WANANCHI WILAYANI HAI WALIA NA WIZI WA PEMBEJEO ZA KILIMO
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Hai Novatus Makunga. |
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Hai Mjini Wilayani
Hai wamelalamikia upotezo wa vocha 135 zenye dhamani ya zaidi ya shilingi
million 9 ambazo zilikuwa zigawanywa kwa wakulima wa kata hiyo.
Wakizungumza na Dira ya Leo mwenyekiti wa mtaa
wa gezaulole kwenye kata hiyo Simon Mnyampanda amesema kuwa kwenye kikao cha
WDC cha tarehe 06/03 walisomewa agenda kuu ambayo ilikuwa ni vyocha za
pembejeo ambazo mtendaji alisema kuwa kata hiyo imepata vocha 550.
Amesema kuwa hoja ya idadi hizo za vocha
iliyosomwa na Mtendaji wa Kata hiyo Neema Lema iliungwa Mkoni pia na Diwani wa
kata hiyo jafar kiure,ambapo baada ya kufuatilia idadi iliyotolewa na Serikali
kwenye Kata hiyo kutoka Serikalini ni vocha zipatazo 685.
Hata hivyo dira ya leo imewasiliana na
Mwenyekiti wa vocha kwenye kata hiyo Abuu Kimaro hakupenda kutoa ushirikiano
kuhusiana pamoja na afisa mtendaji neema lema baada ya kupiga simu zao za
mkononi bila kupatikana.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halm ya hai
Melkizedeki humbe alisema kuwa hana taarifa ya wizi huo wa vocha za
pembejeo,huku akisema suala hilo atalifuatilia.
Naye diwani kata ya mjini jafari kiure
alipoulizwa kuhusiana na upotevu huo wa vyocha alisema yeye hausiki kwenye
kutoa taarifa ya vocha kwa sababu siyo
mtendaji,ila kama kuna udanganyifu ni suala la kuhoji,huku akisema hafahamu
idadi ya vocha zilizogawanywa kwenye kata yake .
Hata hivyo dira ya leo ilifanikiwa kuinasa
barua iliyokuwa im etoka halm ya hai ambayo ilikuwa inahusu mgao wa vocha za
pembejeo kwa mwaka 2011/12 kuonesha kuwa idadi ya vocha ni kwenye kata hai ni 685.
No comments:
Post a Comment