwakilishi wao bungeni na vikao vya baraza la madiwani amewaruhusu .
“ujue tulianza kuwashangaa sana polisi wa FFU kufika katika eneo hili na mabomu ya machozi kutaka kutotoa wakati wao wenyewe walikuwepo katika mkutano wa Chadema pale mwembetogwa ambapo mbunge wetu Msigwa alituruhusu kurejea eneo hili….kweli tungeshindwa kulielewa jeshi la polisi iwapo wangetumia nguvu kutuondoa sisi wakati aliyetoa kauli ya kuturuhusu anafahamika “
Kwa upande wake mwanasheria wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Innocent Kihaga alisema kuwa eneo hilo kisheria limepigwa marufuku kwa biashara za umachinga na kuwa
kwa mtu ambae atapatikana akifanya biashara hapo faini yake ni shilingi
50,000 ama kifungo cha miezi sita jela ama vyote kwa pamoja.
Hatua hiyo ya machinga kurejea katika eneo hilo la barabara imeonyesha kuichanganya serikali ya mkoa wa Iringa na kulazimika kukutana kwa masaa kadhaa na kamati ya ulinzi na usalama.
Akizungumzia suala hilo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa na kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Leticia Warioba ambae ni mkuu wa wilaya ya Iringa alisema kuwa serikali ya mkoa inapinga kwa nguvu zote kitendo cha wafanyabiashara hao kurejea eneo hilo.
Dr Warioba alisema kuwa anashangazwa na hatua ya mbunge Msigwa kuwaruhusu wafanyabiashara hao kuvunja sheria wakati mbunge huyo katika vikao vya baraza la madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni diwani ni katika maamuzi ya kuwatoa wafanyabiashara hao alishiriki .
Hata hivyo Dr Warioba aliwataka wafanyabiashara hao kwa jumapili ijayo kutofanyabiashara eneo hilo na kuonya wale wote watakaokiuka kauli hiyo na sheria iliyowekwa juu ya kutofanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi.
Wakati huo mbunge wa jimbo la Mbeya mjini ,Joseph Mbilinyi (MR SUGU) jana ameonekana
katika Manispaa ya Iringa akiingia katika mashine ya kutoa pesa ATM ya
NMB iliyopo nje ya jengo hilo la Manispaa ya Iringa na kusalimiana na
viongozi wa Manispaa waliokuwepo nje ya jengo hilo.
|
Machinga wakiendelea na shughuli zao kama kawaida eneo la mashine Tatu asubuhi hii kutokana na kauli ya mbunge Msigwa kuwaruhusu kurejea ,chini polisi wakiwa eneo hilo |
Hali si shwari katika Manispaa ya Iringa baada ya
kauli mbunge wa
jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kuwataka
wafanyabiashara wadogop wadogo
(machinga) kurejea kufanya kazi katika eneo la barabara ya Mashine
tatu kutekelezwa na machinga hao.
Msigwa ambae aliitoa
kauli hiyo April 23 mwaka huu katika
mkutano wa wabunge wa chadema
waliosimamishwa bungeni
,mkutano uliofanyika katika uwanja
wa Mwembetogwa mjini hapa,kwa kuwataka Machinga kurejea
eneo hilo na iwapo mtu atafika
kuwanyanyasa basi wana----!!!?
Machinga hao leo
wameitikia kauli hiyo kwa kurejea
eneo hilo na kupelekea askari
wa kutuliza ghasia (FFU)
kutanda eneo hilo na kushindwa kutumia nguvu
zaidi ya kuwataka wafanyaiashara
hao kuendelea na shughuli zao
eneo hilo .
habari na francis godwin.Iringa.
.
Timu ya waandishi wa habari ya mpira wa pete(waliovalia jezi za rangi ya njano)wakiwa na wachezajiw a Marenga Investment.Katika mtanange huo timu ya Waandishi wa habari iliweza kuibuka kidedea kwa kuwafunga Marenga mabao 35 kwa mabao 12 hadi mwisho wa pambano.
KWA UPANDE WA MPIRA WA MIGUU MAMBO NAYO YALIKUWA HIVI
WAANDISHI WA HABARI 5-MARENGA 3 HADI DAKIKA 90.
Mchezo huo wa kirafiki ulirushwa moja kwa moja na radio moshi fm ambapo waandishi wa habari walianza kupata bao lao la kwanza dakika ya 1 ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika waandishi waliokuwa wakiongoza kwa bao 3.
Hadi mwisho wa mpira waandishi waliongoza timu zote za mpira wa miguu na mpira wa pete hivyo kuweka historia mpya katika uwanja wa mpira wa Chuo Kikuu cha Ushirika(MUCOBS) Mjini Moshi.
Hapa ni timu ya waandishi wa habari wakingozwa na james Paul wa kwanza kushoto wakijiandaa kuingia uwanjani wakiwa wamevalia jezi nyekundu kama za Man United.
Timu ya Marenga wauza unga hawa waliweza kulambishwa unga na Sukari hatimaye kumwaga chozi uwanjani.
Thursday, April 18, 2013
MEYA WA MOSHI "HATA BODA BODA NI USAFIRI KAMA USAFIRI MWINGINE..
Meya wa Moshi,Japhary Michael (Chadema)kama alivyokutwa na kamera ya Tanzania leo akitumia usafiri wa bodaboda kama mwananchi wa kawaidai licha ya kuwa na gari la Meya pamoja na yeye mwenyewe kumiliki magari.
KITIMA "DEMOKRASIA YA TANZANIA IMETEKWA NA WATU WACHACHE"
Makamu mkuu wa chuo Kikuu cha St Augustine
Dr Charles Kitima Akisisitiza jambo wakati akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari,hawapo pichani.
Na Rodrick Mushi,Mwanza.
, amesema kuwa demokrasia ya Tanzania imetekwa na watu wachache,huku
kukiwepo na msukumo mkubwa kutoka chama tawal (CCM),kuendelea kukandamiza
demokrasia ya vyama vingi ili kiendelee kubaki madarakani.
Kitima aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akifunga
mafunzo kwa waandishi wa habari
za uchunguzi za biashara
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Best Ac, jukwaa la kilomo(ANSAF)kwa kushirikiana na chuo kikuu cha St
Augustino Mwanza.
Mbali na kuwepo kwa matukio mbalimbali ya ukandamizaji wa
demokrasia Kitima alisema kuwa muda wa
CCM kuondoka madarakani ukifika wataondoka kwa aibu na wataingiza taifa kwenye
mahafa mabaya mbeleni.
“CCM ni chama kizuri na sera zake ni nzuri ila kinaponzwa na
watu wachache, mwisho wa siku wananchi wataikataa kwa kutoleta
mabadiliko pamoja na kutotaka kuondoka madrakani”Alisema Kitima.
Alisema kuwa nchi ya Tanzania ingepaswa
kuongozwa kwa nchi za afrika mashariki kuwa nchi yenye demokrasia bora,kutokana
na misingi aliyoacha baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini
misingi hiyo imepotoshwa na baadhi ya viongozi waliokosa uadilifu.
Kitima anasema kuwa demokrasia ni kujali utu na kuheshimu haki ya kila
mtu,watu kujitawala na kuweka serikali inayowajibika kwao,na pindi itakashindwa
kuwajibika itapaswa iondoke na kuomba msamaha kwa kushindwa kuwatendea haki
wanananchi walioichagua.
“Inasikitisha nchi yenye demokrasia na mfumo wa vyama vingi
kusikia chama tawala kikijidai majukwaani kuwa kitaendelea kutawala milele,wakati
wananchi ndiyo wenye maamuzi ya mwisho,huo unaweza ukawa ni ukiukwaji wa demokrasia
au kujiendesha kidikteta”Alisema Kitima.
Kutokana na matukio ya kutekwa kwa demokrasia Kitima alisema
kuwa hali hiyo inaendelea kulelewa nchini,na kuendelea kukua kwani mtu ambaye
anaweza kuiba kura kwenye uchaguzi au kugaramikia wizi wa kura anapewa cheo na
kudhaminiwa.
Matukio mengine ya ukiukwaji wa demokrasia aliyoelezea Kitima
ni pamoja na kufunguliwa kwa kesi wabunge wa upinzani zaidi ya 10 kwa wakati
mmoja,na kushinda kuwatumikia wananchi,huku akihoji ni kwa nini hakuna Mbunge
wa chama tawala ambaye amekuwa akifunguliwa kesi kama wanavyofanyiwa wa
upinzani?
Hata hivyo alieleza kuwa kwa nchi yenye Demokrasia wananchi wanapaswa
kua na sheria zao,ikiwa ni pamoja na haki ya kuwawajibisha viongozi
waliowachagua kwa kushindwa kuwajibika kwao.
Alisema
kuwa Mwalimu Nyerere alijenga misingi mizuri ya demokrasia nchini ya
watu kuheshimiana na kuheshimu haki za wengine,lakini
misingi hiyo imeachwa na baadhi ya viongozi wa sasa.
“Wakati wa enzi za Mwalimu Nyerere michezo hiyo haikuwepo na
alikuwa akigundua unataka kuteka demokrasia kwa kuwanyima haki wananchi
usingeweza kupata madaraka kama inavyofanyika hivi sasa”Alisema Kitima.
Mwisho
PICHA ZA SAFARI YA MWISHO YA BI KIDUDE...
Picha za mazishi ya Bi. Kidude. Viongozi wa serikali kama rais Jakaya
Kikwete, rais wa Zanzibar Ali sheni, makamu wa kwanza wa rais wa
Zanzibar maalim Seif Sharif Hamad, na wasanii kama Mzee Yusuf, Diamond
Platnumz, nk walikua miongoni mwa wahudhuriaji katika kumsindikiza gwiji
huyo wa Taarabu katika safari yake ya mwisho.
Tuesday, April 9, 2013
Profesa Lipumba, alia na uchumi wa Tanga
Profesa Lipumba, akiiangalia ukuta uliojengwa na wananchi wa Kijiji cha Kigombe mkoani Tanga, mara baada ya kuuzindiwa, kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mzee Said.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigombe Mzee Said, akitoa maelezo kwa Profesa Lipumba kuhusu ujenzi wa kingo ya Bahari ambao umejengwa kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa thamani ya Sh milioni 108.
Profesa Lipumba, akiiangalia ukuta uliojengwa na wananchi wa Kijiji cha Kigombe mkoani Tanga, mara baada ya kuuzindiwa, kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mzee Said.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigombe Mzee Said, akitoa maelezo kwa Profesa Lipumba kuhusu ujenzi wa kingo ya Bahari ambao umejengwa kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa thamani ya Sh milioni 108.
washiriki wa kongamano hilo wakimsikiliza kwa makini. 3. Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), akifuatilia mada kuhusu uchumi wa mkoa inayowasilishwa na Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba, akipata maelezo ya zahanati ya Kijiji cha Kigombe kutoka kwa Daktari wa zahanati hiyo Dk. Uwesu Mtulia.
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Mkoa wa Tanga ni moja kati ya mikoa maarufu kwa viwanda nchini lakini hivi saa hali ya kimaendeleo katika mkoa huo imekuwa mbaya.
Kauli hiyo ameitoa leo mjini hapa alipokuwa akiwasilisha mada inayohusu maendeleo ya uchumi kwa Mkoa wa Tanga katika kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kwa kushirikiana Taasisi ya Maendeleo ya demokrasi kwa vyama vya siasa ya nchini Denmark (DIPD).
Profesa Lipumba alisema kuwa hakuna haki bila kuwa na maendeleo yanamgusa mwananchi wa kawaida.
Alisema Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuwa na rasimali nyingi ikiwemo zao la Mkonge ambalo kwa sasa limekosa msukomo hali inayochangia umaskini kwa wananchi wa mkoa huo.
"Pamoja na Tanga kuwa na fursa nyingi za kiuchumi lakini bado kadri siku zinavyokwenda umaskini umekuwa ukiwatesa wananchi. Viwanda vilikuwa zaidi ya 70 lakini sasa hakuna hata kimoja kinachofanya kazi huku zao la mkonge lilikosa msukumo wa makusudi kwa wananchi wake.
"Katika soko la dunia inaonyesha kuwa Tanga ilikuwa ikizalisha tani 234,000 kwa mwaka lakini sasa mkonge umeporomoka na kufikia tani 25,000 tu hali ambayo imekuwa ikiongeza umaskini kila kukicha. Kama kungekuwa na msukumo wa makusudi wa kufufu zao hili ni wazi Tanga ingekuwa imepaa kimaendelo kwa wananchi wake kutokana na kuwa na kila aina ya rasilimali zikiwemo za matunda na mbogamboga," alisema Profesa Lipumba
Profesa Lipumba, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi duniani, alisema ili kuweza kufikia malengo ya mkoa huo kuweza kupambana na umaskini ni lazima serikali ikubali kwa kufanya uwekezaji hasa katika kufungua bandari ya Tanga ambayo ni lango kuu la kiuchumi.
Alisema Bandari ya Tanga imekuwa haitumiki ipasavyo hali inawechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa umaskini na hazorotesha harakati za mkoa na wananchi kwa ujumla.
"Bandari ya Tanga, zao la mkonge pamoja na kukosekana kwa msukumo wa kuimarisha sekta ya elimu ni moja ya masuala yanayoufanya mkoa huu kuzidi kurudi nyuma kiuchumi pamoja na wananchi wake,” alisema Profesa Lipumba.
Monday, April 8, 2013
KIKULETWA KUFUFULIWA JE CHUO CHA ARUSHA KITAWEZA KUZALISHA UMEME KAMA ILIVYOKUWA APO AWALI??
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama(Katikati) akipata maelezo ya
Kituo cha Kuzalisha umeme cha Kikuletwa kilichopo wilayani Hai mkoani
Kilimanjaro kutoka kwa Mtaalamu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Aliyesimama
nyuma ya mkuu wa mkoa mwenye miwani ni mkuu wa chuo hicho Dk Richard
Masika
Chuo cha
Ufundi Arusha kimeanza mkakati wa kufufua mitambo ya kuzalishia umeme wa maji wa
Kituo cha Kikuletwa iliyopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo hadi
itakapokamilika itaweza kutosheleza mahitaji ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha
na umeme mwingine kubaki.
Ufafanuzi
huo umetolewa na mkuu wa Chuo hicho Dk
Richard Masika kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama aliyetembelea
mitambo hiyo ambayo imekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Umeme
Nchini(TANESCO)
Alisema
kuwa chuo hicho ambach kitakuwa cha kwanza barani Afrika kumiliki kituo cha
kufua umeme,kitatumia kituo hicho kwa malengo matatu ambayo ameyataja kuwa ni
pamoja na kutumika kwa mafunzo,kutengeneza vipuri vya mitambo ya umeme pamoja
na kuzalisha umeme.
Dk Masika
ameeleza kuwa baada ya kukabidhiwa kituo hicho mapema wiki iliyopita na baadaye
kuanza kazi za awali wamebaini kwamba kwa kufunga mitambo mipya ya kufua umeme
wataweza kutoa megawati 17 ambazo zitaingizwa katika gridi ya taifa.
“Kiasi
hicho kitaweza kutosheleza mahitaji ya umeme kwa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha
na kiasi kingine kubaki,”
Akifafanua
zaidi alisema kuwa kituo hicho ambacho kilijengwa mwaka 1930 kwa sasa kina
mashine tatu ambazo zilikufa na kuacha kuzalisha umeme mwishoni mwa miaka ya
Themanini zikiwa na uwezo wa kuzalisha umeme kati ya megawati moja na moja na
nusu.
Dk Masika
ameeleza kuwa mashine mbili kati ya hizo tatu chuo chake kina uwezo wa
kuzifufua na kuanza kufua umeme utakaoingizwa katika gridi ya taifa wakati chuo
chake kikiendelea na mkakati wa mpango mkubwa wa uzalishaji umeme kwa kutumia
mitambo ya kisasa
Kwa upande
wa mafunzo,Dk Masika ameeleza kuwa cuo hicho kimelenga kutoa idadi kubwa ya
wataalamu wafanyakazi ambao wenye taalamu ya stashahada ambao kwa kawaida ndiyo
wacahapa kazi ili kuzipa pengo la sasa la idadi kubwa kukimbilia katika shahada
na baada ya kuhitimu kwa wasimamizi na si wachapa kazi
Alisema
kuwa mitambo ya kituo hicho chenye eneo la jumla ya Ekari 400 yanategemea maji
ya mito miwili ambayo Kware unaoanzia Mlima Kilimanjaro na Mto Mbuguni unaonzia
mlima Meru ambapo maji hayo huduma katika kipindi kizima cha mwaka na
kuongezeka wakati wa kiangazi
Kwa upande
wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanajro,Gama amewataka wataalamu wa cuo hicho pamoja
na mipango mizuri na kuonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kukiendesha lakini
aliwataka kuwa na uzalendo ambao utalisaidia taifa katika kutatua tatizo la
upatikanaji wa nishati ya umeme.
Alisema
kuwa ni vyema sasa wakatambua kwamba taifa limewapa dhamana kubwa kwa
kuwakabidhi raslimali kubwa ambayo inatakiwa kusimamiwa vyema kwa ajili ya
manufaa ya watanzania na siyo ya watu binafsi.
Gama
aliwataka kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji yanayotumika katika mitambo
hiyo vya Chemka kilichopo wilayani Hai na cha Mto Mbuguni ambacho kipo wilayani
Arumeru mkoani Arusha.
Alisema
kuwa uongozi wa serikali mkoani Kilimanjaro unakiweka kituo hicho katika miradi
yake mikubwa ya kimkoa na utakuwa tayari kikusaidia chuo hicho wakati wowote
kitakapohitaji msaada wa hali na mali.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameahidi kukipa ushirikiano chuo
hicho na kukitaka kuhakikisha kinaimarisha kitengo chake cha uhusiano ili kujenga
mahusiano na vijiji vinavyozunguka kituo hicho.
Alisema
kuwa kutokana na mazingira yanayozunguka kituo hicho kutunzwa vizuri katika
miaka yote tangu uzalishaji uliposiamama,mara nyingine wakati wa ukame mkali
baadhi ya wenyeji ujaribu kuingiza mifugo kwa ajili ya kupata malisho na hivyo
kusababisha vurugu.
Makunga
alisema kuwa ni vyema chuo hicho kikajipanga kwa kushirikiana na uongozi wa
wilaya katika kuhakikisha kinawaelimisha wananchi wanaoishi maeneo ya jirani
ili watambue umuhimu wa kituo hicho na madhara ya kutaka kuingiza mifugo kwa
nguvu
Tuesday, April 2, 2013
WAANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ZA BIASHARA NA UCHUMI IBJ WAANZA MAFUNZO YAO ST AGOSTINO UNIVERSITY MWANZA...
Kaimu Mkuu wa Chuo kikuu cha St Agustiono Mwanza Padre Tadeus Mkamwa akizungumza na waandishi wa habari wanaosoma mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi za biashara course ambayo ilianza mwaka jana |
Mkufunzi wa chuo kikuu cha St Agustino Denis Mpagaze akitoa mada kwa waandishi wa habari(hawapo pichani). |
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini,television,magazeti na radio,ambao ni wanafunzi wa course ya habari za uchunguzi za biashara yanayoendelea chuo Kikuu cha St Agostino Mwanza. |
WAANDISHI wa
habari nchini wamesisitizwa kusoma zaidi ili kuboresha taaluma zao kwa lengo la
kuisaidia nchi kutokana na matatizo yanayoikabili.
Makamu mkuu
wa chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT)Dk,Padri Thadeus Mukamwa amewaambia
waandishi wa habari 16 wanaosoma kozi za uandishi wa habari za uchunguzi biashara katika chuo kikuu hicho.
Amesema
waandishi ni chachu ya mabadiliko hivyo wanapaswa kujiongezea maarifa ,”tumieni
maarifa hayo kwa maslahi ya umma wala si kwa maslahi yenu….angalieni maslahi ya
umma kwanza”alisema.
Alitoa mfano
wa nchi ya Marekani kuwa wagombea wake walitanguliza zaidi nchi kuliko nafasi
zao.
“Uhuru wa
waandishi katika nchi zingine unalindwa sana …ingawa kwetu hapa kuna matatizo
mengi yanayowasibu…lakini jikiteni zaidi kuandika ukweli kwa kuibua changamoto
zinazokabili jamii”alisema Mukamwa.
Mmoja wa
wakufunzi wa kozi hiyo iliyoanza julai 2012 chini ya ufadhili wa Best –Ac,Ansaf
na Saut aliwataka waandishi kuwa na malengo ili kuboresha taaluma yao.
“Someni,fanyeni
utafiti ili msiwe waandishi wa kupelekwa na wimbi la wanasiasa …chambueni issue
ili muweze kuleta mabadiliko kwa kuibua mambo ambayo yanatasaidia kukuza uchumi
wa nchi na kufichua mambo yanayosumbua kama mikataba “alisema.
Subscribe to:
Posts (Atom)