Tuesday, March 20, 2012

Rungu la NEC laiangukia CCM,CHADEMA   

TUME ya Taifa Uchaguzi kupitiakamati ya Maadili imevionya vyama vya CCM na CHADEMA kutokana na kukiukataratibu za uchaguzi ikiwemo kutumia lugha za matusi na kuchana picha zawagombea.

Akitangaza uamuzi huo kwawaandishi wa habari  jana Msimamizi waUchaguzi wa Jimbo la Arumeru Trasias Kagenzi, alisema kutokana na matukio hayokamati hiyo ya maadili ilipokea malalamiko kutoka kwa vyama vya Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambapo kila chamakilalamika kufanyiwa fujo.

Alisema katika malalamiko hayoyaliyowasilishwa Machi 13, mwaka huu NEC ilipokea barua za malalamiko kutokaCHADEMA ambapo waliishutumu CCM kwa kutumia wafuasi wake kung’oa picha za mgombeawa ubunge wa chama hicho Joshua Nassari katika eneo la Usa River.

Kagenzi alisema Machi 18 mwakahuu nacho Chama Cha Mapinduzi (CCM),  iliwasilisha malalamiko katika ofisi yakedhidi ya CHADEMA kwa kushambulia msafara wa mgombea wa CCM katika eneo la MeruGarden na kuharibu gari namba T655 BEW ambapo tukio hilo lilipotiwa Polisi kwahatua zaidi.

“Kamati ya maadiliinakutanisha vyama vyote vinavyogombea na baada ya kupitia kwa kina malalamikohaya na tumalazimika kutoa maamuzi kwa vyama vya CCM na CHADEMA kutokana nakila chama kuwa na kosa.

“Kabla ya hapo malalamikokutoka CHADEMA yaliyokuwa manne na CCM yalikuwa mawili, kwa hatua hii kamati yamaadili inavitaka vyama vyote vya siasa kufuata sheria na utaratibu za uchaguziikiwemo kutangaza sera na sio kutumia lugha za matusi na kebehi aidha kwamgombea wa chama husika au wapambe wake.

“Vingozi wa vyama vya siasapamoja na wagombea wa Ubunge endapo watakiuka sheria hii ya uchaguzi basiwatapewa adhabu kwa mujibu wa sheria za uchaguzi ikiwemi kutozwa faini ya Sh.50,000 hadi 100,000 na kama ikibainika zaidi hata ikiwezekana mgombea aukiongozi naweza kuizuiliwa asishiriki kampeni za uchaguzi,” alisema Kagenzi.

Aidha alisema kutokana nahatua hiyo kesi zote za jinai zilizowasilishwa Polisi zitaendelea kushughulikiwakwa mujibu wa sheria na NEC haitaweza kuziingilia.

Akizungumzia maandalizi yauchaguzi, msimamizi huyo alisema hivi sasa NEC ipo katika mpango wa kutoa elimukwa wapiga kura ikiwemo kuhakikisha wanatunza shahada zao.

“NEC imeandaa kutoa elimu yauraia kwa wananchi wa jimbo la Arumeru ikiwemo kutunza shahada zao nakuhakikisha wanajitokeza kuoiga kura. Elimu hii itawasaidia kujua haki zao.

“Naomba ielewekea fomu namba17, hailalishi kuwa ndiyo kitambulisho cha kupigia kura nah ii hutolewa kamakiapo na endapo itabainika mpiga kura amedanganya katika hili NEC itamchukuliahatua kali za kisheria ikiwemo ya kumfikisha mahakamani,” alisema msimamizihuyo wa Uchaguzi.

Kampeni za uchaguzi  mdogo katika jimbo la Arumeru Mashariki,zilifunguliwa  rasmi Machi 9, mwaka huuambapo vyama mbalimbali vya siasa vinaendelea kupiga kampeni zake huku matukioyangu uvunjifu wa amani yakianza kujitokeza.

Machi 19, mwaka huu Mwenyrkitiwa tawi la Magadirisho Kata la Usa River, Nuru Maeda, wa Chama Cha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA), alitetekwa na watu wanaosadikiwa kuwa vijana wa ChamaCha Mapinduzi (CCM).

Mwenyekiti huyo alikutwa namkasa huo juzi  asubuhi alipokuwa akipitakuhakiki wanachama wa CHADEMA waliojitandika katika daftari la kudumu la wapigakura, ambapo  alivamiwa na viongozi waCCM na kupelekwa katika kambi ya mateso ambapo alidhalilishwa kwa kupigwa nakubanwa sehemu zake za siri.

Akizungumzia tukio hilo Mkuuwa Oparesheni wa Uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki Naibu Kamishna wa Jeshila Polisi Isaya Mngulu, alisema mara baada ya kutokea tukio hilo watuhumiwawametambuliwa kwa jina moja moja ingawa hakuwa tayari kuwataka ili kuwezakupisha taratibu za uchunguzi kuchukua mkondo wake.

“Ni kweli tumepokea tukiohilokutokana juhudi zilizofanywa na jeshi la Polisi tumefanikiwa kuwabainiwatuhumiwa kwa jina moja moja na hivi sasa askari wetu wamengia katika doriaili kuweza kuwakamata.

“Siwezi kuwataja kwamajina  kwani kfanya hivyo unawezakusababisha wahusika wakatoroka, nasi kazi yetu ni kuhakikisha ulinzi nausalama unaimarika kuanzia katika kipindi hiki cha kampeni hadi siku yauchaguzi Aprili Mosi Mwaka huu,” alisema Kamishana Mngulu.
Na Mwandishi Wetu Arumeru

No comments:

Post a Comment