Wafuasi wa muungano wa CORD.
Wakati huo huo, tume ya wangalizi kutoka Jumuiya ya Afrika
Mashariki na mataifa wanachama wa COMESA imetoa ripoti yao ya mwanzo
kuhusiana na zoezi nzima la uchaguzi.
Kiongozi wa ujumbe huo, Abdulrahman Kinana kutoka Tanzania, amesema kuwa
uchaguzi wa Kenya uliendeshwa kwa njia ya kidemokrasia na kuisifu tume
ya uchaguzi kwa kutekeleza wajibu muhimu kulingana na katiba.
Hadi kufikia majira ya jioni, kura bado zilikuwa zikihesabiwa na matokeo
kamili yanatarajiwa wakati wowote.
Kwa mujibu wa katiba, tume inayo
nafasi ya kutoa matokeo yote katika kipindi cha wiki nzima tokea siku ya
kupiga kura.
Mwandishi: Reuben Kyama/DW Nairobi
No comments:
Post a Comment