Wednesday, October 10, 2012

Rais Kibaki azuia mswada wa wabunge kujipatia marupurupu.



 Rais wa Kenya, Mwai Kibaki ameuzuia mswada wa sheria ambao ungewawezesha wabunge kujipatia marupurupu kiasi cha dola 110,000 watakapomaliza mihula yao ya kazi bungeni mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.
Uamuzi wa jana wa Kibaki ulifuatia kilio cha wananchi wakati nchi hiyo ikiwa imepandisha kodi zake kuziba pengo katika mahitaji yake ya fedha huku ikikabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi. Josephat Charo amekusanya maoni ya baadhi ya wakenya kuhusu uamuzi wa rais Kibaki.
(Kusikiliza maoni hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

No comments:

Post a Comment