Friday, December 21, 2012

BREAKING NEWS..ALIYEKUWA MBUNGE WA ARUSGA GODBLESS LEMA AREJESHEWA UBUNGE WAKE..





Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema leo ameshinda rufaa ya kesi yake. Mahakama imejiridhisha kuwa madai ya udhalilishaji hayakuathiri uchaguzi wala mlalamikaji (CCM). Tangu sasa Lema ni mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema. CCM wameamriwa kulipa gharama za kesi hii tangu ilipofunguliwa mpaka ilipoishia!


MATAMKO MBALIMBALI AMBAYO ALIKWISHATOA LEMA WAKATI ALIPOVULIWA UBUNGE WAKE..MUNGU AMESIKIA KILIO CHAKO..
 
IKULU ILIINGILIA KESI YA UCHAGUZI. – GODBLESS LEMA.
“ Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)
“Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge”.
Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .
Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.
Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni “Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu “ umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako , hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa , Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar , mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .
Mh Rais , Mama Theresa , Nelson Mandela , Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao , sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu , nahitaji dhamira safi , nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini , nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya , ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta , magorofa , magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki ,Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo, pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi , Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe , hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho , nitakufa siku moja ambayo siijui , napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana , lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki , kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana , unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako , niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.
Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.
Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .
Mh Rais “Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri” Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .
“ ONLY TIME WILL TELL”.
GODBLESS .J. LEMA.

FAMILIA YA WALEMAVU WATANO YAOMBA MSAADA.


Watoto wa tano wa familia moja ambao ni walemavu wa viungo eneo la chome Wilayani Sama wakiwa kwenye picha ya pamoja.


Familia ya watoto watano wenye ulemavu Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wameomba jamii kujitokeza kusaidia kutokana na  ulemavu wa viongo ambao umekuwa ukiwakabili kwa muda mrefu sasa, na kuwafanya kuishi katika hali ngumu kimaisha.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mama wa watoto hao,Nirenjigwa Joseph alisema kuwa ana watoto nane lakini kati yao watoto watano ni walemavu na mume wake  Amini Joseph alifariki tangu mwaka 1992 na baada ya hapo yeye ndo amekuwa akilelea familia hiyo.

Watoto hao ni Joseph  Amini( 38),Nafikahedi( 33) ,Wediel(30) Gadison (28) na Julius(25)wote ni walemavu wa viongo ambao wanatembea kwa kutambaa  na wanahitaji kuwa na muangalizi wakati wote kwa hakuna wanaloweza kufanya.

Watoto walizaliwa wakiwa wazima lakini tatizo likaanzia kwenye kutambaa wakashindwa kusimama na tulijaribu kupeleka hospitali na kuambiwa kuwa haitawezekana tena .

Kwa sasa ukiwaangalia watoto hao tayari wameshakuwa wakubwa kabisa na changamoto kubwa ni kwamba familia haiwezi kuwaacha kukaa pekee yao kwani wapo pia wakike na jamii pia imekuwa na makusudio mabaya kwa wale wenye imani potofu juu yao au wanaopewa maagizo ya imani za kishirikina.

“Baada ya mume wangu kufariki nilikuwa nailelea familia mwenyewe na nilikuwa najishughulisha na kilimo siku na kazi nyingine ya kufanya,lakini nashukuru Mungu pia wapo watu waliojitoa kwa moyo lakini bado mahitaji ya kuwatunza ni makubwa sana”Alisema mama huyo.

Mmoja watoto wa familia hiyo ambaye ni kati ya watoto watatu ambao hawana tatizo la ulemavu ambaye ni Mwalimu Chediel Amini (28)alisema kuwa wapo wafadhili ambao  wamejitokeza kuwasaidia lakini bado tatizo ni kubwa kwani nyumba aliyojenga bado inahitaji kumaliziwa.

Kikundi cha utukufu kwa Mungu kupitia kwa Mwenyekiti wake Samweli Njau  baada ya kutembelea familia hiyo walisema kuwa watasaidia kufunga huduma ya maji pamoja na tenki la kuhifadhia  maji ili kusaidia kuondoa tatizo la maji lilipo kwenye familia hiyo.

Baada ya kutembelea familia hiyo waliona kuwa jamii hiyo inahitaji kusaidiwa kwani wanapoishi walemavu hao hakuna kivuli na wamekuwa wakitambaa kwenye jua na kusumbuliwa na tatizo la funza hivyo kusaidia kuweka baraza kwenye nyumba hiyo,ambapo wanasema msaada wao hautaishia tu hapo bali wataendelea kuhamasisha na jamii nyingine.

Chediel alisema kuwa anaomba watu wenye mapenzi mema kuweza kujitokeza kusaidia familia hiyo kwa chochote watakachokuwa nacho ili kupunguza ugumu wa maisha ambao wamekuwa wakiishi kutokana na familia kutegemea kilimo kuwalea watoto hao.

Kwa mawasiliano  ya mmoja wa mtoto wa familia hiyo Chediel Amini ambaye ndiye aliyebeba jukumu la kusaidia ndugu zake wenye ulemavu, simu 0654118385.

Thursday, December 20, 2012

UJENZI WA SOKO LA LOKOLOVO MWAROBAINI WA BIASHARA ZA MAGENDO KUPITIA NJIA ZA PANYA KILIMANJARO.

 

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Katikati Leonidas Gama,akizungumza na viongozi wa kamati ya Usalama Wilaya ya Rombo,aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo,Peter Toima baada ya kukamatwa kwa gari ambalo lilikuwa likisafirisha mazao aina ya mahindi kwenye Kenye kwa kupitia njia za Panya.
 Rodrick Mushi,Moshi
MWAROBAINI wa tatizo la usafirishaji wa mazao ya biashara na chakula  nchini umepatikana baada ya Serikali kupitisha mradi  wa ujenzi wa soko la kimataifa la bidhaa za mazao .
Ujenzi wa Soko hilo unatarajiwa kufanyika katika eneo la Himo Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanajaro,ambalo linakadiriwa kugarimu zaidi ya shilingi billion 5,mpaka kukamilika kwake.
Mpango wa ujenzi huo umekuja baada ya kuwepo kwa wimbi kubwa la usafirishaji wa mazao ya bidhaa kwenda nje ya nchi kwa kupitia njia za panya.
Hatua za kwanza baada ya kupatikana kwa eneo la ujenzi wa soko hilo,tayari Serikali Mkoani Kilimanjaro imeshatiliana saini na benki ya Uwekezaji (TIB) kupitia kwa Meneja wake Allan Magoma kwa ajili ya kupatiwa fedha za ujenzi wa soko hilo la kimataifa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama anasema kuwa ujenzi wa soko hilo ulikuja kwenye kikao cha Mkoa kilichofanyika mwezi wa tatu mwaka huu,baada kilio cha wafanyabiashara pamoja na kushamiri kwa biashara ya magendo.
Lakini anasema kuwa jitihada za Serikali siyo  kujenga soko la bidhaa za mazao bali pia kwenye mkataba walioingia na benki ya uwekezaji walipewa kiasi cha shilingi billion 10  kwa ajili ya ujenzi wa soko la mbogamboga eneo la njia panda.
Anasema kuwa ujenzi wa soko hilo unaweza kuchukua zaidi ya miaka miwili endapo shughuli za ujenzi na mkandarasi atakayeshinda tenda ya ujenzi wa soko hilo litafanya kwa wakati.
“Mwazo soko hilo lilikuwa lijengwe eneo la njia panda lakini eneo likawa dogo hivyo kulazinmika kulitumia kujenga soko la mbogamboga ukubwa wake ni hekari 9 na kwenda na eneo la Lokolova  lina ukubwa wa hekari 140”Alisema Gama.
Eneo ambalo soko hilo linajengwa linajulikana kama Lokolova ambalo lilikuwa eneo la ushirika wa wafugaji,hivyo Serikali kufanya mazungumzo nao kwa ajili kujenga soko eneo hilo.
Gama anasema Ugumu wa ujenzi wa soko hilo ulikuwa ni jinsi ya kupata fedha kwa ajili ya ujenzi,lakini baada ya hatua za awali za jinsi soko hilo linatakiwa kukamilika na kupitishwa imekuwa rahisi kuingia mkataba na benki ya uwekezaji.
“Kinachotakiwa  hivi sasa ni kutengenezwa kwa  garama halisi ya ujenzi wa soko (bill of quantity)ambapo baada ya kujua garama halisi itakayotumika  ni kutangaza tenda kwa ajili ya kumpata mkandarasi.”Alisema Gama.
Utaratibu wa soko hilo utakuwa unahusisha wafanyabishara kutoka mikoa yote nchini  kununua bidhaa za mazao sehemu mbalimbali na kuleta kwenye soko hilo la lokolova kwa ajili ya kuwauzia wateja kutoa ndani na nje ya nchi.
Mazao ya bidhaa za nafaka ambayo yatakuwa yanauzwa  kwenye soko la Lokolova ni pamoja na mahindi,mpunga mchele,mahindi maharage,Ulezi,uwele na mazao mengine ambapo yamekuwa yakisafirishwa kwa wingi kwa njia za panya kwenda nje ya nchi.
Ujenzi wa soko hilo utatoa fursa kwa wafanyabishara kutoka nchi za Afrika Mashariki na nyinginezo kuingia nchini hadi kwenye soko hilo na kununua bidhaa mbalimbali za mazao ambayo yanapatikana nchini.
Faida za ujenzi wa soko la lokolova.
Usafirishaji wa bidhaa za mazao kwenda nje ya nchi kwa njia ya panya ulikuwa ukikosesha Serikali mapato ambayo yangetokana na kodi ambayo ingetakiwa kutozwa kwenye mazao yanayoenda nje.
Lakini mbali na kuikosesha Serikali mapato pia ilikuwa inachangia kukosekana kwa takwimu sahihi ya mazao ambayo yameuzwa nje ya nchi kutokana na kutokuwepo kwa rekodi ya mazao yanayotoroshwa kwa njia za panya.
Hili la kukosekana kwa Takwimu, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Christopher Chiza anakiri kuwa Serikali imekuwa ikikosa takwimu muhimu hususani za Mazao yaliyouzwa nje,kutokana na biashara ya magendo.
Wakati akiwa ziarani Mkoani hapa alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikichangia pia baadhi ya bidhaa na mazao yanayozalishwa nchini kuonekana nchi jirani ndio zinazalisha zaidi ilihali zinatoka nchini.
Serikali  kuzuia biashara ya usafirisha wa bidhaa za mazao bila kuweka utaaratibu wa wananchi kufanya biashara ilitoa mianya kwa mamlaka zilizokuwa zimepewa jukumu la kuzuia zoezi hilo ikiwemo polisi na mamlaka ya mapato (TRA) kulalamikiwa kuwepo kwa vitendo vya  kupokea rushwa kwa wafanyabiashara wa mazao.
Hali ya usafirishaji wa mazao ya bidhaa nje ya nchi yalikuwa yakiongezeka kutokana na mahitaji ya mazao hayo,pamoja na bei ambayo ilikuwa inatoa faida kubwa kwa wafanyabisahara.
Mbali na wafanyabiashara pia soko hili litatoa fursa kwa wakulima wa mazao ya chakula kuuza mazao yao moja kwa moja katika soko hili,na kuepuka kulanguliwa na wafanyabiashara.
Mmoja wa wakulima wa Mahindi,John Malisa,anasema kuwa Serikali imekuwa ikiwaonea wakulima kwa kuwapangia masoko ya kuuza mazao yao,ikiwemo la kuuzuiwa kuuza nje ya nchi.
Lakini kutokana na ujenzi wa soko hilo anasema kuwa atatumia fursa hiyo kufikisha mazao yake kwenye soko hilo kutokana na kuwa na wateja kutoka sehemu mbalimbali nje na ndani hivyo kupata bei nzuri.
Wakati Serikali ikitangaza kuruhusu biashara ya usafirishaji wa mazao nje ya nchi tayari ilitenga soko la muda eneo la Himo ambalo wafanyabiashara  kutoka nchi za Afrika Mashariki kuiingia nchini na kununua mazao kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
Utaratibu huo ulianza mwezi marchi mwaka huu,hadi mwezi  julai ambapo hali hiyo imesaidia Serikali kujua takwimu ya mazao yaliyouzwa nje kwa kipindi hicho kifupi tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa vigumu kupata takwimu kutokana na mazao kutoroshwa kwa njia za panya.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama anasema kuwa kwa kipindi cha mwezi marchi hadi julai mwaka huu kiasi cha mahindi yaliyouzwa nje kwa wafanyabiashara kuingia nchini ni zaidi ya tani 26,588.
Lakini kwa upande wa mazao mengine kama Mikunde maharage zaidi ya tani tani 131 zilizwa nje na kusaidia kupatikana kwa mapato kwenye vijiji halmashauri za Wilaya husika ambapo biashara hiyo ilikuwa ikiufanyika.
Kwa Kijiji cha himo pekee ambapo ndipo soko hilo la muda lilipo kiliweza kupata mapato ya zaidi ya shilingi million 25,Huku Wilaya ya Rombo ikipata shilingi million 21,171,000 tangu kuanza kwa soko hilo la muda mfupi.
Halmasahuri ya Wilaya ya moshi vijijina nayo iliweza kupata mapato ya shilingi million 80 ,huku kukiwepo na zaidi ya shilingi 48,000,000 zilizopatikana kutokana na tozo ya magari yalikuwa yanatoka nje ya nchi kuingia nchini kununua mazao.
Hivyo kwa takwimu hiyo utaona ni jinsi gani Serikali ilikuwa ikikosa mapato kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu na jinsi ya kuweza kutoza kodi,pamoja na kushamiri kwa biashara ya kusafirisha mazao kwa njia za panya.
Wafanyabiashara mbalimbali wanaofanya biashara ya mazao wanasema kuwa ujenzi wa soko hilo utakuwa mkombozi kwao,kwani hapo awali walikuwa wakikamatiwa bidhaa zao na wakati mwingine kutaifishwa wakiwa nchini.
Juma Hamisi anasema kuwa ujenzi wa soko hilo ni mwisho wa uonevu kwa wafanyabiashara kwani soko hilo litatoa fursa ya kufanya biashara kwa uhuru tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Lakini pia uwepo wa soko utatoa ajira kwa vijana na wananchi wengine kama lilivyotoa soko la muda pamoja na wajasiriamali wengine kama mama ntilie,kujipatia kipato kupitia wafanyabiashara na wegeni wengine watakaoukuwa waningia nchini.
Waziri wa Afrika Mashariki Samweli Sitta anasema kuwa ujenzi wa soko hilo ni moja wapo ya njia za kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya nchi ambazo zilizopo kwenye soko la pamoja la Afrika Mashariki.
Anasema kuwa soko hilo litatoa chachu kwa wageni na majirani tuliopakana nao kuingia nchi kwa utaratibu uliowekwa na kuwezesha nchi kupata mapato pamoja na kumaliza biashara ya magendo.
Mwanzoni mwa mwaka huu kwenye mwezi Januari hadi marchi kulikuwepo na wimbi kubwa la usafirishaji wa mazao ya nafaka kwenda nje ya nchi,licha ya Serikali kupiga marufuku usafirishaji wa bidhaa hizo za mazao nje ya nchi.
Mwisho 

MAKAMU WA RAISI DK BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Watumishi wa Umma, zilizopo eneo la Ada Estate, jijini Dar es Salaam, leo Desemba 20, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiri uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Watumishi wa Umma, zilizopo eneo la Ada Estate, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Elius Mwakalinga, wakati akitembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Watumishi wa Umma, zilizopo eneo la Ada Estate, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa jengo hilo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo na kuonyeshwa Ramani ya Jengo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Elius Mwakalinga, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Watumishi wa Umma, zilizopo eneo la Ada Estate, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya sanamu la Kinyago cha Umoja, kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Elius Mwakalinga (kulia) na Mwenyekiti wake, Edward Ngwalle, (wa pili kulia) wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Watumishi wa Umma, zilizopo eneo la Ada Estate, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika Picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TBA, baada ya hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakati akiondoka eneo la Ada Estate, baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Watumishi wa Umma, zilizopo eneo la Ada Estate, jijini Dar es Salaam, leo.

MAMA SALMA NA HUDUMA ZA AFYA KWA WAJASIRIAMALI.

 

 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, (WAMA), Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma za Bima ya Afya kwa vikundi vya SACCOS vya UVIMA (Umoja wa vikundi vya WAMA Tawi la Majohe lililoko wilayani Ilala) na Salma Kikwete SACCOS kilichoko Mkuranga. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012 na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Afya Mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi (wa kwanza kushoto). Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya Mheshimiwa Deogratias Ntukamazina (katikati) na kulia ni Afisa wa WAMA ndugu Tabu Likoko akifuatiwa na Grace Michael, Afisa Habari wa Bima ya Afya.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete na viongozi wengine wakiangalia moja ya kadi ya mwanachama wa bima ya Afya mara tu baada ya kuzindua rasmi huduma ya bima hiyo kwa wajasiriamali wa UVIMA na Salma Kikwete SACCOS kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012.  Wengine katika picha kutoka kushoto kwenda kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa Dr. Husein Mwinyi, Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mheshimiwa Deogratias Ntukamazina na Mkurugenzi wa Mfuko huo Ndugu Emmanuel Humba.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akikabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa Bibi Tatu Ngao, Mwenyekiti wa UVIMA mara tu baada ya kuzindua rasmi mpango huo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012.

 
Waziri wa Afya Mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi akimpatia tuzo ya Shujaa wa mfuko wa Bima ya Afya kwa mwaka 2012 Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa WAMA kwa jitihada zake kubwa za kumkomboa mwanamke kiuchumi na kijamii na pia katika kupigania afya kwa wote na hasa makundi maalum katika jamii. Tuzo hiyo ilitolewa baada ya uzinduzi wa huduma ya Bima ya Afya kwa vikundi vya wajasiriamali wa UVIMA na Salma Kikwete SACCOS uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012.

(PICHA NA JOHN LUKUWI – MAELEZO -DAR ES SALAAM)

JK ALIPOKUTANA NA MMILIKI WA KLABU YA SUNDERLAND.

 

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short (kushoto kwa Rais), Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband (kulia kwake), Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii bada y mkutano na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa mmiliki na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan wakiangalia  bada ya  mkutano wa  na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short huku Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband na Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan Ikulu jijijni Dar es salam leo.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Mwenyekiti wa Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Sunderland, Bw. Ellis Short, Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Bw. David Milliband, Mkurugenzi wa Masoko wa klabu hiyo Bw. John Farnan, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kagasheki, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr Fenella Mukangara, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim pamoja na maafisa wa Bodi ya Utalii baada ya mkutano na Rais Ikulu jijijni Dar es salam leo.                              
                               PICHA NA IKULU

POLISI WANAODAIWA KUGAWA FEDHA ZILIZOPORWA WAPEWA SIKU SABA KUJISALIMISHA.

 

JESHI la Polisi limetoa siku saba kwa baadhi ya askari kuzisalimisha  fedha zipatazo sh milioni 150 wanazodaiwa kuiba, ambazo zilizoporwa na majambazi Mtaa wa Mahiwa na Livingston jijini Dar es Salaam juzi.

 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova, alisema kutokana na tuhuma hizo jeshi hilo limeunda Jopo la wapelelezi ili kujua ukweli wa madai hayo.

Alisema Jopo hilo litaundwa na watu watano, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum, Ahmed Msangi, atakayehakikisha kwamba muda mfupi inavyowezekana, ukweli upatikane ili wananchi wajulishwe matokeo.

Kamanda Kova alisema jeshi hilo lina mfumo wake wa kuchunguza askari wake inapotokea amejihusisha katika matukio yanayokwenda kinyume na maadili ya kazi yake.

Alisema tukio hilo halikubaliki hivyo kila aliyepewa jukumu la kulifuatilia ni lazima ahakikishe kuwa anafanya kazi kwa ufasaha ili majibu yapatikane haraka kuondoa shaka shaka kwa wanachi.

Kova alimtahadharisha Msangi kuwa, endapo atashindwa kutoa majibu ya kuridhisha basi atambue hata yeye itabidi awajibike ambapo alisema vitu kama hivi vikiachwa viendelee vinaliletea jeshi hilo sifa mbaya na kupoteza imani kwa wananchi.

“Pamoja na kumkabidhi kazi hiyo Msangi lakini hata mimi sitakaa kimya bali nitalifuatilia kwa karibu ili mradi tuwapatie wananchi ukweli”alisema Kova.

Alibainisha kuwa hawezi kupinga kama askari wanaweza kushiriki katika vitendo hivyo viovu bali suala hilo bado linahitaji ushahidi zaidi hivyo, ni vema wananchi wenye ushahidi wakatoa ushirikiano utakaosaidia kupatikana fedha hizo.

Aidha, Kova alilitaka jeshi la polisi kufanya kazi zake kwa nidhamu, uaminifu na ueledi kwani endapo ofisa au askari atakiuka maadili ya kazi yake, basi  hatua madhubuti zitachukuliwa dhidi yake bila kuchelewa.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza jopo hilo linaundwa na polisi wenyewe bila kushirikisha wadau wengine kwa madai kuwa, eti lifanya kazi kwa kutii sheria zote bila kwenda kinyume.