DICKSON MARWA AKIMALIZA
WANARIADHA WA KILOMETA 12 KATUIKA MBIO ZA NYIKA
WANARIADHA WA KILOMETA 12 WALIPOANZA KUTIMUA MBIO
WANARIADHA kutoka mikoa mbalimbali
nchini jana walishiriki katika mbio za
Taifa za Nyika zilizofanyika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro,huku washindi
waliotawa mbio hizo wakitoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Mashindano hayo ambayo
yalifanyiika katika uwanja wa moshi wa Gofu yalishirikisha Washirikisha wapatao
100 kutoka mikoa ya Mwanza, Arusha, Manyara, Singida, Mara, Zanzibar, mbeya,
Dar es salaam na Kilimanjaro,ambapo Kilimanjaro iliweza kutoa mshindi wa
Kilomita 12.
Pia wanariadha wengine
waliofanya vizuri kwenye mbio hizo wanatoka Mikoa ya Arusha ambao walitawala kwa
kuchukua nafasi za juu katika mbio za kilomita 12, 8 na 6,ambapo jumla ya
wakimbia 100 walishiriki.
Kwenye
Mbio za Kilimita 6 za wanawake wenye umri chini ya
miaka 20 washindi walikuwa ni Anjeline Irene 21:19;57, Selina Amosi 21:31:86,
Fadhila Salum wote kutoka Arusha mbio za km 8 wanawake Jaeldine Sakilu
(JWTZ-Arusha) 27:00:34, Zakia Mrisho (Arusha) 27:24:58 na Catherine Lange
(Manyara) 28:12:91.
Kwa upande wa wanaume kwa mbio
za kilomita 8 washindi walikuwa ni Dotto
Ikangaa 23:53:95 JWTZ-Arusha, Joseph Theophil Mbulu 23:56:41 na Mohammed Ally
24:13:54 JWTZ- Arusha huku mbio za km 12 wanaume akichukua Dickson Marwa
36:34:52 kutoka Holili-Kilimanjaro.
Rais wa Shirikisho la Riadha
Taifa, (RT), Anthony Mtaka alisema kuwa madhumuni ya mbio hizo, ni kuandaa
kikosi kitakacho iwakilisha Taifa katika mbio za Nyika za dunia zitakazofanyika
Machi 24, nchini Poland pamoja na kuibua vipaji vya riadha nchini.
Alisema kuwa ili kuweza
kufanya vizuri katika mashindano ya dunia ni lazima kuwepo na maandalizi mazuri
kwa kuweka wachezaji kambini,kwa kuwapa mazoezi na majiribio ndipo Watanzania
wataweza kufanya vizuri katika mbio zinazofanyika kimataifa.
Anthony alisema kuwa chanagamoto kubwa katika kuandaa
mashindano ipo katika kuwapata wadhamini kwani zoezi la kuwandaa wachezaji
wataoshiriki katika mashindano inahitaji garama kubwa.
“Kwa mfano suala la timu ya
taifa ya Riadha kushindwa kufanya vizuri RT, hatupaswi kulalamikiwa kwani sisi
kama RT hatuna timu, na majukumu yetu ni kusimamia timu na kuhakikisha kuwa
timu inapata huduma zote kabla ya mashindano”Alisema.
Mgeni
Rasmi kwenye riadha za Nyika alikuwa ni Mkuu wa Chuo cha Polisi
Moshi, Matanga
Mbushi,kwa muda mrefu nchi yetu ya Tanzania kuwa washiriki katika mashindano
mbalimbali badala ya kwua washindi hivyo wanariadha wanahitaji kufanya
mabadiliko.
“Mimi
chuo changu kimeandaa wanamichezo wapo 12,tunataka wawe mfano na baadae
ikiwezekana tutawachukua wengine ili kuweza kuleta mabadiliko kwenye mchezo wa
riadha”Alisema Mbushi.
Mmoja wa mwanariadha aliyeshiriki
mbio za jana, Dickson Marwa, aliyeshinda mbio za km 12 mwanaume, alisema kuwa
endapo kukiwepo na maandalizi mazuri wanariadha wataweza kufanya vizuri katika
mashindano ya riadha ambapo yeye alisema yupo tayari kuiwakilisha nchi katika
mbio za Poland.
Hata hivyo katika mashindano
hayo ambayo yalikuwa na mchuano mkali mshindi wa kwanza alipokea zawadi mbalimbali
ikiwa ni pamoja na fedha taslimu.
No comments:
Post a Comment