Thursday, December 20, 2012

MAMA SALMA NA HUDUMA ZA AFYA KWA WAJASIRIAMALI.

 

 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, (WAMA), Mama Salma Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma za Bima ya Afya kwa vikundi vya SACCOS vya UVIMA (Umoja wa vikundi vya WAMA Tawi la Majohe lililoko wilayani Ilala) na Salma Kikwete SACCOS kilichoko Mkuranga. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012 na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Afya Mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi (wa kwanza kushoto). Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya Mheshimiwa Deogratias Ntukamazina (katikati) na kulia ni Afisa wa WAMA ndugu Tabu Likoko akifuatiwa na Grace Michael, Afisa Habari wa Bima ya Afya.
Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete na viongozi wengine wakiangalia moja ya kadi ya mwanachama wa bima ya Afya mara tu baada ya kuzindua rasmi huduma ya bima hiyo kwa wajasiriamali wa UVIMA na Salma Kikwete SACCOS kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012.  Wengine katika picha kutoka kushoto kwenda kulia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa Dr. Husein Mwinyi, Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mheshimiwa Deogratias Ntukamazina na Mkurugenzi wa Mfuko huo Ndugu Emmanuel Humba.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akikabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa Bibi Tatu Ngao, Mwenyekiti wa UVIMA mara tu baada ya kuzindua rasmi mpango huo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012.

 
Waziri wa Afya Mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi akimpatia tuzo ya Shujaa wa mfuko wa Bima ya Afya kwa mwaka 2012 Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa WAMA kwa jitihada zake kubwa za kumkomboa mwanamke kiuchumi na kijamii na pia katika kupigania afya kwa wote na hasa makundi maalum katika jamii. Tuzo hiyo ilitolewa baada ya uzinduzi wa huduma ya Bima ya Afya kwa vikundi vya wajasiriamali wa UVIMA na Salma Kikwete SACCOS uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 20.12.2012.

(PICHA NA JOHN LUKUWI – MAELEZO -DAR ES SALAAM)

No comments:

Post a Comment