Tuesday, April 2, 2013

WAANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI ZA BIASHARA NA UCHUMI IBJ WAANZA MAFUNZO YAO ST AGOSTINO UNIVERSITY MWANZA...

Kaimu Mkuu wa Chuo kikuu cha St Agustiono Mwanza Padre Tadeus Mkamwa akizungumza na waandishi wa habari wanaosoma mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi za biashara course ambayo ilianza mwaka jana

Mkufunzi wa chuo kikuu cha St Agustino Denis Mpagaze akitoa mada kwa waandishi wa habari(hawapo pichani).

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini,television,magazeti na radio,ambao ni wanafunzi wa course ya habari za uchunguzi za biashara yanayoendelea chuo Kikuu  cha St Agostino Mwanza.
WAANDISHI wa habari nchini wamesisitizwa kusoma zaidi ili kuboresha taaluma zao kwa lengo la kuisaidia nchi kutokana na matatizo yanayoikabili.

Makamu mkuu wa chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT)Dk,Padri Thadeus Mukamwa amewaambia waandishi wa habari 16 wanaosoma kozi za uandishi wa habari za uchunguzi  biashara katika chuo kikuu hicho.

Amesema waandishi ni chachu ya mabadiliko hivyo wanapaswa kujiongezea maarifa ,”tumieni maarifa hayo kwa maslahi ya umma wala si kwa maslahi yenu….angalieni maslahi ya umma kwanza”alisema.
Alitoa mfano wa nchi ya Marekani kuwa wagombea wake walitanguliza zaidi nchi kuliko nafasi zao.

“Uhuru wa waandishi katika nchi zingine unalindwa sana …ingawa kwetu hapa kuna matatizo mengi yanayowasibu…lakini jikiteni zaidi kuandika ukweli kwa kuibua changamoto zinazokabili jamii”alisema Mukamwa.

Mmoja wa wakufunzi wa kozi hiyo iliyoanza julai 2012 chini ya ufadhili wa Best –Ac,Ansaf na Saut aliwataka waandishi kuwa na malengo ili kuboresha taaluma yao.
“Someni,fanyeni utafiti ili msiwe waandishi wa kupelekwa na wimbi la wanasiasa …chambueni issue ili muweze kuleta mabadiliko kwa kuibua mambo ambayo yanatasaidia kukuza uchumi wa nchi na kufichua mambo yanayosumbua kama mikataba “alisema.

No comments:

Post a Comment