Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama(Katikati) akipata maelezo ya
Kituo cha Kuzalisha umeme cha Kikuletwa kilichopo wilayani Hai mkoani
Kilimanjaro kutoka kwa Mtaalamu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Aliyesimama
nyuma ya mkuu wa mkoa mwenye miwani ni mkuu wa chuo hicho Dk Richard
Masika
Chuo cha
Ufundi Arusha kimeanza mkakati wa kufufua mitambo ya kuzalishia umeme wa maji wa
Kituo cha Kikuletwa iliyopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ambapo hadi
itakapokamilika itaweza kutosheleza mahitaji ya mikoa ya Kilimanjaro na Arusha
na umeme mwingine kubaki.
Ufafanuzi
huo umetolewa na mkuu wa Chuo hicho Dk
Richard Masika kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama aliyetembelea
mitambo hiyo ambayo imekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Umeme
Nchini(TANESCO)
Alisema
kuwa chuo hicho ambach kitakuwa cha kwanza barani Afrika kumiliki kituo cha
kufua umeme,kitatumia kituo hicho kwa malengo matatu ambayo ameyataja kuwa ni
pamoja na kutumika kwa mafunzo,kutengeneza vipuri vya mitambo ya umeme pamoja
na kuzalisha umeme.
Dk Masika
ameeleza kuwa baada ya kukabidhiwa kituo hicho mapema wiki iliyopita na baadaye
kuanza kazi za awali wamebaini kwamba kwa kufunga mitambo mipya ya kufua umeme
wataweza kutoa megawati 17 ambazo zitaingizwa katika gridi ya taifa.
“Kiasi
hicho kitaweza kutosheleza mahitaji ya umeme kwa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha
na kiasi kingine kubaki,”
Akifafanua
zaidi alisema kuwa kituo hicho ambacho kilijengwa mwaka 1930 kwa sasa kina
mashine tatu ambazo zilikufa na kuacha kuzalisha umeme mwishoni mwa miaka ya
Themanini zikiwa na uwezo wa kuzalisha umeme kati ya megawati moja na moja na
nusu.
Dk Masika
ameeleza kuwa mashine mbili kati ya hizo tatu chuo chake kina uwezo wa
kuzifufua na kuanza kufua umeme utakaoingizwa katika gridi ya taifa wakati chuo
chake kikiendelea na mkakati wa mpango mkubwa wa uzalishaji umeme kwa kutumia
mitambo ya kisasa
Kwa upande
wa mafunzo,Dk Masika ameeleza kuwa cuo hicho kimelenga kutoa idadi kubwa ya
wataalamu wafanyakazi ambao wenye taalamu ya stashahada ambao kwa kawaida ndiyo
wacahapa kazi ili kuzipa pengo la sasa la idadi kubwa kukimbilia katika shahada
na baada ya kuhitimu kwa wasimamizi na si wachapa kazi
Alisema
kuwa mitambo ya kituo hicho chenye eneo la jumla ya Ekari 400 yanategemea maji
ya mito miwili ambayo Kware unaoanzia Mlima Kilimanjaro na Mto Mbuguni unaonzia
mlima Meru ambapo maji hayo huduma katika kipindi kizima cha mwaka na
kuongezeka wakati wa kiangazi
Kwa upande
wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanajro,Gama amewataka wataalamu wa cuo hicho pamoja
na mipango mizuri na kuonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kukiendesha lakini
aliwataka kuwa na uzalendo ambao utalisaidia taifa katika kutatua tatizo la
upatikanaji wa nishati ya umeme.
Alisema
kuwa ni vyema sasa wakatambua kwamba taifa limewapa dhamana kubwa kwa
kuwakabidhi raslimali kubwa ambayo inatakiwa kusimamiwa vyema kwa ajili ya
manufaa ya watanzania na siyo ya watu binafsi.
Gama
aliwataka kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji yanayotumika katika mitambo
hiyo vya Chemka kilichopo wilayani Hai na cha Mto Mbuguni ambacho kipo wilayani
Arumeru mkoani Arusha.
Alisema
kuwa uongozi wa serikali mkoani Kilimanjaro unakiweka kituo hicho katika miradi
yake mikubwa ya kimkoa na utakuwa tayari kikusaidia chuo hicho wakati wowote
kitakapohitaji msaada wa hali na mali.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ameahidi kukipa ushirikiano chuo
hicho na kukitaka kuhakikisha kinaimarisha kitengo chake cha uhusiano ili kujenga
mahusiano na vijiji vinavyozunguka kituo hicho.
Alisema
kuwa kutokana na mazingira yanayozunguka kituo hicho kutunzwa vizuri katika
miaka yote tangu uzalishaji uliposiamama,mara nyingine wakati wa ukame mkali
baadhi ya wenyeji ujaribu kuingiza mifugo kwa ajili ya kupata malisho na hivyo
kusababisha vurugu.
Makunga
alisema kuwa ni vyema chuo hicho kikajipanga kwa kushirikiana na uongozi wa
wilaya katika kuhakikisha kinawaelimisha wananchi wanaoishi maeneo ya jirani
ili watambue umuhimu wa kituo hicho na madhara ya kutaka kuingiza mifugo kwa
nguvu
No comments:
Post a Comment