Watoto wa tano wa familia moja ambao ni walemavu wa viungo eneo la chome Wilayani Sama wakiwa kwenye picha ya pamoja. |
Familia ya
watoto watano wenye ulemavu Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wameomba jamii kujitokeza
kusaidia kutokana na ulemavu wa viongo
ambao umekuwa ukiwakabili kwa muda mrefu sasa, na kuwafanya kuishi katika hali
ngumu kimaisha.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mama wa watoto hao,Nirenjigwa Joseph alisema kuwa ana
watoto nane lakini kati yao watoto watano ni walemavu na mume wake Amini Joseph alifariki tangu mwaka 1992 na
baada ya hapo yeye ndo amekuwa akilelea familia hiyo.
Watoto hao
ni Joseph Amini( 38),Nafikahedi( 33) ,Wediel(30)
Gadison (28) na Julius(25)wote ni walemavu wa viongo ambao wanatembea kwa
kutambaa na wanahitaji kuwa na
muangalizi wakati wote kwa hakuna wanaloweza kufanya.
Watoto walizaliwa
wakiwa wazima lakini tatizo likaanzia kwenye kutambaa wakashindwa kusimama na tulijaribu
kupeleka hospitali na kuambiwa kuwa haitawezekana tena .
Kwa sasa
ukiwaangalia watoto hao tayari wameshakuwa wakubwa kabisa na changamoto kubwa
ni kwamba familia haiwezi kuwaacha kukaa pekee yao kwani wapo pia wakike na
jamii pia imekuwa na makusudio mabaya kwa wale wenye imani potofu juu yao au
wanaopewa maagizo ya imani za kishirikina.
“Baada ya
mume wangu kufariki nilikuwa nailelea familia mwenyewe na nilikuwa
najishughulisha na kilimo siku na kazi nyingine ya kufanya,lakini nashukuru
Mungu pia wapo watu waliojitoa kwa moyo lakini bado mahitaji ya kuwatunza ni
makubwa sana”Alisema mama huyo.
Mmoja watoto
wa familia hiyo ambaye ni kati ya watoto watatu ambao hawana tatizo la ulemavu
ambaye ni Mwalimu Chediel Amini (28)alisema kuwa wapo wafadhili ambao wamejitokeza kuwasaidia lakini bado tatizo ni
kubwa kwani nyumba aliyojenga bado inahitaji kumaliziwa.
Kikundi cha
utukufu kwa Mungu kupitia kwa Mwenyekiti wake Samweli Njau baada ya kutembelea familia hiyo walisema kuwa
watasaidia kufunga huduma ya maji pamoja na tenki la kuhifadhia maji ili kusaidia kuondoa tatizo la maji lilipo
kwenye familia hiyo.
Baada ya
kutembelea familia hiyo waliona kuwa jamii hiyo inahitaji kusaidiwa kwani
wanapoishi walemavu hao hakuna kivuli na wamekuwa wakitambaa kwenye jua na
kusumbuliwa na tatizo la funza hivyo kusaidia kuweka baraza kwenye nyumba
hiyo,ambapo wanasema msaada wao hautaishia tu hapo bali wataendelea kuhamasisha
na jamii nyingine.
Chediel
alisema kuwa anaomba watu wenye mapenzi mema kuweza kujitokeza kusaidia familia
hiyo kwa chochote watakachokuwa nacho ili kupunguza ugumu wa maisha ambao
wamekuwa wakiishi kutokana na familia kutegemea kilimo kuwalea watoto hao.
Kwa mawasiliano ya mmoja wa mtoto wa familia hiyo Chediel
Amini ambaye ndiye aliyebeba jukumu la kusaidia ndugu zake wenye ulemavu, simu 0654118385.
No comments:
Post a Comment