Sunday, March 10, 2013

MACHANGU AWAPIGA JEKI WANAWAKE KILIMANJARO.

 Picha namba 62:Mbunge wa Viti maalumu Mkoani Kilimanjaro Betty Machangu akizungumza na wanawake wa Kata ya Uru Kusini,Wilaya ya Moshi Vijijini wakati alipofika kutekeleza ahadi yake waliyokuwa wameomba kwa Mbunge huo ya kuwaanzishia mradi wa Nguruwe.
 Mbunge wa Viti Maalumu Betty Machangu mkoani Kilimanjaro(CCM)akikabidhi Mradi wa nguruwe kwa wanawake wa umoja wa wanawake UWT Kata za Uru Kusini na Uru Mashariki.kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.,Picha na Rodrick Mushi.
Mbunge wa Viti Maalumu Betty Machangu mkoani Kilimanjaro(CCM)(katikati)akizungumza na wanawake wa Kata ya Mbokomu baada ya kuwakabidhi mradi wa nguruwe pamoja na mashine ya kuangulia vifaranga likiwa ni ombi la wanawake wa Kata hiyo baada ya Mbunge kufanya ziara kwenye Kata hiyo.Picha na Rodrick Mushi.


Mbunge wa Viti Maalumu Betty Machangu mkoani Kilimanjaro(CCM) amesema kuwa ili wanawake kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na hali ya kuwa  tegemezi ni vema wakajiunga kwenye vikundi ili iwe rahisi kuweza kupatiwa mikopo katika taasisi mbalimbali za fedha ili kuanzisha miradi.

Alisema kuwa kuna taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitoa mikopo kwa bei nafuu,ikiwemo Vicoba pamoja Saccos hivyo wanawake wakijiunga kwenye vikundi itakuwa rahisi kupatiwa fedha na kujiingiza kwenye shughuli za ujasiriamali.

Machangu aliyasema hayo wakati akikabidhi miradi mbalimbali ikiwemo ya nguruwe pamoja na mashine za kuangulia vifaranga kwa wanawake wa Umoja wa Wanawake CCM kwenye Kata za Uru Kusini,Uru Mashariki na Kata ya Mbokomu kutoka Wilaya ya Moshi Vijijini.

Hata hivyo alisema kuwa utoaji wa miradi hiyo ameitoa kwenye Kata hiyo baada ya ziara yake kwenye Wilaya Mbalimbali za Mkoa wa Kilimanajaro na kusikiliza vipaumbele vyao walivyotoa kwake ili kuweza kuanzisha miradi na kujikwamua na umaskini.

“Nilifanya ziara yangu kila tarafa na kila Wilaya,hivyo niliwaambia wanawake wanipe vipaumbele vyao ili niweza kuwasaidai,ndio wanawake niliowakabidhi msaada huu leo wakaniomba miradi ya nguruwe na kuku,nab ado kuna Wilaya nyingine wameomba miradi kama ya mbuzi”Alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Wilaya ya moshi Vijijini Grace mzava alisema kuwa njia pekee ya mwanamke kuweza kujikwamua na hali ngumu ya maisha ni kujishighulisha katika kazi mbalimbali za Ujasiriamali.

Alisema kuwa wapo wanawake ambao wamekuwa najitihada za kujiingiza na kubuni miradi lakini changamoto kubwa imekuwa ni mtaji,hivyo wengi kujikuta wakishindwa kufikia malengo hivyo wanawake wakisaidia miradi idadi ya wanawake tegemezi itapungua.

No comments:

Post a Comment