Na Rodrick Mushi,Mwanza.
, amesema kuwa demokrasia ya Tanzania imetekwa na watu wachache,huku
kukiwepo na msukumo mkubwa kutoka chama tawal (CCM),kuendelea kukandamiza
demokrasia ya vyama vingi ili kiendelee kubaki madarakani.
Kitima aliyasema hayo mwishoni mwa wiki, wakati akifunga
mafunzo kwa waandishi wa habari
za uchunguzi za biashara
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini yaliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Best Ac, jukwaa la kilomo(ANSAF)kwa kushirikiana na chuo kikuu cha St
Augustino Mwanza.
Mbali na kuwepo kwa matukio mbalimbali ya ukandamizaji wa
demokrasia Kitima alisema kuwa muda wa
CCM kuondoka madarakani ukifika wataondoka kwa aibu na wataingiza taifa kwenye
mahafa mabaya mbeleni.
“CCM ni chama kizuri na sera zake ni nzuri ila kinaponzwa na
watu wachache, mwisho wa siku wananchi wataikataa kwa kutoleta
mabadiliko pamoja na kutotaka kuondoka madrakani”Alisema Kitima.
Alisema kuwa nchi ya Tanzania ingepaswa
kuongozwa kwa nchi za afrika mashariki kuwa nchi yenye demokrasia bora,kutokana
na misingi aliyoacha baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere lakini
misingi hiyo imepotoshwa na baadhi ya viongozi waliokosa uadilifu.
Kitima anasema kuwa demokrasia ni kujali utu na kuheshimu haki ya kila
mtu,watu kujitawala na kuweka serikali inayowajibika kwao,na pindi itakashindwa
kuwajibika itapaswa iondoke na kuomba msamaha kwa kushindwa kuwatendea haki
wanananchi walioichagua.
“Inasikitisha nchi yenye demokrasia na mfumo wa vyama vingi
kusikia chama tawala kikijidai majukwaani kuwa kitaendelea kutawala milele,wakati
wananchi ndiyo wenye maamuzi ya mwisho,huo unaweza ukawa ni ukiukwaji wa demokrasia
au kujiendesha kidikteta”Alisema Kitima.
Kutokana na matukio ya kutekwa kwa demokrasia Kitima alisema
kuwa hali hiyo inaendelea kulelewa nchini,na kuendelea kukua kwani mtu ambaye
anaweza kuiba kura kwenye uchaguzi au kugaramikia wizi wa kura anapewa cheo na
kudhaminiwa.
Matukio mengine ya ukiukwaji wa demokrasia aliyoelezea Kitima
ni pamoja na kufunguliwa kwa kesi wabunge wa upinzani zaidi ya 10 kwa wakati
mmoja,na kushinda kuwatumikia wananchi,huku akihoji ni kwa nini hakuna Mbunge
wa chama tawala ambaye amekuwa akifunguliwa kesi kama wanavyofanyiwa wa
upinzani?
Hata hivyo alieleza kuwa kwa nchi yenye Demokrasia wananchi wanapaswa
kua na sheria zao,ikiwa ni pamoja na haki ya kuwawajibisha viongozi
waliowachagua kwa kushindwa kuwajibika kwao.
Alisema
kuwa Mwalimu Nyerere alijenga misingi mizuri ya demokrasia nchini ya
watu kuheshimiana na kuheshimu haki za wengine,lakini
misingi hiyo imeachwa na baadhi ya viongozi wa sasa.
“Wakati wa enzi za Mwalimu Nyerere michezo hiyo haikuwepo na
alikuwa akigundua unataka kuteka demokrasia kwa kuwanyima haki wananchi
usingeweza kupata madaraka kama inavyofanyika hivi sasa”Alisema Kitima.
Mwisho
No comments:
Post a Comment