Wednesday, March 13, 2013

KANISA KATOLIKI LAPATA PAPA MPYA.


Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina amechaguliwa kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki.
Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa.
Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.
Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa. Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao.
Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.
Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.
Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya.
Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani angelichaguliwa.
Moshi mweupe
Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne.
Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa .

Papa Francis I ni nani?

Alizaliwa Mjini Buenos Aires huko Argentina mwaka1936.
Papa Francis 1 ni mtu wa kwanza katika kipindi cha miaka elfu moja (1,000) kwa mtu kutoka nje ya bara la Ulaya kutawazwa kuwa papa wa Kanisa Katoliki.
Papa Francis 1 ni mwana wa Mtaliano aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la gari Moshi kabla ya kuhamia nchini Argentina miaka ya zamani.
Kama kadinali wa Jimbo la Buenos Aires ,Kadinali Bergoglio amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Argentina.
Hata hivyo Kadinali Bergoglio anapendwa sana na wafuasi wa kanisa hilo huko Argentina na hasa watu maskini.
adinali Jorge Bergoglio, mwenye umri wa mwaka 76, kwa karibu miaka yake yote kama Kasisi amehudumu nyumbani kwao Argentina.
Kadinali huyo wa Jimbo la Buenos Aires inasemekana aliibuka nambari mbili wakati Papa Benedict alipochaguliwa mwaka 2005
Papa Francis akijitokeza
Anaaminika kuwa na ujuzi mkubwa ambao wengi wanasema utamsaidia sana katika uongozi wake.
Katika maisha yake ya huduma kwa Kanisa Katoliki huko Amerika Kusini ambapo Kanisa Katoliki lina waumini wengi zaidi duniani, Kadinali Bergoglio ameibuka kuwa mtu anayependa sana udhabiti wa kisiasa katika nchi zilizo katika bara la Amerika Kusini.
Bergoglio anasifiwa kwa kuleta mageuzi makubwa katika Kanisa la Argentina huku katika eneo hilo la Amerika Kusini Kanisa bado linashikilia itikadi za kale.
source BBC.

Sunday, March 10, 2013

SIMBA BADO TUPO..


Wachezaji wa Simba, Abdallah Seseme, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa wakimpongeza Haruna Chanongo (6) kufunga bao la pili katika mchezo wa leo.

Na Mahmoud Zubeiry
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wamezinduka leo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wao, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Uwanjwa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Simba SC itimize pointi 34, baada ya kucheza mechi 19, ikiendelea kubaki nafasi ya tatu, nyuma ya Azam FC yenye pointi 37, wakati wapinzani wao wa jadi, Yanga SC wapo kileleni kwa pointi zao 45.  
Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyopatikana ndani ya dakika tatu za muda wa nyongeza baada ya kutimu kwa dakika 45 za kipindi hicho.
Coastal ndio waliuanza vema mchezo huo, wakisukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba na kama si uimara wa kipa Mganda, Abbel Dhaira wangeweza kupata bao la mapema.
Ndani ya dakika tatu, kipa huyo namba wa Uganda aliokoa michomo miwili ya hatari, mmoja wa chini na mwingine wa juu na kuwafanya mashabiki wa Simba warukwe kwa shangvwe, wakiamini wamepata kipa bora.
Ikumbukwe hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa Dhaira kudaka katika Uwanja wa Taifa tangu asajiliwe Simba SC dirisha dogo akitokea Iceland nay a pili katika ardhi ya Tanzania, baada ya Simba na Bandari Kombe la Mapinduzi.
Kiulainiii; Mrisho Ngassa akiifungia Simba SC bao la kwanza leo. Kipa Shaaban Kado amekwishapotea mabode kulia, langoni yupo beki Philip Mugenzi, ambaye hakuwa na la kufanya.
Zaidi ya hapo, Dhaira alidaka dakika 45 kila mechi katika mechi mbili za kirafiki nchini Oman na dakika zote 90, wakati Simba ikilala 4-0 mbele ya Recreativo de Libolo nchini Angola wiki iliyopita.     
Mrisho Khalfan Ngassa alikuwa wa kwanza kuwainua vitini wana Simba dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza, baada ya kumchambua kipa Shaaban Kado, akimalizia gonga safi zilizosababisha kizazaa langoni mwa Wagosi wa Kaya.
Haruna Athumani Chanongo alipigilia msumari wa pili kwenye ‘jeneza’ la Coastal hii leo dakika ya tatu wa muda nyonegza akimalizia kazi nzuri ya Ngassa, kufuatia shambulizi la kushitukiza. 
Kipindi cha pili, Coastal walikianza tena kwa kasi na kufanikiwa na kupata bao la kufutia machozi dakika ya 49 na ushei, lililofungwa na kiungo Razack Khalfan aliyeunganisha krosi ya Twaha Shekuwe.
Baada ya hapo, timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu na hadi kipyenga cha refa Martin Sanya kutoka Morogoro kinapulizwa kuhitimisha mchezo huo, Wekundu wa Msimbazi waliibuka kidedea.
Simba SC ilichelewa kuingia uwanjani hii leo na kukosa hata muda wa kupasha misuli moto, kutokana na matatizo ya kufungiwa hotelini.  
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Miraj Adam, Hassan Hatibu, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Rashid Ismail/Saim Kinje, Abdallah Seseme, Haruna Chanongo na Mrisho Ngassa/Ramadhan Singano ‘Messi’.
Coastal Union; Shaaban Kado, Hamad Hamisi, Abdi Banda, Mbwana Hamisi, Philip Mugenzi, Razack Khalfan, Daniel Lyanga/Twaha Shekuwe, Mohamed Athumani, Deangelis da Silva, Suleiman Kassim ‘Selembe’ na Joseph Mahundi/Castory Mumbara. 

USHINDI WA UHURU WAMFUNGA MDOMO MAGUFULI.

Uhuru Kenyetta Rais  wa Taifa la Kenya

WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli jana aliungana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsavangirai kumpigia debe mgombea wa urais wa Kenya, Raila Odinga huku akisema mgombea huyo kupitia Chama cha Orange Democratic Party (ODM), anastahili kuwa Rais wa nchi hiyo kutokana na sifa zake za uongozi.


Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa ODM jana, Dk Magufuli alisema hakuna sababu zozote zitakazowafanya Wakenya wasimchague Odinga.

“Nataka kuwaambia Wakenya kwamba Odinga ni mcha Mungu, mnatakiwa kujua hilo. Kama mimi ningekuwa Mkenya ningempigia huyu jamaa kura ili aongoze nchi. Lakini sasa kwa kuwa siruhusiwi hata kupiga kura, basi nawaambia msiache kumchagua huyu atawaongozeni vizuri,” alisema Dk Magufuli.


Dk Magufuli alisema kati ya wagombea wote waliojitokeza kuwania kiti cha urais nchini Kenya, hakuna anayemfikia Odinga na hiyo inaonyesha kuwa wakimchagua atawasaidia bila ubaguzi.

Waziri Dkt Magufuli.
Alisema na hata Odinga ambaye ni Waziri Mkuu wa Kenya akiamua kugombea ubunge katika Jimbo lake la Chato, hawezi kumshinda.
“Kwa hiyo nasimama hapa ndugu zangu wana ODM kuwapa pongezi kubwa sana, mmmefanya kitu kikubwa sana kwa sababu mmechagua jembe,” alisema.

MACHANGU AWAPIGA JEKI WANAWAKE KILIMANJARO.

 Picha namba 62:Mbunge wa Viti maalumu Mkoani Kilimanjaro Betty Machangu akizungumza na wanawake wa Kata ya Uru Kusini,Wilaya ya Moshi Vijijini wakati alipofika kutekeleza ahadi yake waliyokuwa wameomba kwa Mbunge huo ya kuwaanzishia mradi wa Nguruwe.
 Mbunge wa Viti Maalumu Betty Machangu mkoani Kilimanjaro(CCM)akikabidhi Mradi wa nguruwe kwa wanawake wa umoja wa wanawake UWT Kata za Uru Kusini na Uru Mashariki.kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.,Picha na Rodrick Mushi.
Mbunge wa Viti Maalumu Betty Machangu mkoani Kilimanjaro(CCM)(katikati)akizungumza na wanawake wa Kata ya Mbokomu baada ya kuwakabidhi mradi wa nguruwe pamoja na mashine ya kuangulia vifaranga likiwa ni ombi la wanawake wa Kata hiyo baada ya Mbunge kufanya ziara kwenye Kata hiyo.Picha na Rodrick Mushi.


Mbunge wa Viti Maalumu Betty Machangu mkoani Kilimanjaro(CCM) amesema kuwa ili wanawake kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na hali ya kuwa  tegemezi ni vema wakajiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi kuweza kupatiwa mikopo katika taasisi mbalimbali za fedha ili kuanzisha miradi.

Alisema kuwa kuna taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitoa mikopo kwa bei nafuu,ikiwemo Vicoba pamoja Saccos hivyo wanawake wakijiunga kwenye vikundi itakuwa rahisi kupatiwa fedha na kujiingiza kwenye shughuli za ujasiriamali.

Machangu aliyasema hayo wakati akikabidhi miradi mbalimbali ikiwemo ya nguruwe pamoja na mashine za kuangulia vifaranga kwa wanawake wa Umoja wa Wanawake CCM kwenye Kata za Uru Kusini,Uru Mashariki na Kata ya Mbokomu kutoka Wilaya ya Moshi Vijijini.

Hata hivyo alisema kuwa utoaji wa miradi hiyo ameitoa kwenye Kata hiyo baada ya ziara yake kwenye Wilaya Mbalimbali za Mkoa wa Kilimanajaro na kusikiliza vipaumbele vyao walivyotoa kwake ili kuweza kuanzisha miradi na kujikwamua na umaskini.

“Nilifanya ziara yangu kila tarafa na kila Wilaya,hivyo niliwaambia wanawake wanipe vipaumbele vyao ili niweza kuwasaidai,ndio wanawake niliowakabidhi msaada huu leo wakaniomba miradi ya nguruwe na kuku,nab ado kuna Wilaya nyingine wameomba miradi kama ya mbuzi”Alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Wilaya ya moshi Vijijini Grace mzava alisema kuwa njia pekee ya mwanamke kuweza kujikwamua na hali ngumu ya maisha ni kujishighulisha katika kazi mbalimbali za Ujasiriamali.

Alisema kuwa wapo wanawake ambao wamekuwa najitihada za kujiingiza na kubuni miradi lakini changamoto kubwa imekuwa ni mtaji,hivyo wengi kujikuta wakishindwa kufikia malengo hivyo wanawake wakisaidia miradi idadi ya wanawake tegemezi itapungua.

MBIO ZA NYIKA TAIFA ZIMEFANYIKA LEO MJINI MOSHI; ARUSHA WATESA


 DICKSON MARWA AKIMALIZA
 WANARIADHA WA KILOMETA 12 KATUIKA MBIO ZA NYIKA
WANARIADHA WA KILOMETA 12 WALIPOANZA KUTIMUA MBIO

WANARIADHA kutoka mikoa mbalimbali nchini  jana walishiriki katika mbio za Taifa za Nyika zilizofanyika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro,huku washindi waliotawa mbio hizo wakitoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Mashindano hayo ambayo yalifanyiika katika uwanja wa moshi wa Gofu yalishirikisha Washirikisha wapatao 100 kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha, Manyara, Singida, Mara, Zanzibar, mbeya, Dar es salaam na Kilimanjaro,ambapo Kilimanjaro iliweza kutoa mshindi wa Kilomita 12.

Pia wanariadha wengine waliofanya vizuri kwenye mbio hizo wanatoka Mikoa ya Arusha ambao walitawala kwa kuchukua nafasi za juu katika mbio za kilomita 12, 8 na 6,ambapo jumla ya wakimbia 100 walishiriki.

Kwenye Mbio za Kilimita 6  za wanawake wenye umri chini ya miaka 20 washindi walikuwa ni Anjeline Irene 21:19;57, Selina Amosi 21:31:86, Fadhila Salum wote kutoka Arusha mbio za km 8 wanawake Jaeldine Sakilu (JWTZ-Arusha) 27:00:34, Zakia Mrisho  (Arusha) 27:24:58 na Catherine Lange (Manyara) 28:12:91.

Kwa upande wa wanaume kwa mbio za kilomita 8 washindi walikuwa ni  Dotto Ikangaa 23:53:95 JWTZ-Arusha, Joseph Theophil Mbulu 23:56:41 na Mohammed Ally 24:13:54 JWTZ- Arusha huku mbio za km 12 wanaume akichukua Dickson Marwa 36:34:52 kutoka Holili-Kilimanjaro.

Rais wa Shirikisho la Riadha Taifa, (RT), Anthony Mtaka alisema kuwa madhumuni ya mbio hizo, ni kuandaa kikosi kitakacho iwakilisha Taifa katika mbio za Nyika za dunia zitakazofanyika Machi 24, nchini Poland pamoja na kuibua vipaji vya riadha nchini.

Alisema kuwa ili kuweza kufanya vizuri katika mashindano ya dunia ni lazima kuwepo na maandalizi mazuri kwa kuweka wachezaji kambini,kwa kuwapa mazoezi na majiribio ndipo Watanzania wataweza kufanya vizuri katika mbio zinazofanyika kimataifa.

 Anthony alisema kuwa chanagamoto kubwa katika kuandaa mashindano ipo katika kuwapata wadhamini kwani zoezi la kuwandaa wachezaji wataoshiriki katika mashindano inahitaji garama kubwa.

“Kwa mfano suala la timu ya taifa ya Riadha kushindwa kufanya vizuri RT, hatupaswi kulalamikiwa kwani sisi kama RT hatuna timu, na majukumu yetu ni kusimamia timu na kuhakikisha kuwa timu inapata huduma zote kabla ya mashindano”Alisema.

Mgeni Rasmi kwenye riadha za Nyika alikuwa ni Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, Matanga Mbushi,kwa muda mrefu nchi yetu ya Tanzania kuwa washiriki katika mashindano mbalimbali badala ya kwua washindi hivyo wanariadha wanahitaji kufanya mabadiliko.

“Mimi chuo changu kimeandaa wanamichezo wapo 12,tunataka wawe mfano na baadae ikiwezekana tutawachukua wengine ili kuweza kuleta mabadiliko kwenye mchezo wa riadha”Alisema Mbushi.

Mmoja wa mwanariadha aliyeshiriki mbio za jana, Dickson Marwa, aliyeshinda mbio za km 12 mwanaume, alisema kuwa endapo kukiwepo na maandalizi mazuri wanariadha wataweza kufanya vizuri katika mashindano ya riadha ambapo yeye alisema yupo tayari kuiwakilisha nchi katika mbio za Poland.

Hata hivyo katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na mchuano mkali mshindi wa kwanza alipokea zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha taslimu.
 

Wednesday, March 6, 2013

COMESA, EAC WATOA RIPOTI YA AWALI.


  Wafuasi wa muungano wa CORD.
Wakati huo huo, tume ya wangalizi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na mataifa wanachama wa COMESA imetoa ripoti yao ya mwanzo kuhusiana na zoezi nzima la uchaguzi.

Kiongozi wa ujumbe huo, Abdulrahman Kinana kutoka Tanzania, amesema kuwa uchaguzi wa Kenya uliendeshwa kwa njia ya kidemokrasia na kuisifu tume ya uchaguzi kwa kutekeleza wajibu muhimu kulingana na katiba.

Hadi kufikia majira ya jioni, kura bado zilikuwa zikihesabiwa na matokeo kamili yanatarajiwa wakati wowote. 

Kwa mujibu wa katiba, tume inayo nafasi ya kutoa matokeo yote katika kipindi cha wiki nzima tokea siku ya kupiga kura.
Mwandishi: Reuben Kyama/DW Nairobi

MATOKEO YA UCHAGUZI WA KENYA 2013,CORD WAWALAMIKA

Kenyan Prime Minister Raila Odinga (L), Vice President Kalonzo Musyoka (C) and Trade Minister Moses Wetangula gesture at supporters in Nairobi on December 4, 2012 after agreeing to form a powerful alliance as running mates in presidential elections due in March 2013. The former rivals along with leaders of 10 other smaller parties, signed an agreement in front of thousands of supporters to form the Coalition for Reform and Democracy (CORD) party. Odinga is widely tipped to be the presidential candidate with Musyoka as his deputy, although no formal announcement was made. AFP PHOTO / TONY KARUMBA (Photo credit should read TONY KARUMBA/AFP/Getty Images)


Viongozi wa muungano CORD wamelalamikia namna matokeo ya kura yanavyotolewa, huku waangalizi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na wa Soko la Pamoja la COMESA wakitoa ripoti zao za awali.
Huku matokeo ya uchaguzi yakizidi kutiririka kutoka katika kituo cha kuhesabia kura jijini Nairobi, viongozi wa muungano wa CORD wamelalamika kwamba utaratibu unaotumiwa kutangaza matokeo hayo unatia shaka.
Kulingana na taarifa iliyosomwa na Kalonzo Musyoka, mgombea mwenza wa Raila Odinga, viongozi kutoka vyama vinavyounda muungano huo wameowaomba wafuasi wao kuwa watulivu wakati matokeo yote yanavyosubiriwa.
Kalonzo alisema kuwa bado wana uhakika wa kushinda katika uchaguzi na akaongeza kuwa endapo watashindwa wako tayari kusalimu amri.
Kauli ya CORD yanakuja wakati ambapo kinara wa mrengo wa Jubilee, Uhuru Kenyatta, anaonekana kuongoza katika matokeo ya awali yaliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Hata hivyo, Kenyatta na mpinzani wake wa karibu Odinga wanamenyana vilivyo huku kila mmoja wao akiwa ametimiza zaidi ya kura milioni mbili.
Katika mkutano na waandishi wa habari, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Isaack Hassan amewaomba wanasiasa wawe watulivu wakati huu wa kuhesabiwa kwa kura na akakiri kuwa kulikuwa na hitilafu Fulani za kimitambo ambazo zilichangia kucheleweshwa kwa matokeo.
Hata hivyo, mgombea mwenza wa muungano wa Jubilee, William Ruto, alisiifu IEBC kwa kuendeleza shughuli za uchaguzi kwa utaratibu unaofaa. Ruto amewashukuru Wakenya kwa kujitokeza kwa wingi ili kupiga kura siku ya Jumatatu.

TAKUKURU MBEYA WAMNASA MWALIMU AKIPOKEA RUSHWA KUTOKA KWA MWANAFUNZI YA SHILINGI 200


MWALIMU Faustin wa shule ya sekondari ya Forest iliyopo Jijini Mbeya amejikuta akitiwa mbaroni baada ya muda mrefu kuwaomba na kupokea rushwa ya Sh.200 kutoka kwa wanafunzi wake wanaochelewa na kuvaa viatu ambavyo havina kamba.
Arobaii za mwalimu huyo zilitimia jana baada ya maafisa wa Takukuru mkoa wa Mbeya kuinyaka issue hiyo na kutege mtego uliofanikisha kumnasa mwalimu huyo kinara wa rushwa shuleni hapo.
Mwalimu huyo alikutwa na maafisa wa Takukuru akiwa tayari amekusanya kiasi cha Sh.64,000 huku msaidizi wa ulaji rushwa hiyo Mwalimu Mwasote akifanikiwa kuwazidi mbio maafisa wa Takukuru kisha kutokomea kusikojulikana.
Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na kikosi kazi cha mtandao wa kalulunga.com kilipofika shuleni hapo walisema kuwa wamefurahishwa na Takukuru kumkamata mwalimu huyo mwenye urefu usiozidi futi tno na nusu huku akiwa na kitambi.
Walisema kuwa mwalimu huyo lich ya kuwatoza Sh.200 wanafunzi wanaochelewa au kuwa na makosa mbalimbali shuleni hapo, pia alikuwa akiwavua viatu wanafunzi ambao wazazi wao hawana uwezo wa kununua viatu vya kamba na kuwatoza kati ya Sh.500-2000 endapo wanafunzi wakishindwa kumpa rushwa hiyo alikuwa akivipeleka viatu vyao kwenye matanuru ya matofali ili kuwashia moto.
Sanjari na hayo mwalimu Faustine, anatuhumiwa na wanafunzi kuwatesa kwa kuwainamisha miguu juu kichwa chini bila kujali jinsia zao wala mavazi na ambao wanashindwa anawaambia watoe Sh.200 na kwamba ofisi ya walimu inaitwa Gwantanamo!
Shule hiyo ni ile ambayo Mkuu wa shule ambaye ni mwanamke aliwahi kuwaambia wazazi kuwa watoto wao wa kike wote ni wake za watu baada ya kuwapima na kutofanikia kumkuta hata mmoja na usichana wake.

BAJAJI ZA WAJAWAZITO ZASHINDWA KUPUNGUZA KERO KWA WAKINA MAMA WAJAWAZITO


Kulia ni mganga mkuu wa kituo cha afya cha Ikizu Dk. Abahehe Kanora katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara, akionesha bajaji ya Kikwete ikiwa imetolewa kitanda cha kubeba mjamzito, kutokana na kushindwa kukitumia kwa ubovu wa barabara na haikati kona upande wa kushoto.

Wilaya ya Bunda ina kata 28 kati ya hizo kata 4 tu ndio zina vituo vya afya kama Ikizu, Manyamanya na Kasuguti vituo hivyo vina Bajaji ya Kikwete lakini hazitumiki kwa ubovu wa barabara, baada ya kutoa kitanda hicho wanatumia pikipiki kwenda kuchukua dawa wilayani.habari na Kalulunga Blog

JUKWAA LA WAHARIRI LATOA TAMKO KUHUSU KUVAMIWA KWA MWENYEKITI WA JUKWAA HILO ABSALOM KIBANDA


   
 

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na Dimba, Absalom Kibanda amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake wakati akiingia nyumbani kwake Mbezi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kibanda alivamia majira ya saa sita usiku wa kumkia leo, akitokea kwenye majukumu yake ya kila siku. 

Inadaiwa kuwa alichomolewa kwene gari, akapigwa na vitu vyenye ncha kali kichwani, ametobolewa jicho lake la kushoto pamoja na kunyofolewa kucha na baadhi ya vidole na hatimaye kutupwa umbali kidogo ya nyumbani kwake.

Baada ya hapo wasamalia wema walijitokeza na kumkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambako alipokelewa vizuri na madaktari na kumpatia tiba ya awali na baadaye kumhamishia Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).

Watu waliomfanyia madhara hayo, hawakuweza kuchukua kitu chochote kwenye gari ambapo kulikuwemo Laptop, simu na nyaraka zingine.

Amepelekwa Afrika kusini kwa ajili ya matibabu zaidi.